Nakumbuka siku ile
maana tulivyoenda kwenye maandamano mara ya pili, watu tuliambiwa hakuna
mtu kukimbia. Tukafika pale mlimani city tukakaa chini. FFU wakaanza
mbwembwe zao za kutupa onyo, onyo la kwanza likatolewa ondokeni aaaaah
watu tumekaaa kimya tu, onyo la pili likatolewa, kisha wakamalizia onyo
la tatu na la mwisho kisha bendera nyekundu ikapandishwa juu.
Nakumbuka likarushwa bomu ya machozi juu (vertically) likadondoka
katikati yetu watu tukanawa maji machoni na lile bomu pia likamwagiwa
maji. Likapigwa bomu la pili tena juu, watu tukatulia tukanawa maji.
Hapo FFU wakaona hawa wanafunzi wagumu wakaamua kurusha mabomu
horizontally halafu kwa wingi, mmoja aliyekuwa karibu yangu kipande cha
bomu kikampiga kwenye paji la uso akapasuka na damu zikaanza kumtiririka
hapo kila mtu halihamaki na kuanza kukimbia. Kila mtu na njia yake.
Mimi nilikimbia njia ya makongo jeshini nakumbuka nilifika sehemu
tukakuta mafundi wa fridge mmoja wetu akaingia na kujificha ndani ya
fridge. Kuna wengine walikimbilia ardhi university wakati huo uclas, FFU
walifuata huko huko ndani ya chuo na kuwapiga sana, watu wengi
waliporwa simu na vitu vingine na hao FFU.
Kesho yake chuo kikafungwa na kupewa masaa mawili tuwe tumeondoka
chuoni, nakumbuka tangazo lilitolewa kama saa saba mchana na saa kumi
jioni hatakiwi kuonekana mwanafunzi yeyote. Huu ni moja ya mgomo wa
mwisho mkubwa kutokea UDSM. Kwa jinsi BAHATI TWEVE alivyokuwa anafafanua
kwa nini tunagoma jamii nzima ilikuwa upande wetu. Miaka ya hivi
karibuni unawaona wanafunzi wamegoma, vyombo vya habari vikija na
kuuliza kwa nini wanagoma wanashindwa kuwa mtu ambaye anaweza kudadavua
kwa undani kiini cha mgomo wao. Kuna migomo mengine mkiwa mmejipanga
vizuri hata wahadhiri wanakuwa upande wa wanafunzi.