Kwa wamiliki wote wa magari ya Nissan tukutane hapa

Kwa wamiliki wote wa magari ya Nissan tukutane hapa

Mkuu mimi nimetumia za Nissan mbili, nilianza na Nissan cube, kagari kangu ka kwanza kabisa ka kuanzia maisha. Haka nilikaa nako miaka 5. Pamoja na udogo wake, kalikuwa very stable barabarani, kipindi cha kikombe cha babu kalitoka iringa hafi loliondo-samunge kwa babu na kurudi iringa..
Nice experience..
 
Mimi nilikua na Nissan X-Trail na nimekaa nayo kwa takribani miaka 8 baadae nikaiuza ilikua mwaka jana. Changamoto nilizokumbana nazo zingine zilikua ni za kawaida na zilikua zinafanyiwa kazi na kutatuliwa.

Changamoto kubwa zilikua ni 2:-
1. Ilishanitokea kwa Injini kuzima nikiwa naendesha tena kama mara 4 na baada ya kuangalia tatizo kwa kutumia Diagnosis Machine, tatizo ilikua ni sensor moja ya kwenye engine, hii gari inakua na sensor 2, ya pili nadhani ni kwenye gearbox ama Crank Shaft na nilinunua zote mpya nikazifunga na tatizo likaisha.


2. Kwa mafundi wetu kuja kugundua tatizo inachua muda ni kufa kwa Bearings za kwenye shockup za mbele ambazo zinakuwa kwenye Top Cover za Shockup, hizi bearings zikifa kunasikika mlio wa kitu kinagonga, hapa inatakiwa unaponunua Shockup, basi nunua shockup iliyo kamilika ama kama unanunua Shockup peke yake bila Top Cover na Spring Coils zake basi fundi awe anazipitia hizo bearings kwa kuweka grease na hapo utakua umetatua tatizo la hizo bearings kufa. Hii ilinitokea ikiwa kila kitu cha chini kwenye gari vikiwa vimebadilishwa lakini bado tatizo likawepo, baadae ndio ikagundulika ni bearings za kwenye Shockup za mbele na zilipobadilishwa tatizo likaondoka.

Kwa kifupi hizi gari ni nzuri, ukibadilisha spare zinakaa muda mrefu ila kwa sasa nimehamia kwenye magari ya Mjerumani na Mmarekani.

Baadhi ya mafundi wetu wamekariri magari, ukimpelekea gari nyingine zaidi ya magari ya Mjapani hajui wapi pa kuanzia, sasa mimi ndio namuelekeza nini cha kufanya, Wengine hata hawajui wapi zinapokaa Air Conditioner Filters za magari ya Ulaya/Marekani.

Kumbukeni magari yenye gear box za Automatic zilipoanza kuja mafundi walikua wanaziponda wakizisiia za Manual sababu walishazoea kucheza nazo, hawakumbuki kwamba Teknolojia inabadilika na ukiangalia magari yenye Gear Box za Automatic, Engine zake zinadumu tofauti na za Manual. Nilishakua na gari aina ya Toyota Mark II GR na nilidumu nayo kwa takribani miaka 4 nikaiuza yenye gear box ya manual ilikua baada ya muda fulani lazima ubadilishe Clutch Plate, hii nilibadilisha mara 2 na kuifanyia Engine Overhaul mara 1 wakati hiyo Nissan nilikaa nayo miaka 8 hakukua na usumbufu wowote kwenye Engine wala kwenye Gear Box
 

Attachments

  • Nissan X-Trail Engine Sensors, Switches & Connectors.jpg
    Nissan X-Trail Engine Sensors, Switches & Connectors.jpg
    7.7 KB · Views: 20
  • Nissan X-Trail Front Shock Absorber Bearing.jpg
    Nissan X-Trail Front Shock Absorber Bearing.jpg
    17.2 KB · Views: 22
Mimi nilikua na Nissan X-Trail na nimekaa nayo kwa takribani miaka 8 baadae nikaiuza ilikua mwaka jana. Changamoto nilizokumbana nazo zingine zilikua ni za kawaida na zilikua zinafanyiwa kazi na kutatuliwa...
Much thanks...
Umeeleza vizuri sana..
Vipi tatizo la kuchemsha kama watu wengi wanavyoziponda hizi gari za x trail..?
Tupe uzoefu kidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Much thanks...
Umeeleza vizuri sana..
Vipi tatizo la kuchemsha kama watu wengi wanavyoziponda hizi gari za x trail..?
Tupe uzoefu kidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijawahi kukumbana na tatizo la gari kuchemsha.

