Kwa waliomaliza form 4, kama una roho ndogo usiende kusoma special schools (shule za vipaji maalumu)

Nilienda nimechelewa nikakuta hao mabongoland wamesharipoti wameshamaliza topic zote

Nikataniwa niandike electronic configuration Mimi akili yangu nikawa natumia zile za o level 2:8:8 walicheka balaa mambo ya orbitals ,Wala vi theory vya aufbau , Pauling exclusion sijui kama zipo

Majamaa yakawa yanadhusha ma theory ya electro chemistry na ma reaction ya delocalization za benzene na Ortho and para kwenye organic nilitaka kulala mbele nimwbie mshua anipeleke shule za arts
 
mimi wakati naripoti 4m five nilikutana na the same issue but ki ukweli maisha haya ni kuomba sana wakati unapambana .Unaweza kuwa best darasani but ukaja kupata kazi ya kawaida sana
 
Útakuta mtu amemeza Lambert na Abbott zote.
 
Inanikumbusha enzi zetu Singida tuliomba tufanye mock na ma form six Sema walitubania.
Nakumbuka ticha wa chemistry alikua akiingia darasani anajitetea kabisaa eti hatufundishani bali tunadiskass! Dadeki. Watu tulimeza topic zote za five kwa mkandawire. Ile elimu nyoko niulize saivi nna mbishe gani.
 
Mtanzania pekee aliyekuwa T.O O-level na Advanced level ni Martin Chegere,Akaenda mlimani akawa best student,masters akaongoza,PhD Sweeden pia akaongoza!
now yuko Udm anapiga madogo pindi.
 
Mtanzania pekee aliyekuwa T.O O-level na Advanced level ni Martin Chegere,Akaenda mlimani akawa best student,masters akaongoza,PhD Sweeden pia akaongoza!
now yuko Udm anapiga madogo pindi.
Nikajua atakuwa Harvard, oxford, Cambridge anafundisha au kaajiriwa TESLA , google na makampuni makubwa ila kaishia UDSM ,duu basi hatari sana

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Mtanzania pekee aliyekuwa T.O O-level na Advanced level ni Martin Chegere,Akaenda mlimani akawa best student,masters akaongoza,PhD Sweeden pia akaongoza!
now yuko Udm anapiga madogo pindi.
Huyu niliyesoma nae alikua T.0 o level na advance pia... Yaani alivyokuja advance akawa anaitwa T.O nadhani Kuna watu hata jina lake walikua hawalijui

Mwaka wetu top 10 jamaa ndo aliongoza huku hao Tisa wote waliobaki wakiwa mademu tupu, kipindi hicho kifungilo na Marian girls weka mbali na watoto
 
Haha jamaa umenikumbusha jina mmenye..... Vipi ulipita hapo nikupe 1,2,3 za hapo?

Ndio lakini sio miaka uliyotaja, nyuma kidogo...

Afu usikariri, si mwaka wetu Kuna watu wawili walipata div 4... Sio kwamba special school Kila mtu anatoboa chief

Waliokuwa wanapata ufaulu hafifu ni wale waliokuwa...
1. Waoga kama wewe

2. Mabitozi na wapenda starehe

3. Wasukuma na Wakurya ambao kuja kwao shule za mjini kuliwafanya wajihusishe na shughuli za kuwaingizia kipato (kukusanya ada), mfano hapo umenyeni kulikuwa na jamaa mpiga picha maarufu alikuwa hadi na baiskeli, anakula deal za kupiga picha shule kibao kuanzia Ngateu, Kiding'a, Enaboishu hadi Akeri huko, mwingine alikuwa anapiga deal za kusaga nafaka kwa wamenye kwenye mashine ya shule n.k...
 
Nikajua atakuwa Harvard, oxford, Cambridge etc ,ila Kwa kumbukumbu nilizonazo Martin chegere O'level alipata Div one ya point 10 na hakuwa T.O na alimaliza mwaka 2003 au 2004 o'level

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
Elimu ya bongo konyo sana, jamaa alikua T.0 hata scholarship hakupata Kila siku tukawa nae tunapigwa vumbi tu kwenye vimbweta vya coet
 
Elimu ya bongo konyo sana, jamaa alikua T.0 hata scholarship hakupata Kila siku tukawa nae tunapigwa vumbi tu kwenye vimbweta vya coet
Hehehehehe ,embu piga hesabu top ten wote kuanzia 2000 Hadi Leo 2024 anza kuwafanyia analysis walipo sasa Yani utakuja kuchoka wengine wanamiliki stationary mjini na kupambana na usafiri wa mwendokasi

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Basi umenyeni hapo ndo nimepiga, weekend kwenda mjini ilikua ruksa tulikua tunasikia raha kweli kuvaa vile vi t shirt vya shule... Mi mwenyewe nilikua hustler nimefanya sana deals nyingi shule, ila kunywa Yale maji ya mtoni pale ni kitu kilinishinda... Jioni ikifika Kuna mademu tulikua tunawapigisha tizi kwenye kile kimlima Cha kupanda pitch hukosi hata buku 2 ya kusogeza siku😃😃

Sijawahi kusoma kwa usongo kuanzia o level nilikua nasoma kiasi na relax kabisa
 
Siku Moja nilienda kibaha kujisomea maana nilikua na mshikaji pale, aisee saa 5 naenda kulala watu wananishangaa, nikasema hii elimu siyo mateso,

Watu walikuwa wanalala saa 3 usiku, michezo wanacheza vizuri na wana single digit...

Ili ufaulu unapaswa uelewe ulichosoma, usikisahau na uweze kujua namna ya kukitumia unapopata swali...

Kwa muda gani mtu asome? Kila mtu ana uwezo tofauti wa kusoma na kuelewa...
 
Mbuzi hizo unakuta zimerudia shule mara kadhaa, tulisoma na watu wa mvi na wengine wana ndevu mpaka kwenye matundu ya pua na masikio
 
Ile pepa ya 2013 ilikuwa balaa... Nimemaliza pugu pcm.... Nakumbuka, ile pepa natoka tu kwa mtihani wa adv math 1... Kichwa kinuma balaaa😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…