Kwa walioolewa: Ulikutaje Nyumba au Chumba chako uliporudi kutoka Safari ambayo ulienda peke yako bila Mwenza?

Moral of the story unaogopa chura,ila nyie wakaka wa siku hizi😁😁😁😁
 
Kuna kijana ukuta wa chumba chake uliachia kwa nyuma usawa wa kitanda kutokana na mvua kunyesha.... mwenyewe alikuwa mihangaikoni......

Yaani kulikuuwa na chupa za mikojo kama zote......aisee kuna watu ni wachafu......

Nyumba imezungushiwa ukuta lakini anaogopa kutoka nje usiku.......
 
Mimi huwa nakuta shuka analotandika kitandani limefungwa pande zote ili lisichomoke. Kwahiyo akilala akiamka hamna haja ya kutandika.

Vingine navikuta kama vilivyo, hagusi kitu zaidi ya anapokaa aangalie TV. Hapiki hata chai hadi mbwa anawanunulia chakula.
 
Zile pilika pilika za kuweka vitu kimpangilio kwa kusema kweli zinaleta uvivu sana. Mambo ya kutandika kitanda, kupanga nguo kabatini yamenishinda.... mamsap asipokuja geto acha pabaki ivyo ivyo tu.
Tupo wengi bhn kuna siku unaamka unajifanya una hali ya kuweka mambo sawa unaishia kufua nguo kazaa na kufuta viatu
 
Duh mm nguo huwa navalia sebuleni hadi zinaisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…