Kwa wanandoa: Unamalizaje haja zako Ukiwa mbali na mwenza wako?

Kwa wanandoa: Unamalizaje haja zako Ukiwa mbali na mwenza wako?

Kama yupo ndani ya hiyo nchi mnapanga ratiba kukutana, kama mmoja yupo dar mwengine yupo singida hivi basi mnakutana dom week-end mnafanya yenu hata mara 2 kwa mwezi si mbaya
Wale wa Moja kigoma mwingine dsm
 
Laiti kila mmoja wetu angefunguliwa macho ya rohoni akaona uthamani wa kumpa Yesu maisha yake, amkomboe mazima, na thawabu zile watakazozipata wale watakaoishi maisha matakatifu hapo baadaye, hakika tungelifikiria matakatifu na yaliyo ya Mungu na wala tusingejinajisi.

WAEFESO 1:18 inasema, Macho yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake, jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo.

MATHAYO 19: 27, INASEMA, 27Ndipo Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi? 28Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli. 29Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele. 30Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.

anaposema walio wa kwanza watakuwa wa mwisho na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza anamaanisha nini? Yesu alitoa mfano MATHAYO 20, kwamba kuna mtu alikuwa na shamba, akaita wafanyakazi wengine saa asubuhi, wengine mchana, na wengine jioni kabisa, ila mshahara aliwapa ule ule sawa wote regardless ya muda waliospend. hivyo wale wa asubuhi wakalalamika kwamba hao wa jioni wasipate sawa; inatufundisha nini?

1. kuna watu wameokoka, watadumu katika wokovu hadi Yesu atakuja na kuwachukua, au watakufa katika wokovu na kwenda mbinguni kwenye raha.

2. kuna watu hawajaokoka, ni watenda dhambi sana, ila kabla hawajafa wanaweza kubahatika kuitikia sauti ya Mungu wakaokoka wakafa katiak Bwana au Yesu akarudi na kuwakuta wakiwa katika wokovu. watapona.

3. Yesu alisema, makahaba wanaweza kuwatangulia ufalme wa mbinguni kwasababu ata pamoja na kufanay sana ukahaba na dhambi nyingi, walikuja kuokoka mwishoni wakapona, ila wewe mshika dini umeishika bila Mungu maisha yako yote, unashida siku, unashika sheria za mwilini badala ya sheria ya Rohoni, unaabudu masanamu ya maria, unaabudu mungu wa kiarabu, hutaki kuokoka, utaenda motoni hivyo hivyo. kahaba uliyemcheka na kumtenga atageuka mwishoni, na atakutangulia.

4. wewe uliyeokoka, Neno la Mungu linasema shika sana ulicho nacho, asije mwovu akaitwaa taji yako ya uzima. ukiteleza, rudi kwa Mungu haraka usije kufa katika dhambi, ni hatari mno, kwani muda wako wote uliookoka utakuwa ulipoteza. kimbia dhambi, mwombe Mungu akusaidie ushinde dhambi, Yusufu alisema nimtendeje Mungu dhambi kubwa namna hii, mwogope Mungu hata ukiwa sirini, acha unafiki kujifanye umeokoka mbele za watu ila sirini una madudu, una hirizi, una waganga, una rushwa, una uzinzi, una chuki, hausamehi n.k. amua mazima kumtumikia aidha Mungu.

5. wachungaji kuweni makini, Neno la Mungu linasema, wale wenye kuongoza wengi kutenda mema watang'aa kama nyota. usije kujidanganya kwamba kwasababu wewe ni mchungaji basi una exception kwenye dhambi, unaweza tu kuwa na kiburi chako, dharau, wizi wa sadaka, miujiza ya uongo, uzinzi na waumini, ugomvi ninyi kwa ninyi mkigombania vyeo, uchawi ili kushika cheo as if unafanya kazi ya kaisari sio ya Mungu, acha michanganyo, makahaba wanaweza kukutangulia mbinguni, ukaenda motoni.

zaidi ya yote, Okoka leo, halafu shikila hapo hapo, shika sana ulicho nacho, shikilia wokovu hadi siku yako ya mwisho au hadi Yesu atakaporudi, kwasababu ndio kitu cha thamani kuliko vyote. Mungu ameandaa kitu cha thamani sana kwa wale watakaovumilia hadi mwisho, UZIMA WA MILELE PAMOJA NAYE, na wale wengine ni moto wa milele na milele. waza uzima, ogopa mbele yako kuna moto kama hautakuwa makini, ogopa ogopa ogopa. kwanini umkose Mungu kwa ajili ya ajira tu, kwa hirizi tu, kwa waganga tu, kwa uzinzi tu, kwa chakula tu, kwa kinywaji tu umkose Mungu? kwa mambo ya dunia hii ambayo yanapita kweli umkose Mungu? kweli? Mungu anakuona hata unapomsaliti kwa dhambi mbalimbali, anakuvumilia, anatamani ugeuke, na upendo wake kwetu ni mkuu mno, hauna kipimo, ukigeuka na kuacha dhambi atakusamehe zote kabisa. kwanini usimrudie tu Mungu? kwanini? kuna sababu gani utakayojitetea siku ile wakati amekupa uzima, amekupa maisha, ameshikilia pumzi yako, wengine wamelala sasaivi ICU wewe upo hapa unaagalia JF upo mzima, kwanini umkose Mungu wakati amekupa nafasi? unajua utakufa lini? unajua Yesu atakuja lini? wengi walikuwa na mipango ila wakaamka asubuhi wamegongwa wamekufa gafla hata nafasi ya kutubu wamekosa, wewe unayo, geuka, mrudie Mungu wako, wakati umeisha, YESU KRISTO ANARUDI, YESU KRISTO ANARUDI, YESU KRISTO ANARUDI, YESU KRISTO YU MALANGONI ANARUDI ANARUDIIIIIIII. KESHENI BASI KWA MAANA HATUJUI SIKU WALA SAA. SIKU YA KUFA AU YA KURUDI KWAKE. KESHA NDANI YA WOKOVU, POKEA WOKOVU NA USIKUBALI MWANAUME WALA MWANAMKE AU YEYOTE KAZINI AU POPOTE AKUFANYE UMKOSE MUNGU. USIKUBALI.
 
Back
Top Bottom