Kwa waliopita UDSM- Mlimani Campus

Kwa waliopita UDSM- Mlimani Campus

Hata me kanikumbusha mbali sana hii meeting na kawambwa ilikua iwe nkrumah hall watu wakagoma padogo wakaamishia viwanja vya pool baada ya mkutano pipo zikaanza kuzomea na kuwarushia maji FFU wakafanya yao nakumbuka nilikimbia kutoka uwanjani nikajikuta mbele ya mawasiliano tower kuna mvulana alianguka mbele yangu nilimruka kama siyo demu vile ctakaa nisahau revolution for changes:sly:

Hahahah watu walipoona msafara unaondoka wapo haiwezekani yan mnaondoka hivihivi.....wakaanza kuwarushi ffu makopo ya maji. Nilikimbia siku ile sitasahau....ningekuwa na ugonjwa wa moyo that day ningeR.I.P
 
We acha kabisa wengi wamepotea ila wale wabishi i meant home kwao wapo safi waliponea turkey,india,norway or Sweeden kuna jamaa moja mwaka jana ndo kagraduate MD turkey huku alitakiwa amalize 2010, mi nakumbuka mkuu wa polisi oysterbay alitaka kunibambikizia kesi kubwa ipo siku ntakutana nae nimeyasahau lakn ila alitaka kunifuta kwenye uso wa dunia asante my parents am here. Struggle never cease.

inaonekana kuna mbinu zinafanyika kuwapunguza watu kutoka kanda ya ziwa!

i may think so, wazazi nao wanatupiga mikwara mingi sana tujapo huku...

kuna jamaa kafukuzwa UD karibu miaka 10, basi kila siku huwa ananipa wosia wa kutogoma...
 
Pole sana mkuu, kaza mwendo komaa na maisha jenga nchi andaa mazingira bora kwa vizazi vijavyo.

Yani huyo mkuu wa oysterbay aone matunda yako katika jamii ndipo ajutie kosa ndani ya nafsi yake. Ila usitamani kulipiza wala usimchukie.


We acha kabisa wengi
wamepotea ila wale wabishi i meant home kwao wapo safi waliponea
turkey,india,norway or Sweeden kuna jamaa moja mwaka jana ndo kagraduate
MD turkey huku alitakiwa amalize 2010, mi nakumbuka mkuu wa polisi
oysterbay alitaka kunibambikizia kesi kubwa ipo siku ntakutana nae
nimeyasahau lakn ila alitaka kunifuta kwenye uso wa dunia asante my
parents am here. Struggle never cease.
 
Hahahah watu walipoona msafara unaondoka wapo haiwezekani yan mnaondoka hivihivi.....wakaanza kuwarushi ffu makopo ya maji. Nilikimbia siku ile sitasahau....ningekuwa na ugonjwa wa moyo that day ningeR.I.P

Hahaaaa ile siku watu waliumia wengine walizimia baadae mkandala akaenda kuwasabahi pale dispensary.
 
Benedikti Mtungirehi (spelling does not matter) alinunulika kirahisi kama kashata, Mkumbo saliti wa Chadema aliuza uhuru na utu wa wanafunzi. Huyu kaanza zamani sana kutumika wao na Mtungirehi ambaye kwa sasa nafikiri ni mkuu wa wilaya huko Kusini. Kusaga sijui yuko wapi huyu ila alikuwa na busara sanakatika kukabiliana na setikali na wanafunzi.
 
Hapa sijaona rika langu. mimi nilikua pale VC alikua papaa Kuhanga. CADO papaa Mkude. CACO papaa msuya RIP uongozi wa serikali ya wanafunzi. Papaa Ozias Sam Kilewo. papaa Bazigiza. papaa Kakeneno. papaa Kakonko nadhani meneja tanroads Arusha. baadae papaa Matiko Matare enzi za ruksa. PM alikua pm kweli papaa Warioba. miaka ile mwanamke akivaa nusu uchi papaa mzee PUNCH anamuanika Manzese cafeteria iliyo karibu na bookshop. hivi abortion valley bado lipo ? academic bridge je ? hall one kwa ma hog bado ipo ? Zile sinema kule FoE A21 na vitafunio baada ya filamu vipo ?enzi zile wanawake marufuku kunywa chai ya saa kumi cafeteria ili wakaimprove culinary skills zao. enzi zile hakuna colleges ni faculty tu nazo no tano tu. FASS. FCM. FSc. FoE na FL.

Tuko pamoja mkuu alikuwa papaa Luhanga si Kuhanga. Bogus fulani hivi mlevi kupindukia. Enzi zile mzee punch hatari mno ila kunji nyingi sana. Daruso ilikuwa kweli na ukileta mzaha unatimuliwa. Mtungirehi alikimbizwa hadi akaanguka chini ya meza watu wanavuta tai karibu wamuue
 
Unayemwongelea wewe siye. She is out of udsm politics. Utakuwa unakaongelea kadada flani kakutokea songea nako kanapiga harakati. DARUSO walijitahidi sana kukazimisha mpk ikabidi ajitolee jamaa mmoja (excom) akawa anakagegeda ndo kakapunguza mzuka
hahhaha mkuu nmecheka Sana hiyo post....
 
