Kwa waliokojoa kitandani tu!!

Kwa waliokojoa kitandani tu!!

Aiseeee nimecheka sana, kuna siku nilikunywa maji sana(napenda maji tangu mtoto) ila nilikuwa najiepusha kunywa maji mengi usiku. Sasa hiyo siku tukawa tunafanya mashindano ya kunywa maji na kaka yangu. Nikanywa maji hadi tumbo likauma.

Nikalala na mama siku hiyo, usiku nikaota nakojoa kichakani kumbe nakojoa kitandani, nilistuliwa tu na kofi na mama. Yaani asubuhi ni full kuchekwa. Since that day nikawa makini sana kutokunywa maji mengi usiku.
Ntautafuta tushindane kunywa maji dada espy
 
kukjoa ktandan hakukuwai kumuacha mtu salama. mi nlkjoa ugenini nlpstuka ckjua ni saa ngap ila ckulal tena mpk asubuhi nltamn kua mchawi ili niukaushe mkojo kichawi.[emoji56][emoji56]
😀😀😀😀😀😀
 
Weeee, huu mchezo hauhitaji hasira, nakumbuka mimi na bwana mdogo ( enzi hizo sasa hivi tu maofsa flani hivi usihoji) tulikuwa vikojozi mbayaa, kama mibakora tullichezea sana tu, tukaibuka na mbinu ya kulala kwa zamu aaa wapi ikafeli, tukaibuka na mbinu mpya, tunaongoa matandiko ( godoro anasa) tunajaladia asubuhi tuaamka na kurudishia mchezo unasonga, tena kwa mbwembwe tu natangaza tumeacha ukojozi, ngoma alikuja mgeni weee asubuhi ilitembea fimbo mbaya, nilisahau kukojoa kila nikikumbuka kipigo, tulimpiga mande kalowa chepe chepe.
😀😀😀😀
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Kweli we noma, kwahiyo dogo alikuwa anachapwa kwa kosa lako!!
Kuna walianza ukatili wakiwa wadogooo, halafu anamfanyia bro wake.Huyo bro wake atakua alikua hajui inakuaje akojoe...
 
Mi nilikuwa mtundu sana and so nilikuwa nalala kama nimekufa..! Mkojo ulikuwa unanitoka bila ya kuota..! Dawa ilikuwa kulala mchana.. yaani nikilala mchana sikojoi nikisema nicheze mpaka jioni basi usiku lazima nilimwage
 
Nazani kwa sisi wote humu ndani hiyo laza hakuna ambae haja ionja nilikuwa nakeleka sana ninapo amka nimelowa
 
Nimekojoa sana sitaki.hata kujiwazia kuna kipindi hadi kuingia kulala naogopa basi natafuta nguo nazikusanya naziweka eneo la godoro nyingii ili nikikojoa nguo ndio zilowe na sio godoro, nikibahatika kuamka usiku napelek mkono kwenye godoro taratibu nijue kama nimeharibu
Nakuta sijaharibu, sasa kosa nikilala tena uhiii asubuhi mkojo mtupu.kwenye nguo, kuamka nashindwa naendaje kufua, uzuri mmoja nilikwa sipigwi nikikojoa ila kugombwa sasa uhiii nalia mapema,
Nilikuwa nasal sala zote nisikamatwe hapo.
Natoaje godoro nje kimbembe,
Siku nyingine nakojoa naenda shule lakin huko shule hapakaliki nawaza home lile godoro bibi akiingia si balaa, na bibi yangu kupiga alikuwa anajua haswAa sema alikuwa anamuhofia babu,

Utakuta narudi home nakuta godoro nje limeanikwa unajua kuwa na was was wa kusemwa, sasa ubaya wa bibi yangu ni mtu.wa kuweka vitu ndani siku ukifanya kosa tu ataunganisha yoote hadi kukojoa hasem ila nikawa naelewa tu.
Kwetu tulikuwa tuna utaratibu mnakula mapema baada ya muda mnapiga magoti mmoja anasali.
Na mimi katika sala zangu zote nilikuwa namwambia Mungu nisaidie niache kukojoa na mimi hata.kwa siku 100, siku 1000, yan nilikuwa nasema kwa miaka 100, miaka 1000 ,nisikojoe Mungu nisaidie nilikuwa mdogo hii ilikuwa std 2 had 3
It was serious bsnes prayer to my God. Nilikuwa naona aibu mnoo katoto kazuri halafu nakojoa too bad nimekojoa muda mrefu had la 4, huku la 4 ilikuwa naweza kaa hata miez 6 sikojoi mwanzoni. Jmn kukojoa ni aibuu ah ah ah sitak kuwaza mimi utoto

Basi utakuta watoto wengine wanasema ukiangalia mwez usiku unakojoa, ukihesabu nyota unakojoa,
Sasa mm ikifika usiku sithubutuu kuangalia juu. Kuogopa kulowanisha godoro

Nimekunywa maji.ya mchele mimi.aha ah ah uhii, bibi yangu alikuwa ananiambia kunywa ili usikojoe , na kwel siku ninayo kunywa sikojoi,

Naambiwa na dada yetu wa ndani panda juu ya mti ukojoe mimi huyo mtoto.wa kike paramia mti nakojoa juu ya mti ah ah naandika huku nacheka hapa.

Vuta picha mchana kweupe upande kwenye mti ukojoe jmn uhii acheni ile karaha.
Na hapi ukinikuta nimeogoa vzr sinuk hata mkojo utajua kama mm kikojozi

Ingiaa room sasa uhii harufu kali ajabu.
Acheni hili suala watu wametoka mbali

Hapo enz hizo baba yangu alikuwa anasafiri tu, akija kwa mama yake hapo utasikia yan sisafir na wew utanitia aibu bure kukojoa kwako roho inaniuma bas naachwa home kisa nakojoa
Kali sasa siku mchana kweupeee nimelala si nikakojoa, wee baba yangu mdogo kaja wrwe kwanini umekojoa? Kashika fimbo nililiaa nikasema nimeotaaa mama kafa ndio maana nikakojoa
Jamn baba yangu mdogo alichekaa fimbo.alitupa akasema aisee hii lazima nikaiandike ktk diary yangu
Kumbe mwenzio niliota nakojoa nikaliachia kitandani uhiii.
Ulivyoandika nimekuonea huruma utafikiri ni jambo limetokea leo.Pole sana.
 
Umenichekesa sana eti tulimpiga mande mgeni kama yupo shamba la irrigation maana hapo lazima utoboze chini.

Sent from my SM-J200F using JamiiForums mobile app
We acha tu, deibii tumesepa yeye atatokaje[emoji1] [emoji2] [emoji2] [emoji13]. MAMA alikuwa shujaa wetu manake alitunyuka all time we what? We irrigate our bedroom.
 
Back
Top Bottom