Kwa wanaoamini hakuna Mungu, njooni hapa

Kwa wanaoamini hakuna Mungu, njooni hapa

Hakuna Mungu wa aina yeyote ile.

Hakuna Mungu wa dini.

Hakuna Mungu Muumba.

Hakuna Mungu wa kila kitu.

Hakuna Mungu The great architecture.

Hakuna Mungu Designer.

Hakuna Mungu wa aina yeyote ile.
Sawa kwa tueleze kwa unavojua ww je binaadamu wa kwanza alikujaje hapa duniani ñaomba muongozo wako
 
Mkuu.

Inawezekanaje, kila sehemu ya Dunia kuna watu wanaamini Mungu yupo na asiwepo.

Yaani kila utakakokwenda wewe hapa duniani kuna watu wanaamini Mungu yupo. Haijalishi wanamuitaje au wa namna gani. Ila wanaamini yupo.
Keyword: “wanaamini”.

Maana yake ni kwamba ‘hawajui’.

Wewe unajua kama baba yako yupo au unaamini baba yako yupo?
 
Sawa kwa tueleze kwa unavojua ww je binaadamu wa kwanza alikujaje hapa duniani ñaomba muongozo wako
Hakuna binadamu wa kwanza kwa watu wote.

Kungekuwa na binadamu wa kwanza kwa watu wote duniani, Kusingekuwa na utofauti wa rangi na vinasaba kwa binadamu.

Kama kungekuwa na binadamu wa kwanza kwa watu wote, Basi binadamu wote ulimwenguni tungefanana vinasaba vyetu pamoja na rangi.

Lakini sivyo Binadamu tume tofautiana, Kuna waafrika weusi, wazungu weupe, wahindi weusi, wachina, Wajapan, wafilipino, waarabu, wahindi wekundu, wahindi weupe n.k

Huu ni uthibitisho tosha kwamba hakuna binadamu wa kwanza ulimwenguni wa watu wote.
 
Keyword: “wanaamini”.

Maana yake ni kwamba ‘hawajui’.

Wewe unajua kama baba yako yupo au unaamini baba yako yupo?

Nani alikwambia kuamini hakuambatani na kujua ?

Jifunzeni maana za maneno.

Imani imegawanyika katika makundi makuu mawili, kuna imani sahihi hii inatanguliwa na elimu sahihi yaani kujua kisha unaamini, na kuna imani potofu ambayo sio sahihi hii inatanguliwa na ujinga kama imani ya ukana Mungu na mfano wake.

Kuna muda unaweza ukasema naamini fulani yupo huku ukiwa na uhakika na kujua ya kuwa yupo.

Suala la uwepo wa Mungu na utambuzi wake ni suala la kimaumbile na kila mwanadamu aliumbwa katika umbile hilo na hili lina ushahidi mwingi sana.

Kinachotokea hapa ni watu kuja kujazwa fikra potofu ambazo haziambatani na kufikiria mambo kiundani ambazo zimejengeka katika dhana na nadharia ambazo hazina ushahidi wowote.
 
Leta uthibitisho kwamba hakuna mungu acha siasa
Mungu hayupo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika yupo.

Na huu ni uthibitisho tosha kwamba hayupo.

Wewe unayesema Mungu yupo ndio uthibitishe yupoje?

Una elewa?
 
Kungekuwa na binadamu wa kwanza kwa watu wote duniani, Kusingekuwa na utofauti wa rangi na vinasaba kwa binadamu.

Kama kungekuwa na binadamu wa kwanza kwa watu wote, Basi binadamu wote ulimwenguni tungefanana vinasaba vyetu pamoja na rangi.

Lakini sivyo Binadamu tume tofautiana, Kuna waafrika weusi, wazungu weupe, wahindi weusi, wachina, Wajapan, wafilipino, waarabu, wahindi wekundu, wahindi weupe n.k

Huu ni uthibitisho tosha kwamba hakuna binadamu wa kwanza ulimwenguni wa watu wote.

Matumizi yako ya tamko "nge" yanaonyesha wazi ya kuwa hujui na huna ushahidi juu ya hicho unachokiandika. Tutakuuliza umejuaje hili ?

Andika vitu ambavyo una uhakika navyo na uhitimishe kwa lile unalo lijua.

Bado hujathibitisha bali umetengeneza sentensi ambazo zina hitaji ushahidi, ya kwamba utuambie ilikuwaje hao watu tofauti wakawepo ?
 
Matumizi yako ya tamko "nge" yanaonyesha wazi ya kuwa hujui na huna ushahidi juu ya hicho unachokiandika. Tutakuuliza umejuaje hili ?
Wewe ukiulizwa umejuaje kuna Mungu?

