Kwa waliomaliza form 4, kama una roho ndogo usiende kusoma special schools (shule za vipaji maalumu)

Kuna muda data unapika ukishajua range inaendaje...ukishaangalia pilot test iko aje unaweza kupika za chini...
 
Zamani kulikua na spirit sana unakuta wababe wote wa hesabu, au labda physics wanajulika kwa majina hata kama husomi nae habari utazipata tu
 
Hizi shule(mzumbe,pugu,kisimiri,ilboru,kibaha and the likes) japokua siku izi nyingi zimepoteza sifa zake aisee kama una moyo mwepesi usiende huko unaweza kupata depression au pressure ukashindwa kusoma
Kupoteza sifa kivipi mkuu wakati sasa hivi zimeongeza ufaulu kuliko miaka hiyo. Fuatalia matokeo yaliyotoka leo halafu linganisha na enzi zako. Kuna 1.7 zaidi ya 40 kwenye shule moja hizi za Kibaha , Mzumbe na Ilboru wakati enzi zako idadi hiyo ilikuwa kwa Tanzania nzima. Hizo shule bado zinapiga sana halafu ni kwa msuri wa kujitegemea.

Ila umenifurahisha kwenye kukata topick halafu ukaingia mtupu lazima uscore mswaki mpaka ukae sawa umepitia magumu. Jambo la msingi ilikuwa ni kuhakikisha uko miongoni mwa wanafunzi 100 waliopata division 1 maswala ya u T.O unawaachia wakina E. G na E.K and company[emoji1787]
 
Kuna muda data unapika ukishajua range inaendaje...ukishaangalia pilot test iko aje unaweza kupika za chini...
Yaani mi nilikua nikishapata pilot test natupa mavifaa Yao Huko yaani hapo practical imeisha.....

Mwaka wetu kemia practical ya titration tulifanya mpaka jasho likatoka, ngoma haibadiliki Wala Nini... Mpaka jamaa mmoja akaropoka 'huu ni ujinga' watu wakacheka, msimamizi anauliza Nini watu wakamwambia mbona hii practical Kila mtu inamgomea, wakamtafuta teacher wa kemia kaja kujaribu ikamshinda... Kumbe Hawa kenge walileta chemical sijui za wapi bana, ikabidi msimamizi aandike ripoti kuhusu Hilo swala tukaambiwa tuachane na Hilo swali... Wajinga sijui kama walitupa marks zetu
 
Ukapika data zinazokaribia na uhalisia. Walimu wa hizo shule wandundisha mbinu za kufaulu mitihani pia kuhakikisha unamaliza kwa muda muafaka kisha urejee kuokoteza marks kuitafuta A au B [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kuna mwaka niliangalia top 10 za matokeo ya form 6 nikazikosa kibaha, ilboru,mzumbe yaani kisimiri na tabora boys ndo zilikuwepo nilisikitika sana
 
Hata mwaka wetu ilikua very slow hasa ..sema ilileta majibu muda umeenda..hapo ndo mpiko wa data ulifanyika kiufasaha maana hakuna namna muda ukiisha huwezi ongezewa...
 
mie nilipewa bichwa naweza hesabu nikaenda pcm...weee .kemia hadi leo.sielewagi kitu..😏...physics ni formulas tu ziwe akilini na ubongo uwe twisted kila mara....kemia shikamoo..sijui matitration...pyee
 
mie nilipewa bichwa naweza hesabu nikaenda pcm...weee .kemia hadi leo.sielewagi kitu..😏...physics ni formulas tu ziwe akilini na ubongo uwe twisted kila mara....kemia shikamoo..sijui matitration...pyee
Organic chemistry shikamoo, Kuna dogo aisee alimeza organic yaani akawa kama kichaa anatembea anaongea mwenyewe maswala ya chemical reactions tuπŸ˜ƒ
 
mie nilipewa bichwa naweza hesabu nikaenda pcm...weee .kemia hadi leo.sielewagi kitu..😏...physics ni formulas tu ziwe akilini na ubongo uwe twisted kila mara....kemia shikamoo..sijui matitration...pyee
Mziki ulikua kwenye Organic Chemistry mwalimu wetu alikua muhaya yani anavyoongea huwezi muelewa vzr...aisee somo nililichukia...chemstry ni nomaa....mimi nilikua nakomaa na paractical aisee..
 
Miaka ya tisini tulikuwa tunazungumzia Mzumbe, Ilboru, Kibaha na Tabora Boys (kwa wavulana), na Kilakala, Tabora girls na Msalato (kwa wasichana). Kumbe wenzetu mkaja kuongezewa na "pugu, kisimiri, and the likes"!!! No wonder bado najiuliza hii kauli ya "Miaka Hio mwisho wa miaka ya 2000 niliripoti..." inamaanisha nyakati zipi!!
 
na ifunda tech mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…