Odooooooong! Halaf tunajibu, Odwaaaaar! Mtatiro na mtoto wa mama Leah (a.k.a. Bush) na Rais wao Deo! Nafkiri Mlowe Pasience hatomsahau Odong Odwar katika maisha yake! So sad that the guy was expelled from the varsity and immediately was taken back to his country - Uganda.

odong aliongoza kutetea mikopo ya wanafunzi ilhali hakuwa Mtanzania wakati watanzania waoga wakijificha hall 3
 
Tarehe 12/11/2008 Uongozi wa UDSM ulilazimika kufunga chuo kwa muda usiojulikana Kutokana fujo zilizotokea chuoni pale kwa siku 3 mfululizo! Nakumbuka hapa kulikua na nguvu ya siasa pia! Kikubwa ni kwamba uongozi wa UDSM ulikua unamtaka Pasience Mlowe awe Rais wa DARUSO wakati kwa wanafunzi walikua wanamtaka ODONG ODWAR! Naikumbuka siku hii kwani nilinusurika ajali wakati nawakimbia FFU waliokua na uchu wa kutoa kipigo kwa wanafunzi!

Pasience Mlowe mwenyewe alipata kura 350 tu,alipinduliwa baadae,nakumbuka sana siku ile tulinusurika kipigo baada ya 'task force' kuizingira library wakitaka kuwacharaza watu waliokuwa library wakitaka wajiunge na maandamano,sasa tulitolewa kwa mlango wa dharura.
 
Odong alikuwa anashindana kijana mmoja alikuwa anaitwa Pasiense Mlowe kama sijakosea,wote wakiwa wanafunzi wa kitivo cha sheria.Bwana Pasiense alinivutia sana na kauli yake "Tofautisha kati ya hamu na shauku".Ila Odong alikuwa kiboko,likitajwa jina Odooong,watu wote mnaitikia Odwaaa,hata kama upo chooni.hahahaaaaaa there is nothing like UDSM aisee

[Hata kama upo chooni]
Yaani nimefikiria anachokifanya mtu chooni halafu anaitikia "Odwaaaa"...Nmecheka sana mkuu
 
Tuko pamoja mkuu alikuwa papaa Luhanga si Kuhanga. Bogus fulani hivi mlevi kupindukia. Enzi zile mzee punch hatari mno ila kunji nyingi sana. Daruso ilikuwa kweli na ukileta mzaha unatimuliwa. Mtungirehi alikimbizwa hadi akaanguka chini ya meza watu wanavuta tai karibu wamuue

Papaa umekosea. Nicholas KUHANGA aliondoka akawa balozi Zaire ndio akaja hexagonal professor Geoffrey Mmari alipoondoka ndio kaja mlevi prof. Mathew Luhanga. Huyu KUHANGA hakua prof. alikuaga waziri wa elimu ndio walivyomtoa kule wakampandisha mlimani. Luhanga kaJa kWenye 90 s ni ndugu yake na yule Luhanga wa Tanesco. Mkuu kkiswa bado iko fresh
 
mkuu sokwe hakufukuzwa. Mkenda na ado shaibu wamerudishwa. Mkenda nimemaliza nae mwaka huu. Kama una mawasiliano na evaristo silayo naomba nipm

Hata Nikodemus Kazimili tumemaliza nae this time, though alikuja semister ya pili mwaka wa tatu, ni mtata haswa...
 
Bora mkuu,maisha yatakua mepesi hasa boom likikata,Enzi zangu maji ilikua full kudownload.

Mkuu sidhani kama umeshafikia kiwango changu, nilikua nadownload mzigo wa siku tano za week, nauweka kwenye plastick, nkawa naupiga password za kutosha lakini wajomba still walikunywa tu, BLOCK C , a hood to mark
 
Kunji la sheria ya mikopo ilikua 2004 mkuu, likiongozwa na Tweve. Waziri alikua Dr Pius Ngwa'ndu! Sitasau kunji lile!

Nakumbuka siku ile maana tulivyoenda kwenye maandamano mara ya pili, watu tuliambiwa hakuna mtu kukimbia. Tukafika pale mlimani city tukakaa chini. FFU wakaanza mbwembwe zao za kutupa onyo, onyo la kwanza likatolewa ondokeni aaaaah watu tumekaaa kimya tu, onyo la pili likatolewa, kisha wakamalizia onyo la tatu na la mwisho kisha bendera nyekundu ikapandishwa juu.

