Kwa waliomaliza form 4, kama una roho ndogo usiende kusoma special schools (shule za vipaji maalumu)

Kwa waliomaliza form 4, kama una roho ndogo usiende kusoma special schools (shule za vipaji maalumu)

Imagine natoka kibaha nakuja kupiga kipindi mchikichini kwa mudi physics (rip) ticha

Nilipiga division 4 o level lkn leo mimi ndo yule ambae matangazo yote ya mpira kutoka azam tv hayaendi hewani bila mimi kuhusika kwa asilimia 95%.

Sent from Tesla device phone
Kongole mkuu, maisha ni fumbo! Kuna kitu Mungu alishakuandalia.

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Advance unaenda unafundishwa na mtu lakini mwisho wa siku unakuja kumzidi kila kitu..

Kuna mwanangu alinipiga msasa Mechanics topics zote lakini akaja kuishia kupata three ya mwishoni..iliniuma sana hii.

Kwahiyo vijana wasiogope
Huyo alisoma na akajiamini sanaaaa!! Nahisi hivyo

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Wengi waliopiga One form six miaka ya 2010 kurudi nyuma wana maisha safi... wengi wapo vitengo vizuri wanakula mema ya nchi. Darasa nililomaliza nalo chuo kwa kozi niliyokuwa ninasoma nadhani zaidi ya 35% wako TRA. Tulikuwa kama 40 tu kwenye kozi yetu. Hawa vijana wa sasa wanafanya vizuri sana kitaaluma kwenye CSEE na ACSEE ila watakumbana na changamoto kubwa sana hata kupata sehemu ya field. Huko tuendako watu watakuwa na ONE kali za f4 na f6 huku wakiwa hawana kazi au wanafanya kazi za kuzuia tu msiba. Maendeleo huja na changamoto.
Ni changamoto sanaa kwa kweli!!

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Practical za physics aisee nilikua nazifoji mpaka sio poa
Mkuu hii michezo ipo sana advance ,ndio maana scientist wengi kibongo bongo hawawezi kuwa inventive,maana kiukweli hawajazoea kushika vifaa,kufanya setup na kupata majibu ,kitu ambacho dunia ya sayansi ndio inataka sasa
Mtu kamaliza PCM ana vibanda vya kutosha ,lakini anaogopa sakiti za umeme wa majumbani,bila kishoka hatoboi

Sent from my TECNO BE6 using JamiiForums mobile app
 
Hizi shule(mzumbe,pugu,kisimiri,ilboru,kibaha and the likes) japokua siku izi nyingi zimepoteza sifa zake aisee kama una moyo mwepesi usiende huko unaweza kupata depression au pressure ukashindwa kusoma

Miaka Hio mwisho wa miaka ya 2000 niliripoti Moja ya shule tajwa hapo combination ya pcm... Kipindi hicho special school wamejaa watoto wa dar kutoka (kibaha, Azania, pugu) aisee Hawa madogo wana sifa kishenzi.... Mtu anakuja kuripoti form 5 ameshamaliza topic zote za form 5 anakaribia kumaliza za form 6

Sasa si matozi tulivyomaliza form 4 vitabu tukatupa Kule mpaka siku ya kuripoti hujawahi kupiga pindi lolote... Unakutana na vitoto vimesoma sijui mchikichini huko aisee wamefuta topic zote, aisee nilipata presha sana mpaka kuzoea ile Hali.... Nakuta madogo wanapiga integration kama hawana akili, ukikaa bwenini wanaulizana kwa nguvu reaction za organic. Chemistry huko....

Dah yaani mwezi wa kwanza form 5 watu wanasolve necta review nikasema hapa nimeyatimba... Aisee ile presha ya ku catch up nilipata shida Sana sio Siri... Ukiwa na roho nyepesi unaweza kukata tamaa Moja kwa Moja

Kuna dogo tumeingia form 5 alikua anaitwa T.O (Tanzania one) alitukimbiza wote form 4 aisee huyu Jamaa mpaka Leo hua namuogopa. Hua namwambia hata hii kazi ya u engineer unayofanya unastahili kua somewhere else una potential kubwa sana, picha linaanza tumeingia form 5 hapo.... Sasa form 6 walikua wanafanya fitness tests (hii anatokea mwanafunzi mmoja au wawili wanatunga mtihani alafu wengine wanafanya japo sio lazima)

Ujinga wa hii mitihani wanafunzi wanajua kukomoana yaani maswali yote unakuta ya kibabe... Kuzungusha 0 huku ni kawaida tu ndo maana wengi walikua hawataki huu ujinga, dogo bana tunafika form 5 kaskia form 6 wanafanya fitness test ya physics dogo akazamia akapiga Pepa... Matokeo yanatoka form 6 karibu wote wamefeli dogo kawakimbiza.... Wote wanaulizana hili jina nani mbona hatumjui... Kuja kuulizia wakaja kugundua ni dogo wa form 5 aisee jamaa walimind kinoma akapigwa marufuku kabisa kusogeza pua kwenye fitness tests za form 6

Huyu dogo tulipofika form 6 sidhani kama aliwahi kukaa akasoma, jamaa alikua anakaa zake class watu wamepanga foleni na maswali Yao yaliowashinda dogo anapiga yote tu hajali kama ni ya physics, chemistry, pure au bam ye anasolve tu. Alikuja kua Tanzania one tena form 6 jamaa walimtangaza hesabu paper 1 na 2 zote alipiga 100%.

Huku kama una roho ndogo sio pa kwenda mi nusura panishinde nilitaka nirudishe mpira kwa kipa(kuhamia private)
Pugu nayo ni special school?
 
Kuna watu walienda shule kusomea kijiji...yani kuna dada namkumbuka alikua anasoma mpk akapinda mgongo kila ukikutana nae yuko speed..kula anakula kama anafukuzwa awahi kusoma..siku hizi ni daktari wa macho...
Bidii yake imemzalia matunda
 
... huko ndipo hasa pa kuenda! ... we ukienda kuwa wa kwanza miongoni mwa super-vilaza si unataka kuambulia zero ya form six!!!1?
😅
 
Imagine natoka kibaha nakuja kupiga kipindi mchikichini kwa mudi physics (rip) ticha

Nilipiga division 4 o level lkn leo mimi ndo yule ambae matangazo yote ya mpira kutoka azam tv hayaendi hewani bila mimi kuhusika kwa asilimia 95%.

Sent from Tesla device phone
Mkuu hiyo Tesla device phone ime toka lini 😄😂😂🤣.
 
Back
Top Bottom