PAPAA JIWE
JF-Expert Member
- May 12, 2014
- 863
- 149
- Thread starter
- #121
Deo siku hizi yuko utawala IFM pale.
Jamaa fulani hall five juu
kabisa walikuwa wakitaja Odooooong!!hall zingine zote hadi madarasani
wanaitikia Odwaaaaaaar!!mpaka raha.
Hii ilikuwa baada ya jamaa kunyimwa kupigwa chini kugombea urais kisa
urais baada ya upepo wake kuvuma chuo kizima na kwa kweli alikuwa
achukuwe ushindi wa zaidi ya asilimia 90.
Ila mi naukumbuka uchaguzi wa DARUSO 2006/2007 kati ya Mwita wa
Engineering na jamaa mmoja wa B-COM aitwaye Makoye.
Uchaguzi ule ulitawaliwa na vitimbi na vurugu ajabu hali iliyosababisha
baadhi ya watu kuumizwa vibaya,yaani unafikiri wanaowapiga wenzao
hawakuwa wanafunzi wa chuo.
Upepo kwa mara ya kwanza ulikuwa upande wa MAKOYE lakini katikati ya
game hali ilibadilika ghafla kwani Makoye si mzungumzaji mzuri tofauti
na Mwita ambaye alikuwa kiboko wa kuongea na kushawishi.
Hadi Mwisho Mwita alishinda urais na baadaye alikuja kuwa fisadi wa kufa
mtu.
Baada ya Mwita alikuja Deo ambaye hakuwa na sauti kubwa kumshinda waziri
mkuu wake Mtatiro.
Kwa wote hao Odong angeruhusiwa kushiriki uchaguzi siku ya mwisho basi
ndiye angekuwa mwanaharakati mkuu kuwazidi wote.