Yaani muda wa Service nilikua naifanyia service, Engine Oil nilikua natumia Castrol Edge 5W-40 kila baada ya km 3,000 ila mafundi walikua wananiambia nifanye kila ikifika km 5,000 na nilikua nabadilisha Oil Filter ambazo zilikua Genuine. Gear Box Oil nilikua naweka Matic J kila ikifikia km 20,000 nabadilisha.

Kwenye rejeta nilibadilisha Engine Coolant mara 1 niliyonunua Total Filling Station ambazo ni za Total kutokana na kubadilisha Relay ya kwenye Compressor ya AC, iliyokuwepo ilimwagwa. Haijawahi kutokea maji(Engine Coolant) kwenye rejeta kupungua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shukrani sana...mrejesho mzuri...naimani wengine watajifunza hapa..
Sijawahi kukumbana na tatizo la gari kuchemsha.

Yaani muda wa Service nilikua naifanyia service, Engine Oil nilikua natumia Castrol Edge 5W-40 kila baada ya km 3,000 ila mafundi walikua wananiambia nifanye kila ikifika km 5,000 na nilikua nabadilisha Oil Filter ambazo zilikua Genuine. Gear Box Oil nilikua naweka Matic J kila ikifikia km 20,000 nabadilisha...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mimi nimetumia za Nissan mbili, nilianza na Nissan cube, kagari kangu ka kwanza kabisa ka kuanzia maisha. Haka nilikaa nako miaka 5. Pamoja na udogo wake, kalikuwa very stable barabarani, kipindi cha kikombe cha babu kalitoka iringa hafi loliondo-samunge kwa babu na kurudi iringa. Mpaka nakauza, sikuwahi kupata changamoto kubwa zaidi ya zile za kawaida. Spear pia nilikuwa napata japo bei ilikuwa juu kidogo ukilinganisha na magari ya ukubwa huo ya kampuni ya Toyota. Hata hivyo, spear yake ilikuwa inadumu muda mrefu sana ikifungwa...
Nina Nissan Cube, 2007, nimeridhika nayo kuliko, kila kilichoandikwa kuhusu Nissan ni kweli, spears ghali kidogo, ila wasahau, iko stable, reliable, nimeka-jazz up basi kako poa sana, tairi pana basi kamenyanyuka hivi, nasikitika sijatumia Turbo/Sport kwa safari ndefu, ila nina mpango huo kwa kuenda samilia mama mikoani, gari zake ziko poa sana hizi Nissan, infact I am so hooked in such nimeanza kutafuta Nissan Cube ya 2011 au zaidi.

Tujipongeze kwa kweli. Bad note : Juzi pale Beachcomber Africana nilitolewa show na katoto fulani kavulana kako kama 8-9 yrs of age, kwa kuiita Nissan Cube ina sura mbaya?!😡😡😡 To make matters worst, nikashuhudia kale katoto kametoka na ndugu zake na wazazi wakapanda Bajaj?! Can you believe it?!

Ndorobo kabisa,,,
 
Nina Nissan Cube, 2007, nimeridhika nayo kuliko, kila kilichoandikwa kuhusu Nissan ni kweli, spears ghali kidogo, ila wasahau, iko stable, reliable, nimeka-jazz up basi kako poa sana, tairi pana basi kamenyanyuka hivi, nasikitika sijatumia Turbo/Sport kwa safari ndefu, ila nina mpango huo kwa kuenda samilia mama mikoani, gari zake ziko poa sana hizi Nissan, infact I am so hooked in such nimeanza kutafuta Nissan Cube ya 2011 au zaidi..
Tujipongeze kwa kweli...
Bad note : Juzi pale Beachcomber Africana nilitolewa show na katoto fulani kavulana kako kama 8-9 yrs of age, kwa kuiita Nissan Cube ina sura mbaya?!😡😡😡 To make matters worst, nikashuhudia kale katoto kametoka na ndugu zake na wazazi wakapanda Bajaj?! Can you believe it?!
Ndorobo kabisa,,,
[emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina Nissan Cube, 2007, nimeridhika nayo kuliko, kila kilichoandikwa kuhusu Nissan ni kweli, spears ghali kidogo, ila wasahau, iko stable, reliable, nimeka-jazz up basi kako poa sana, tairi pana basi kamenyanyuka hivi, nasikitika sijatumia Turbo/Sport kwa safari ndefu, ila nina mpango huo kwa kuenda samilia mama mikoani, gari zake ziko poa sana hizi Nissan, infact I am so hooked in such nimeanza kutafuta Nissan Cube ya 2011 au zaidi.,

Hahah hongera sana kwa Hio cube mkuu,ila una moyo hahah.

Kuna nyingine inaitwa Toyota BB si inajua inaundugu na Nissan Cube

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom