Kwa wanaoamini hakuna Mungu, njooni hapa

Vyote unavyosema ni imani tu ndio maana hizo habari zinaitwa za kiimani tu mkuu🤔 siku zikithibitika hazitahitaji kuitwa tena imani bali uhakika na ukwel🤔🤔.
 
Acha ujinga, ulaya makanisa yapo kibao na yalijengwa tokea miaka hiyo viwanda vinajengwa. Hamna uhusiano apo mkuu
 
Hizi thread za kuhusu uwepo wa Mungu au kutokuepo kwa Mungu zimekua nyingi saaana. Wale wenye misimamo ni ya humu JF, in real life hawasimamii misimamo yao
 
Hivi ushawahi kuuona upepo? na je upo au haupo? Naomba nijue roho ni nini?
 
Una maana wanaojinadi kuamini Mungu JF wote hawaamini Mungu in real life?

Thibitisha.
Kuna jamaa yangu yupo umu, anataka apinge uwepo wa Mungu ili aone reaction za wanaJF. Yani kiufupi anawachota
 
Kuna jamaa yangu yupo umu, anataka apinge uwepo wa Mungu ili aone reaction za wanaJF. Yani kiufupi anawachota
Kitu muhimu si jamaa yako.

Jamaa yako ni kinyama tu atakufa miaka si mingi ijayo.

Mimi pia hivyo hivyo.

Kitu muhimu ni hoja, ukweli.

Jadili hoja, usijadili mtoa hoja.

Kujadili mtoa hoja badala ya hoja kutakupeleka kwenye ad hominem logical fallacy.

Twende kazi.
 
Swali lako la kwanza, nimejua kwa kutumia viumbe vyake, kwa kutumia akili, kwa kutumia mazingira, na kwa kutumia ufunuo.
Kama unashindwa kuthibitisha yupo hauna ruhusa ya kusema viumbe vyote ni vyake.

Unamaanisha nini unaposema unathibitisha kwa kutumia ufunuo?

Huo ufunuo umetoka wapi? Huo ufunuo unathibitisha vipi kwamba Mungu yupo?
 
Kama unashindwa kuthibitisha yupo hauna ruhusa ya kusema viumbe vyote ni vyake.

Unamaanisha nini unaposema unathibitisha kwa kutumia ufunuo?

Huo ufunuo umetoka wapi? Huo ufunuo unathibitisha vipi kwamba Mungu yupo?
ufunuo umetoka wapi hayo uliyosoma yakakuaminisha kuwa hakuna mungu ukakubali upagani umeyasoma kutoka wapi? (upotovu)
 
Sifa tu kuna binadamu asiye penda sifaa lakini unajua kuwa akuna alinacha, au imani ya watu walio kulea ujaafikiana nao baada ya kutafuta maarifa zaidi umeamua kukubali upagani upotovu!
Hapo hakuna upagani kwa sababu wapagan nao wanaamini tu kama nyie sema nyie kujiona imani yenu ipo sahihi zaidi ,mkawaita hao wanao amini kama nyie tu wapagani .
 
Ww unaweza kunithibitishia kuwa una akili?

Kama unazo niambie ni rangi gani? Zimekaaje?

Mwenda wazimu ana kichwa kama ww lkn yeye anaambiwa hana akili au mgonjwa wa akili, kidhibiti gani kilichothibitisha kuwa hana akili?

Swali hilo huwezi kulijibu milele.

Sio kila kisichoonekana maana yake hakipo.

Zipo dalili zaidi ya 10000kuthibitisha kuwa Mungu yupo.

Ww huna dalili hata moja, maana kwa akili iliyosalimika inathibitisha uwepo wa Mungu.

Mtoto mdogo tu ambae akili yake ipo salama haijachafuliwa ukimuuliza Mungu yupo wapi? Atakwambia yupo juu.
 
Haliletiti muktadha wa matumizi ya lugha ya kiswahili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…