Kwa wanaoamini hakuna Mungu, njooni hapa

Kwa wanaoamini hakuna Mungu, njooni hapa

Kushindwa kudhibiti mambo, yalokinyume na mapenz yako, ni ushahidi tosha kuna super natural power, inadhibiti mambo ni vile tu nyie mshachagua upande wa kupinga.
Logical non sequitur fallacy.

Kwanza kabisa kuhoji uwepo wa Mungu kwa kuangalia contradictions zilizopo katika habari za uwepo wake si kutetea mambo yaliyo kwenye mapenzi ya mtu.

Ni kuhoji habari za uwepo wa Mungu kwa mujibu wa maelezo ya wanaosema Mungu yupo.
 
Kwa wanaoamini hakuna mungu, ukiwachunguza kwa makini hawa watu ndiyo ujifanya wao ni majiniazi, kumbe ni wapumbavu wa mwisho katika hii dunia, na hoja yao kubwa ni kwamba kila kitu ni nature hoja hii haina mashiko hata kidogo na ni hoja ya kipuuzi ambayo utolewa na watu ambao kwa kawaida wameshindwa kuamini katika imani zao kwa uthabiti maybe wamechunguza kuwa katika imani zao ambazo wamekuwa na kulelewa umo aziko sawa sawa na azijawapa majibu yakutosha kiasi cha wao kuamini

Kuna wengine majeuri tu na kwakweli katika hii dunia watu hao awawezi kukosekana wanajua na kuona lakini nyoyo zao zimekufa na wauwaji ni wenyewe na matendo yao.

Na rudi katika hii hoja ya kusema kila kitu kipo sababu ni nature, huyu huyu anaesema hivi anaamini kwamba simu anatengeneza mzungu internet mzungu,

ila jinsi mungu alivyoumba kila kitu kwa ustadi wa hali ya juu wanasema ni nature, ushuuzi!
ASANTE SANA HAO WAPAGANI WAJE WATUAMBIE KUWA DUNIA ILIUMBWA VIPI?
 
Mkuu, nishakuambia siku za nyuma, kushindwa kudhibiti mambo yalokinyume na mapenzi yako ni ishara ya uwepo wa super natural power inayodhibiti mambo.
Supernatural power gani, ilishawahi kudhibiti jambo lolote lile?
 
I'm quite busy I don't know whether I'll be able to respond to all these comments but those who claim that there is no Designer ( God), the evidence is just overwhelming, let them just look at their bodies, the plants , animals , how perfectly they're made. Those proves there's a designer behind that creation. We all know how chaotic nature is, that's why even the minerals like diamonds etc, they can't look the same when they are extracted from the ground , that's why they go through cutting and refining, nature can't create the same thing over and over again.
Kama kila kilicho complex kinahitaji designer, designer wa Mungu ni nani?
 
Energy, kama Yesu au Mungu hayupo Kwanini ukitaja jina la Yesu watu wanaanguka mapepo. Hapa simanishi wachungaji wakubwa tu. Hata nyimbo za gospel ukizipiga mbele ya mtu mwenye mapepo utaona anachange mood. Hii nimeona kwa watu.
Hivi kwa nini wanaoanguka mapepo ni watu masikini tu? Kwa nini matajiri, watu maarufu na viongozi wa kisiasa huwa hawaanguki mapepo??
 
Mkuu unaionaje ile ya upande wa kina FaizaFoxy na Malaria 2 ya kupata mabikira 72 huko firdaus unakula mzigo muda wote🤣?
KWENU WAKIRISTO

Hurul-'Ayn (Wenye macho mazuri) kwa Waumini

Hurul-'Ayn ni neema inayotajwa mara kadhaa katika Qur'an kama moja ya malipo ya waumini waaminifu katika Pepo (Jannah). Hurul-'Ayn hufafanuliwa kama wake wenye uzuri wa kipekee walioandaliwa kwa waumini wa Peponi. Mifano ya aya za Qur'an zinazotaja Hurul-'Ayn ni kama ifuatavyo:

1. Qur'an 52:20



"Watakuwa wakiegemea kwenye makochi yaliyopangwa safu, na tutawaozesha kwa Hurul-'Ayn."
Hii inaonyesha kuwa waumini waliofuzu Peponi watapata wake warembo walio safi na wa pekee.