Nakumbuka likarushwa bomu ya machozi juu (vertically) likadondoka katikati yetu watu tukanawa maji machoni na lile bomu pia likamwagiwa maji. Likapigwa bomu la pili tena juu, watu tukatulia tukanawa maji. Hapo FFU wakaona hawa wanafunzi wagumu wakaamua kurusha mabomu horizontally halafu kwa wingi, mmoja aliyekuwa karibu yangu kipande cha bomu kikampiga kwenye paji la uso akapasuka na damu zikaanza kumtiririka hapo kila mtu halihamaki na kuanza kukimbia. Kila mtu na njia yake. Mimi nilikimbia njia ya makongo jeshini nakumbuka nilifika sehemu tukakuta mafundi wa fridge mmoja wetu akaingia na kujificha ndani ya fridge. Kuna wengine walikimbilia ardhi university wakati huo uclas, FFU walifuata huko huko ndani ya chuo na kuwapiga sana, watu wengi waliporwa simu na vitu vingine na hao FFU.

Kesho yake chuo kikafungwa na kupewa masaa mawili tuwe tumeondoka chuoni, nakumbuka tangazo lilitolewa kama saa saba mchana na saa kumi jioni hatakiwi kuonekana mwanafunzi yeyote. Huu ni moja ya mgomo wa mwisho mkubwa kutokea UDSM. Kwa jinsi BAHATI TWEVE alivyokuwa anafafanua kwa nini tunagoma jamii nzima ilikuwa upande wetu. Miaka ya hivi karibuni unawaona wanafunzi wamegoma, vyombo vya habari vikija na kuuliza kwa nini wanagoma wanashindwa kuwa mtu ambaye anaweza kudadavua kwa undani kiini cha mgomo wao. Kuna migomo mengine mkiwa mmejipanga vizuri hata wahadhiri wanakuwa upande wa wanafunzi.
 
Mkuu umeandika vizuri sana. Kuna kamgomo flani kalitokea pale Udsm juzijuzi ka kugomea shato, kalikuwa kamgomo mshenzi sana. Hakana kichwa wala miguu.

Nakumbuka siku ile
maana tulivyoenda kwenye maandamano mara ya pili, watu tuliambiwa hakuna
mtu kukimbia. Tukafika pale mlimani city tukakaa chini. FFU wakaanza
mbwembwe zao za kutupa onyo, onyo la kwanza likatolewa ondokeni aaaaah
watu tumekaaa kimya tu, onyo la pili likatolewa, kisha wakamalizia onyo
la tatu na la mwisho kisha bendera nyekundu ikapandishwa juu.

Nakumbuka likarushwa bomu ya machozi juu (vertically) likadondoka
katikati yetu watu tukanawa maji machoni na lile bomu pia likamwagiwa
maji. Likapigwa bomu la pili tena juu, watu tukatulia tukanawa maji.
Hapo FFU wakaona hawa wanafunzi wagumu wakaamua kurusha mabomu
horizontally halafu kwa wingi, mmoja aliyekuwa karibu yangu kipande cha
bomu kikampiga kwenye paji la uso akapasuka na damu zikaanza kumtiririka
hapo kila mtu halihamaki na kuanza kukimbia. Kila mtu na njia yake.
Mimi nilikimbia njia ya makongo jeshini nakumbuka nilifika sehemu
tukakuta mafundi wa fridge mmoja wetu akaingia na kujificha ndani ya
fridge. Kuna wengine walikimbilia ardhi university wakati huo uclas, FFU
walifuata huko huko ndani ya chuo na kuwapiga sana, watu wengi
waliporwa simu na vitu vingine na hao FFU.

Kesho yake chuo kikafungwa na kupewa masaa mawili tuwe tumeondoka
chuoni, nakumbuka tangazo lilitolewa kama saa saba mchana na saa kumi
jioni hatakiwi kuonekana mwanafunzi yeyote. Huu ni moja ya mgomo wa
mwisho mkubwa kutokea UDSM. Kwa jinsi BAHATI TWEVE alivyokuwa anafafanua
kwa nini tunagoma jamii nzima ilikuwa upande wetu. Miaka ya hivi
karibuni unawaona wanafunzi wamegoma, vyombo vya habari vikija na
kuuliza kwa nini wanagoma wanashindwa kuwa mtu ambaye anaweza kudadavua
kwa undani kiini cha mgomo wao. Kuna migomo mengine mkiwa mmejipanga
vizuri hata wahadhiri wanakuwa upande wa wanafunzi.
 
Mkuu enzi zangu mwaka wa kwanza pale block c palikuwa panaitwa BBA. Tulikuwa tunaishi na kiume na wa kike mle ndani, sasa kwenye kugawana mabafu na vyoo ndio palikuwa kituko kiaina.

Mkuu unamaanisha kuna wakati ulikuwa unashindwa hata kula RB unaishi kwa mihogo ya mtaani?

Mkuu sidhani kama
umeshafikia kiwango changu, nilikua nadownload mzigo wa siku tano za
week, nauweka kwenye plastick, nkawa naupiga password za kutosha lakini
wajomba still walikunywa tu, BLOCK C , a hood to mark
 
Back
Top Bottom