Kwanini unaandika uongo wa wazi ambao unaonyesha wazi kabisa hujafikiria hiki unachokiandika.
Kwetu sisi Waislamu aya nyingi sana zinatuhimiza juu ya kufikiria na kutumia akili ? Dini hasa Uislamu kwa maana ya vitabu vile vinne yaani Taurati, Zaburi, Injili na Qur'an vimekuja kumpa majibu mwanadamu ambayo akili haiwezi kuyajibu.
Swali la kwanza ambalo unatakiwa uniulize na mwenye akili timamu lazima ajiulize tu, kwanini tunaishi ? Je tunaishi ili tukue tuazliane kisha tufe halafu iwe basi ? AKILI iliyo salama inakataa hili. Ikiwa hivi basi itakuwa hakuna maana ya maisha bali kupoteza muda tu.
Lakini, vipi wale watu waovu na wanao wadhulumu watu ? Je itakuwa hivyo tu halafu basi ? Aisee dini inawataka watu wenye akili.