2. Qur'an 55:70-72



"Ndani yake (Pepo) kuna wanawake warembo wenye tabia nzuri... wao ni mabikira, walioshushwa macho, ambao hakuna yeyote aliyewagusa kabla yao."
Hii inaonyesha usafi wa Hurul-'Ayn na jinsi walivyo wa kipekee.



3. Qur'an 56:35-38



"Hakika sisi tumewaumba kwa uumbaji wa pekee, na tukawafanya mabikira, wenye upendo, na wa rika sawa."
Hurul-'Ayn wanatambuliwa kwa uzuri wao na tabia zao nzuri.




---

Adhabu kwa Makafiri Jahannam

Kwa mujibu wa Qur'an, wale wanaokataa kuamini (makafiri) na wanafanya dhambi kubwa bila kutubia, watapata adhabu kali katika Moto wa Jahannam. Mifano ya aya ni kama ifuatavyo:

1. Qur'an 2:39



"Na wale waliokufuru na wakakadhibisha Ishara zetu, hao ni watu wa Motoni, humo watadumu milele."



2. Qur'an 4:56



"Hakika wale wanaokanusha Ishara zetu, tutawachoma Moto. Kila ngozi zao zitakapoteketea, tutawabadilishia ngozi nyingine ili waonje adhabu."



3. Qur'an 98:6



"Hakika wale waliokufuru miongoni mwa watu wa Kitabu na washirikina watakuwa katika Moto wa Jahannam, humo watakaa milele. Hao ndio viumbe waovu kabisa."
 
Wewe huelewi kuwa hiyo hoja yako ni hoja ya kuonesha Mungu hayupo.

Yani ukichoandika, kwa ntu mwenye kufikiri kwa kina, ni hoja ya kukataa uwepo wa Nungu.

Ila wewe hujajua tu, kwa sababu hufikiri kwa kina.

Kimsingi umeweka hoja kwamba order cannot come out of disorder, vitu haviwezi kuwepo tu vimejioanga, lazima kuwepo na aliyevipanga, na aliyevipanga lazima awe na order au intelligence ya zaidi.

Sasa, unalazimisha Mungu awepo na awe ndiyo huyo akiyepanga (hata kama hoja hii ina non sequitur fallacy kutoka kwako, nitaiendekeza tu kwa sasa).

Tuseme Mungu yupo, na ndiye kaumba haya tunayoyaona.

Bado, kwa kufuata kanuni yako ya order au ibtelligence haiwezi juwapo tu, ni kazima iwe imeumbwa na order au ibtelligence ya juu zaidi, utakuwa umejipa hoja kwamba Mungu naye hawezi juwapo, itabidi awe ameumbwa na Mungu wake.

Na Mungu wake hawezi kuwapo, naye lazima kaumbwa na Mungu wake.

Ad infinitum, ad nauseam.

Hapo utaona msururu usioisha wa miungu wanaoumbwa na miungu wao.

Hapo hakuna Mungu muumba vyote.

Hoja yako inaonesha Mungu hayupo.

Of course unaweza kusema Mungu yeye hajaumbwa.

Which is special pleading logical fallacy.

Na hii special pleading logical fallacy inaharibu hoja nzima kuwa order haiwezi kuwapo bila kuumbwa.

Naandika lakini sina hakika kama unaweza kufuatilia mantiki ya ninachoandika.
Hizi hoja hawawezi kuzielewa, ukishasema Mungu hajaumbwa tayari umeconfirm kwamba hayupo.
 
Inabidi waungane kwanza wa mchague Mungu mmoja kati ya hao halafu ndio waseme sasa🤔
Vipi akiwepo wa kukupa bikira 72 baada ya maisha haya halafu pembeni unajichotea gambe mtoni unavyotaka? Utakataa mkuu?
 
NDUGU YANGU NI BORA UWAMINI MUNGU YUPO KULIKO USIAMIN HAYUPO UKAENDA MBINGUNI UKAMKUTA
Mbingu haijawahi kuwepo haipo na haitakaa iwepo.

Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.

Huyo Mungu kama yupo, Alishindwaje kufanya binadamu wote wakamwamini yeye yupo siku zote na kwa wakati wote?