Unaanza kuleta hadithi za kwenye Quran. Mara ooh! Imeandikwa kwenye Quran.

Ukiambiwa uthibitishe ukweli wa hayo maandishi ya Quran huwezi.

Unabaki kuruka ruka tu.
Andika vitu ambavyo una uhakika navyo na uhitimishe kwa lile unalo lijua.
Wewe mwenyewe huna uhakika, uthibitisho wala ushahidi wa uwepo wa Mungu.

Mnafosi fosi tu imani zenu uchwara zisizo na uthibitisho wowote ule.
Bado hujathibitisha bali umetengeneza sentensi ambazo zina hitaji ushahidi, ya kwamba utuambie ilikuwaje hao watu tofauti wakawepo ?
You need mental rehabilitation therapy.

Wewe mwenyewe bado hujathibitisha uwepo wa huyo Mungu yeye kama yeye.

Unaleta hadithi zenu uchwara za vitabuni huko kwenye Quran zisizo na utofauti na hekaya za Abunuwasi.
 
You don't understand what I mean by perfection, I'll use a simple analogy. Nyumba yako Ina paa, Kuta, umepigà rangi, mabati mazur, ceiling ulioyoitengeza na mvuto , milango na madirisha pamoja na ventilators , that's perfection , kwasabb we ni designer umefkria kabla hujajenga au umeona wengne waliovojenga. Hivyo ndivyo kwa " Muumba" yaani God ( designer) . Ukienda kwenye mapango hayana sakafu au tiles kama nyumba yako kwasabb "nature" ndio imeyatengeneza in it's chaotic ways

Mkuu mifano unayotuletea ni Non Sequtal, Unajaribu kuthibitisha perfection ya huyo Mungu wa kwenye vitabu kwa kulinganisha na Nyumba nzuri ambayo aliye iunda pekee ndiye anaiona kua ni perfect, Labda kwakua ametumia Ideas na materials anazozipenda yeye binafsi.

Perfect haikosolewi mfano hewa- Huwezi ukaikosoa hewa, Huu mfano ulioutoa kuhusu nyumba ni wrong, sababu kuna house designer wengine wakiiona hiyo nyumba huenda wakasema "Huyu jamaa kwanini aliezeka bati migongo hii, au kwanini asingepiga rangi hii, Au nyumba nzuri ila Sijapenda ramani ya vyumba" Kwahiyo nyumba haiwezi kuwa perfect.

Kama unathibitisha Mungu ni perfect kwa kumlinganisha na nyumba iliyodizainiwa vizuri lakini bado inakosolewa, Tutawezaje kukukubaliana na wewe kwamba Mungu ni perfect?
 
Wewe ukiulizwa umejuaje kuna Mungu?

Unaanza kuleta hadithi za kwenye Quran. Mara ooh! Imeandikwa kwenye Quran.

Ukiambiwa uthibitishe ukweli wa hayo maandishi ya Quran huwezi.

Unabaki kuruka ruka tu.

Nilikupa kazi uonyeshe uongo wa Qur'an na utuambie ya kuwa kwa vipi Qur'an isiwe ushahidi. Ikaonekana kumbe hata hiyo Qur'an huijui.

Ukaanza kuruka ruka na kukimbia maswali, ukaendelea kukosoa kulinganisha vitu ambavyo havifanani bali ukakosea zaidi hata kuandika jina la Abuu Nawas.

Qur'an inajuthibisha yenyewe kwa kile ilichonacho na kule ilipo Toka. Ndio maana ukashindwa kuonyesha uongo wa Qur'an.

Kuisoma kwenye Qur'an aya inasomeka hivi :

35. Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji?

36. Au wao wameziumba mbingu na ardhi? Bali hawana na yakini. (at-Tur : 35 - 36)

Sasa hicho ndicho ambacho Kimo kwenye Qur'an Sasa uje kutoa majibu kwa ushahidi na utuambie je kilichoandikwa hapo ni uongo ?

Nasisitiza tena, uje uthibitishe ya kuwa yaliyomo kwenye Qur'an ni Hadithi. Kila siku nakupa angalizo hakikisha unakijua unacho kijadili.
Wewe mwenyewe huna uhakika, uthibitisho wala ushahidi wa uwepo wa Mungu.

Mnafosi fosi tu imani zenu uchwara zisizo na uthibitisho wowote ule.

Mimi Nina uhakika, Nina jua na ndio maana kith bitisha uwepo wa Mola muumba sijawahi kushindwa bali ni kitu chochote.

Bakuongezea na hili, katika kila kitu unachokijua na usichokijua kinathibitisha juu ya uwepo wa Mola tena ni mmoja aliye tukuka.

Wewe Imani yako ina uthibitisho gani zaidi ya kuonyesha ni mgonjwa wa akili na una uwezo mdogo wa kufikiri.
You need mental rehabilitation therapy.

Wewe mwenyewe bado hujathibitisha uwepo wa huyo Mungu yeye kama yeye.

Unaleta hadithi zenu uchwara za vitabuni huko kwenye Quran zisizo na utofauti na hekaya za Abunuwasi.

Halafu hakuna mtu anaitwa Abunuwasi, uwe unasoma kwanza kabla ya kuandika. Unaposema ni Hadithi uchwara unatakiwa usihishie hapo, kosoa na uonyeshe uuchwara huo, kinky me na hapo unacheza makida makida na unaleta utoto.

Uwepo wako wewe tu inaonyesha ya kuwa Mungu yupo. Sasa unapo uliza na kutaka uthibitisho inaonyesha wazi ya kuwa hujawahi kufikiria hilo.
 
Mkuu mifano unayotuletea ni Non Sequtal, Unajaribu kuthibitisha perfection ya huyo Mungu wa kwenye vitabu kwa kulinganisha na Nyumba nzuri ambayo aliye iunda pekee ndiye anaiona kua ni perfect, Labda kwakua ametumia Ideas na materials anazozipenda yeye binafsi.

Maana ya mifano sio lazima ilingane sawa sawa, bali inaakisi uhalisia. Unapo pewa mfano ni ili uelewe na kutambua uhalisia.

Hoja zenu mnapozijenga kwa kutumia misingi ya logic, mnazifunga akili zenu zisifikirie nje ya hizo fikra na misingi waliyo iweka Wanafalsafa watu ambao hawakuwa na ala nzuri za kuwafikisha katika kupata majibu sahihi. Logic msingi wake mkuu ni akili, na akili ya mwanadamu ina ukomo.

Mungu hafanani na chochote bali ni mkamilifu mwenye kujua.

Kwa ufupi uwepo wa kitu huonyesha uwepo wa kitu kingine kilicho fanya kitu hicho kuwepo.

Uwepo wa Mungu ni uwepo wa lazima ambao hauhutaji uwepo wa kitu kingine zaidi yake kufanya Mungu awepo, huo ndio ukamilifu wake.
 
Perfect haikosolewi mfano hewa- Huwezi ukaikosoa hewa, Huu mfano ulioutoa kuhusu nyumba ni wrong, sababu kuna house designer wengine wakiiona hiyo nyumba huenda wakasema "Huyu jamaa kwanini aliezeka bati migongo hii, au kwanini asingepiga rangi hii, Au nyumba nzuri ila Sijapenda ramani ya vyumba" Kwahiyo nyumba haiwezi kuwa perfect.

Suala la kukosolewa ni suala lingine ambalo lonahusu dhati, ila maana ya kuwepo Msanifu ndio maana ya msingi.

Wewe unapo ona nyumba akili yako ya kawaida na haraka itakwambia hiyo nyumba haijajijenga yenyewe Wala haijatokea pasi na chochote bali ni mchakato na nidhamu ikafanya nyumba ikawepo.

Wenyewe mnaita "Self evident truth". Hili halipingiki, na ukipinga hili basi wewe utakuwa ni mwendawazimu hasa.
 
Hakuna binadamu wa kwanza kwa watu wote.

Kungekuwa na binadamu wa kwanza kwa watu wote duniani, Kusingekuwa na utofauti wa rangi na vinasaba kwa binadamu.

Kama kungekuwa na binadamu wa kwanza kwa watu wote, Basi binadamu wote ulimwenguni tungefanana vinasaba vyetu pamoja na rangi.

Lakini sivyo Binadamu tume tofautiana, Kuna waafrika weusi, wazungu weupe, wahindi weusi, wachina, Wajapan, wafilipino, waarabu, wahindi wekundu, wahindi weupe n.k

Huu ni uthibitisho tosha kwamba hakuna binadamu wa kwanza ulimwenguni wa watu wote.
Nakubali umesema hakuna binaadamu wakwanza kutokana na urofauti wa rangi na vinasaba unamaanisha tumeombwa tofauti tuchukulie washaumbwa watu warangi tofauti navinasaba je walitokana nann au walikuja kivip mpaka wakawepo duniani tunahitaji chanzo cha uwepo wap utuelezee
 
Back
Top Bottom