Kwa Wanachama wa TAHA, nataka kujiunga

Kwa Wanachama wa TAHA, nataka kujiunga

pettymarcel

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2012
Posts
2,161
Reaction score
880
Wakuu naomba msaada kwa yeyote anaefanya kazi TAHA au mtu au kikundi ambacho ni mwanachama wa TAHA Tanzania, nataka kujiunga na hii taasisi nikiwa na lengo la kubase on long term agriculture yaani kilimo Cha matunda Cha Muda mrefu nataka kulima matunda Kama parachichi, papai na nanansi za kisasa

Maombi yangu kwa wadau
Kujua sifa na taratibu za kujiunga na TAHA coz nataka kufanya hiki kilimo nikiwa chini yao ili nipate mafunzo zaidi

Pili kujua Kama Kuna garama zozote ambazo mwanachama anatakiwa kulipia ili kujiunga nao
Tatu naomba kujua kwa wataalamu wa kilimo je zao la parachichi Hanss inaweza kukubali kwa Mwanza maana nataka kupanda ekari nyingi pili kwa ekari moja yaweza nigarimu Bei gani yaan kwa ile phase one ili nijiandae kulima ekari 10 hadi 15 kwa kuanzia asante
 
Nadhan bado ni 50! Nna contact zao nitakutumia nikiziona!...uulize kila kitu..alafu TAHA wako active arusha zaid...moro wala!
 
Ulilipia garama kiasi gani na kwanini uliacha kiongozi naomba unisaidie maana sisi tunataka kujiunga ila lazima tupate ABC kutoka kwa members

Sent using Jamii Forums mobile app

50000!!! Mie sikuona msaada wao niwe mkweli...nilikua najishughulisha na kilimo cha strawberry ..sana sana unaenda tu kusogoa! Nimeachana na kitu kinachoitwa kilimo! .
Kila la heri
 
Nadhan bado ni 50! Nna contact zao nitakutumia nikiziona!...uulize kila kitu..alafu TAHA wako active arusha zaid...moro wala!
We mwanamke wewe, unanishangaza sana
Hizi hustles unamiaka mingapi unafanya mbona kila kitu unajua wewe tuu?
How are you stay informed na hizi mambo .
 
We mwanamke wewe, unanishangaza sana
Hizi hustles unamiaka mingapi unafanya mbona kila kitu unajua wewe tuu?
How are you stay informed na hizi mambo .

Hee!mwenzako nimemaliza tu chuo nakuanza hustling! Niliajiriwa kwa kipindi kifupi kazi nikaacha 2017 october! Muda wote huo nafanya kazi na mishe za kitaa..kifupi nna miaka kumi had mwaka huu nahangaika tu🤣! Naamini iko siku ntatoka tu iwe isiwe!..nadhani nimekujibu kiasi!

Then apart frm that Familia yangu ni wafanyabiashara wazuri tu na wakulima had kesho
 
Hee!mwenzako nimemaliza tu chuo nakuanza hustling! Niliajiriwa kwa kipindi kifupi kazi nikaacha 2017 october! Muda wote huo nafanya kazi na mishe za kitaa..kifupi nna miaka kumi had mwaka huu nahangaika tu🤣! Naamini iko siku ntatoka tu iwe isiwe!..nadhani nimekujibu kiasi!

Then apart frm that Familia yangu ni wafanyabiashara wazuri tu na wakulima had kesho
Mungu akujalie mkuu, hongera sana kwa njia uliyochagua kupita
Na swali hilo la mwisho mbona hujanijibu?
 

Mie sijawahi pata msaada wao...sikumbuki..wanadai wanakusaidia kufind masoko lakini kwangu ilikua ngumu coz soko lilikuwepo...walinishauri nijiongeze ninunue gari yenye freezer...!

Tunda likivunwa lifike zuri..nikaorganize na wenyeji sikupata ushirikiano...! Zao lilipoanza zoeleka nikaacha..esp Arusha walipoanza kununua miche nikaona haina furute tena..ndo kama unavyoona 🍓🍓🍓 sasa hivi haina soko kbs! Nadhan parachichi kwa sasa ndo habari ya mjini!
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Mie sijawahi pata msaada wao...sikumbuki..wanadai wanakusaidia kufind masoko lakini kwangu ilikua ngumu coz soko lilikuwepo...walinishauri nijiongeze ninunue gari yenye freezer...! Tunda likivunwa lifike zuri..nikaorganize na wenyeji sikupata ushirikiano...! Zao lilipoanza zoeleka nikaacha..esp Arusha walipoanza kununua miche nikaona haina furute tena..ndo kama unavyoona [emoji526][emoji526][emoji526] sasa hivi haina soko kbs! Nadhan parachichi kwa sasa ndo habari ya mjini!
Nilitaka kuwajoin nikilima vitunguu, sa sijui watanitafutiaje soko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wana agronomists wazuri sana na wapo up-to-date kama Kenya. Ada ya uanachama ni laki 1 kwa mwaka, wanakutembelea shamba mara kwa mara bila kulipa chochote.

Unatakiwa kujipanga kifedha na kuwa mvumilivu kwasabababu masharti yao ni mtihani kwa mtu asiyekuwa serious na kilimo
O763718849 afisa huduma za uanachama
 
wana agronomists wazuri sana na wapo up-to-date kama Kenya. Ada ya uanachama ni laki 1 kwa mwaka, wanakutembelea shamba mara kwa mara bila kulipa chochote. Unatakiwa kujipanga kifedha na kuwa mvumilivu kwasabababu masharti yao ni mtihani kwa mtu asiyekuwa serious na kilimo
O763718849afisa huduma za uanachama

Sent using Jamii Forums mobile app


Labda Arusha sio Moro
 
Back
Top Bottom