Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ulikua unaibia sio?Mimi ujuzi wangu wa Kuzungusha shingo kwa haraka sana na kukusanya majibu ulinifikisha mbali sana.
Masomo ya Arts labda..Sijaona sababu ya msingi ya kwenda advance mpaka sasa
Dah kitambo sana mkali , sema nini navutika PM ila mashine ya Mello inanikataa .MWANANGU NIPO TOWN NAUNGA UNGA MWANA NIPE CONNECTION AZA BOY KITAMBO [emoji2935]
Safi kabisaImagine natoka kibaha nakuja kupiga kipindi mchikichini kwa mudi physics (rip) ticha
Nilipiga division 4 o level lkn leo mimi ndo yule ambae matangazo yote ya mpira kutoka azam tv hayaendi hewani bila mimi kuhusika kwa asilimia 95%.
Sent from Tesla device phone
Poleni sanaaa, Form IV ya 2012 na Form VI ya 2013 zilikumbwa na dhoruba kali kama Covid 19!Nina washkaji zangu wakali wa mathematics mwaka huo waliondoka na C ,hata ndegeulaya alipiga C ,ule mtihani wa mwaka 2013 ulikuwa wa laana aisee , Tanzania nzima A za advance mathematics zilikuwa 12
Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
Vijana wa siku hizi!!! "Eti pure mathematics"..... ni Advanced mathematics. Hakuna somo la mathematics A level katika combinations za PCM, PGM na EGM linaloitwa pure mathematics. Hiyo pure maths ni hesabu tu katika Advanced maths. NB: mimi nimesoma PCM miaka kadhaa ya nyuma.Umenikumbusha kijana mmoja anaitwa Rajabu ndegeulaya.
Tuna report advance Azania yeye alipitisha tangazo la kuwa anafundisha tuition Kwa WANACHUKUA PHYSICS, CHEMISTRY NA PURE MATHEMATICS.
WATU walizani ni form six kumbe ni form five alishamaliza topic zote mpaka za six basi ikabidi tuendelee kupiga mapindi kwa Ndegeulaya.
Kwa masomo ya arts ni kupoteza muda Ila sayansi hasa PCM siyo level ya kuiruka.Elimu ya kidato cha tano na Sita ni ya kupoteza muda tu. Binafsi nimeipitia kwa sababu sikuwa na taarifa sahihi za kujitosheleza.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787], daaah!! Hatari sanaaYaani mi nilikua nikishapata pilot test natupa mavifaa Yao Huko yaani hapo practical imeisha.....
Mwaka wetu kemia practical ya titration tulifanya mpaka jasho likatoka, ngoma haibadiliki Wala Nini... Mpaka jamaa mmoja akaropoka 'huu ni ujinga' watu wakacheka, msimamizi anauliza Nini watu wakamwambia mbona hii practical Kila mtu inamgomea, wakamtafuta teacher wa kemia kaja kujaribu ikamshinda... Kumbe Hawa kenge walileta chemical sijui za wapi bana, ikabidi msimamizi aandike ripoti kuhusu Hilo swala tukaambiwa tuachane na Hilo swali... Wajinga sijui kama walitupa marks zetu
Not pure mathematics ni Advanced mathematics.Alikua headboy wangu MKUU nimesoma nae O level na Na advance nimepiga nae yeye alipiga PCM Mimi nilikua napiga EGM tulikua tunakutana kwenye Pure mathematics.
Ni Advanced mathematics siyo pure mathematicsNina washkaji zangu wakali wa mathematics mwaka huo waliondoka na C ,hata ndegeulaya alipiga C ,ule mtihani wa mwaka 2013 ulikuwa wa laana aisee , Tanzania nzima A za advance mathematics zilikuwa 12
Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
Kuna dogo Alisoma ilboru nadhani alimaliza 2011 kama sikosei ana asili ya kiarabu/mhindi alifanya hizo Pepa zote 4 sijui kwa kusimamiwa mwenyewe au vipi, ikitokea bahati mtu alipita hapo huu mwaka atakuja kuelezea... Alikua anasoma pcbmHaiwezekani siku ya pure ndiosiku ya bam.hapo umetupiga fix🤣🤣🤣🤣🪑💺
.Wanafunzi pia hawapendi kufundishwa wanaona kama wanapotezewa muda tu... Tulikua na mwalimu wa chemistry jamaa alikua anafundisha shule mbili za private huku kaajiriwa serikali
Jamaa ukiacha practical sidhani kama aliwahi hata kutufundisha, alikua mtu wa vyombo alikua anakuja class tunapiga nae story tu za mademu[emoji2][emoji2]
Au alikuwa mtu wa system?Kuna dogo nyuma yetu alikua anasoma pcbm.... Yaani physics, chemistry, biology na pure mathematics.... Na bam juu nikawa namwambia ikifika necta utakataliwa kufanya mtihani wa pure mathematics maana hawawezi ruhusu usome masomo manne, aisee sijui ilikuaje nilikuja sikia aliruhusiwa kufanya mitihani yote
Wataalam hapa watatusaidia
.Yaani mi nilikua nikishapata pilot test natupa mavifaa Yao Huko yaani hapo practical imeisha.....
Mwaka wetu kemia practical ya titration tulifanya mpaka jasho likatoka, ngoma haibadiliki Wala Nini... Mpaka jamaa mmoja akaropoka 'huu ni ujinga' watu wakacheka, msimamizi anauliza Nini watu wakamwambia mbona hii practical Kila mtu inamgomea, wakamtafuta teacher wa kemia kaja kujaribu ikamshinda... Kumbe Hawa kenge walileta chemical sijui za wapi bana, ikabidi msimamizi aandike ripoti kuhusu Hilo swala tukaambiwa tuachane na Hilo swali... Wajinga sijui kama walitupa marks zetu
Acha kuwatisha vijana, hakuna cha ajabu hukoHizi shule(mzumbe,pugu,kisimiri,ilboru,kibaha and the likes) japokua siku izi nyingi zimepoteza sifa zake aisee kama una moyo mwepesi usiende huko unaweza kupata depression au pressure ukashindwa kusoma
Miaka Hio mwisho wa miaka ya 2000 niliripoti Moja ya shule tajwa hapo combination ya pcm... Kipindi hicho special school wamejaa watoto wa dar kutoka (kibaha, Azania, pugu) aisee Hawa madogo wana sifa kishenzi.... Mtu anakuja kuripoti form 5 ameshamaliza topic zote za form 5 anakaribia kumaliza za form 6
Sasa si matozi tulivyomaliza form 4 vitabu tukatupa Kule mpaka siku ya kuripoti hujawahi kupiga pindi lolote... Unakutana na vitoto vimesoma sijui mchikichini huko aisee wamefuta topic zote, aisee nilipata presha sana mpaka kuzoea ile Hali.... Nakuta madogo wanapiga integration kama hawana akili, ukikaa bwenini wanaulizana kwa nguvu reaction za organic. Chemistry huko....
Dah yaani mwezi wa kwanza form 5 watu wanasolve necta review nikasema hapa nimeyatimba... Aisee ile presha ya ku catch up nilipata shida Sana sio Siri... Ukiwa na roho nyepesi unaweza kukata tamaa Moja kwa Moja
Kuna dogo tumeingia form 5 alikua anaitwa T.O (Tanzania one) alitukimbiza wote form 4 aisee huyu Jamaa mpaka Leo hua namuogopa. Hua namwambia hata hii kazi ya u engineer unayofanya unastahili kua somewhere else una potential kubwa sana, picha linaanza tumeingia form 5 hapo.... Sasa form 6 walikua wanafanya fitness tests (hii anatokea mwanafunzi mmoja au wawili wanatunga mtihani alafu wengine wanafanya japo sio lazima)
Ujinga wa hii mitihani wanafunzi wanajua kukomoana yaani maswali yote unakuta ya kibabe... Kuzungusha 0 huku ni kawaida tu ndo maana wengi walikua hawataki huu ujinga, dogo bana tunafika form 5 kaskia form 6 wanafanya fitness test ya physics dogo akazamia akapiga Pepa... Matokeo yanatoka form 6 karibu wote wamefeli dogo kawakimbiza.... Wote wanaulizana hili jina nani mbona hatumjui... Kuja kuulizia wakaja kugundua ni dogo wa form 5 aisee jamaa walimind kinoma akapigwa marufuku kabisa kusogeza pua kwenye fitness tests za form 6
Huyu dogo tulipofika form 6 sidhani kama aliwahi kukaa akasoma, jamaa alikua anakaa zake class watu wamepanga foleni na maswali Yao yaliowashinda dogo anapiga yote tu hajali kama ni ya physics, chemistry, pure au bam ye anasolve tu. Alikuja kua Tanzania one tena form 6 jamaa walimtangaza hesabu paper 1 na 2 zote alipiga 100%.
Huku kama una roho ndogo sio pa kwenda mi nusura panishinde nilitaka nirudishe mpira kwa kipa(kuhamia private)
.Organic chemistry shikamoo, Kuna dogo aisee alimeza organic yaani akawa kama kichaa anatembea anaongea mwenyewe maswala ya chemical reactions tu[emoji2]
Kilaza namba moja ni kutokuwa na pesa tuVilaza huwa mnapenda sana kutisha watu!