Huyo Mungu kama alitaka aaminiwe yupo, Alishindwaje kuumba binadamu watakao mwamini yupo?
 
Binafsi naamini Mungu yupo kwa sababu hizi
- Hakuna mwenye uwezo wa kutengeneza hii technology tunayoiona ni wizi wa maarifa. Ndo maana kitabu cha Enock hakiko hadharani, mle zipo hadi habari za Aliens.

- Utabiri wa vitabu vya dini. Hata kama bible ni kitabu cha hekaya lakini ni nani wangekaa na kutabiri haya tunayoyaona leo. Waliosoma Daniel (ndoto ya Nebkadineza) tunaelewana.

Mafanikio ya Watu waovu. Wazungu, wachina na Wajapan wana mafanikio makubwa na ni watu wachafu sana. Kama ulishaajiriwa na mchina utanielewa. Kama tunavyojua dunia ipo chini ya mwovu. Hapa hamna cha ubishi - kumtumikia shetani mali njenje. Sawa mtawatetea na kuwaita magineas lakini tazama maisha yao. Genius anawezaje kuwa shoga, kutengeneza mabom ya kuua watu na sio kusuruhisha? Genius huyohuyo anatengeneza magonjwa library, genius huyohuyo ni mbinafsi, hawezi share na wewe skills zozote. Na genius huyohuyo nia yake ni kukunyonya. Simanishi Afrika hatuna uovu.

Energy, kama Yesu au Mungu hayupo Kwanini ukitaja jina la Yesu watu wanaanguka mapepo. Hapa simanishi wachungaji wakubwa tu. Hata nyimbo za gospel ukizipiga mbele ya mtu mwenye mapepo utaona anachange mood. Hii nimeona kwa watu.

Anyway, naweza nisiwe sahihi lakini tukumbuke hatupaswi kuamini au kutokuamini kizembe. Mwisho kabisa, tusisahau Mungu hana muda wa kudhihirisha live kama tunavyotaka. Sababu sisi ni wenye dhambi mbele zake na sio wote na hao wachache wanaomtukuza anaweza kulizika nao. Kumbuka aliaza na mtu mmoja tu.
Asante

🤣🤣🤣
Sikiliza Comedy Legendary Akieleza Vizuri kabisa
View attachment 3163613

Halafu sikiliza Hawa Wakigombania Race ya Mungu
View attachment 3163617
Kibongo bongo ni kufuru kali mno utaitwa agent wa shetani kabisa 😂😂
 
Ushawahi kujiuliza kwanini hiyo science haina nguvu kwa watu wako (Afrika) ila kwa wale tu ambao ni mashoga, wabinafsi, na wadhaifu. Nawaita wadhifu sababu hawako strong.
Sayansi ina nguvu Africa, huoni life expectancy yetu ni fupi kuliko kwingine kwenye maendeleo ya Sayansi, huoni miondombinu yetu bado duni, huoni watu wenye pesa wakiugua wanapelekwa nje badala ya kutibiwa hapa ndani, huoni wakina Mwamposa na nabii kiboko ya wachawi wanavyotapeli watu. Sasa utasema Sayansi haina nguvu kwa Africa wakati matokeo ya Sayansi ndogo kwa Africa yanaoenkana wazi??
 
Ukiamua kumtafuta Mungu utampata ni vile hujaaamua tuuu mkuu.
Huyo Mungu anatafutwa kwani amepotea?

Huyo Mungu anacho jifichia huko alipo hadi atufutwe ni nini?

Huyo Mungu anayehitaji kutafutwa ni mjinga sana na wala hajielewi kabisa.

Huyo Mungu kama yupo ajitokeze hadharani ajidhihirishe mwenyewe kama ana huo uwezo.

Aache kujificha ficha kama mwali.
 
Mbingu haijawahi kuwepo haipo na haitakaa iwepo.

Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.

Huyo Mungu kama yupo, Alishindwaje kufanya binadamu wote wakamwamini yeye yupo siku zote na kwa wakati wote?

Huyo Mungu kama alitaka aaminiwe yupo, Alishindwaje kuumba binadamu watakao mwamini yupo?
Soma bible utamjua mungu vizur iman yako itaongezeka imagine kizaz cha sasa asingekuwepo mungu kingekuwaje hofu ya mungu inasaidia
 
Back
Top Bottom