Kwa wanaoamini hakuna Mungu, njooni hapa

Ungejua Imani ni nini Na facts ni nini ? Wala usingehangaika kuleta huu mjadala bali ungejua unachokiamini wewe kitaendelea kuwa imani kwako na kukibadilisha kuwa facts kinahitaji vivid proof... Na watu wenye busara zao wanajua kwamba itakuwa fools errand kujikita kwenye mijadala ya Imani..., Uzuri wa facts are based on learning research and experimentation as well as questioning oneself (wakati hizi imani zilizokuja na meli ni indoctrination ambazo ukitumia logic and upembuzi wako utaambiwa unakufuru)

Huwezi kuanza na jibu alafu unatafuta swali (ukifanya hivyo utakuwa, unatetea na sio kutafuta ukweli)
 
Ukisoma physics ya Quantum Causal Loops utaona kuwa kuna level ya ulimwengu huu ambako cause and effect inavunjika.

Sasa, katika dunia kama hiyo, suala zima la cause and effect linaondoka.

Cause and effect ni illusion inayotokea katika ulimwengu wa level yetu tu, ukizama huko kwenye quangum world cause and effect tunayoijua inaondoka, hata time kama tunavyoijua sisi inaondoka.

Soma zaidi kuhusu Quantum Causal Loops hapa.

Haiwezekani Mungu akawa katika hiyo level ya ulimwengu ambayo cause and effect inavunjika lakini ana transcend pia katika level ya huu ulimwengu wetu ambayo cause and effect inatokea kama illusion?
 
Tupe hoja toa fact
Fact ni kwamba Mungu hayupo.

Hoja ni kwamba, ukidai Mungu yupo thibitisha uwepo wake.

Ukishindwa kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu unayesema na kudai yupo, Ni kwamba madai yako ni ya uongo.

Na huyo Mungu unayedai yupo, Hayupo.

Na fact ya kwamba "Mungu hayupo" inakuwa imethibitika.
 
Ukishaanza habari za "haiwezekani..." chochote kinawezekana, hivyo habari hizo hazitusaidii. Hazitusogezi upande wowote mahsusi. Zinatupeleka all over the place.

In fact ukifuatilia "the many worlds interpretation" ya quantum physics, kila kitu unachoweza kukifikiria kinawezekana. Including ulimwengu ambao Mungu yupo na ulimwengu ambao Mungu hayupo na ulimwengu ambao Mungu yupo na hayupo katika wakati mmoja huohuo.

Ndiyo maana ni muhimu kufanya kazi kwa ushahidi, utafiti, uthibitisho.

Mpaka sasa, hakuna ushahidi, hakuna uthibitisho kwamba Mungu yupo.

Wanaosema Mungu yupo, wathibitishe yupo.
 
Sasa mkuu ukiforce kila kitu kiwe na mwanzo si kutakuwa kuna ulazima pia wa chanzo huyo mungu

Sasa hapo utajibu nini?
Majibu ninayo mkuu usihofu , wakaanzishe Uzi au mjadala Kila mtu aje na uthibitisho, mm uthibitisho wañgu sio wa kibiblia lkn unajitosheleza
 
Tatizo alianza kwa kutakana na kutolea watu povu akifikiri hapa yuko mtaani kwake au kwenye vijiwe vyake ambapo mambo ya mungu yakiongelewa wote wanaitikia Alhamdulillah.
Ameona kila anapogusa anakutana na maswali magumu
 
Tatizo alianza kwa kutakana na kutolea watu povu akifikiri hapa yuko mtaani kwake au kwenye vijiwe vyake ambapo mambo ya mungu yakiongelewa wote wanaitikia Alhamdulillah.
Hapa kuna hoja nzito sana ambazo zimewapita kimo watu wengi wanaojibu kirahisirahisi.

Swali la The Problem of Evil aliulizwa Pope Francis na msichana mmoja mdogo tu huko Ufilipino, kimsingi Papa Francis pamoja na usomi wake wote wa falsafa na dini alishindwa kujibu swali na kubumbabumba tu.

Halafu anakuta kifulambute mmoja wa JF ambaye hata haelewi swali la The Problem of Evil ni nini, anajitutumua kujibu kwa kariri zake shallow tu.

Unaona kabisa huyu hajaweza kulijibu swali, kwa sababu kwanza hata hajaelewa swali ni nini.
 
Fact ni kwamba Mungu hayupo.

Hoja ni kwamba, ukidai Mungu yupo thibitisha uwepo wake.

Ukishindwa kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu unayesema na kudai yupo, Ni kwamba madai yako ni ya uongo.

Na huyo Mungu unayedai yupo, Hayupo.

Na fact ya kwamba "Mungu hayupo" inakuwa imethibitika.
Mimi nathibitisha kupitia Bible wew umesoma kitabu kip kandika nan
 
Kwa nini unasema Binadamu ni perfect? Viumbe hai wengine pia ni perfect kivipi?
You don't understand what I mean by perfection, I'll use a simple analogy. Nyumba yako Ina paa, Kuta, umepigà rangi, mabati mazur, ceiling ulioyoitengeza na mvuto , milango na madirisha pamoja na ventilators , that's perfection , kwasabb we ni designer umefkria kabla hujajenga au umeona wengne waliovojenga. Hivyo ndivyo kwa " Muumba" yaani God ( designer) . Ukienda kwenye mapango hayana sakafu au tiles kama nyumba yako kwasabb "nature" ndio imeyatengeneza in it's chaotic ways
 
Sasa mkuu ukiforce kila kitu kiwe na mwanzo si kutakuwa kuna ulazima pia wa chanzo huyo mungu

Sasa hapo utajibu nini?
Kwa mantiki hiyo Kweli unae hoja

Mungu ndio mwanzo

Yaani kuna Nguvu iliyo juu ya nguvu zote.. hata babu zetu walikuwa na namna yao ya kuwasiliana na Muumba wao. Na hawakufundishwa na mtu yeyote ( kutoka kwa mzungu au mwarabu) etc

Wachina wanasema pia kuwa hakuna Mungu ila kuna practice wanazozifanya au wanazoziamini ukiziangalia zinarudi mule mule kwenye a super natural power fulani
 
Majibu ninayo mkuu usihofu , wakaanzishe Uzi au mjadala Kila mtu aje na uthibitisho, mm uthibitisho wañgu sio wa kibiblia lkn unajitosheleza
Uzi upo huu tayari, kwa nini unataka uzi mwingine?
 
Hapa kuna hoja nzito sana ambazo zimewapita kimo watu wengi wanaojibu kirahisirahisi.

Swali la The Problem of Evil aliulizwa Pope Francis na msichana mmoja mdogo tu huko Ufilipino, kimsingi Papa Francis pamoja na usomi wake wote wa falsafa na dini alishindwa kujibu swali na kubumbabumba tu.

Halafu anakuta kifulambute mmoja wa JF ambaye hata haelewi swali la The Problem of Evil ni nini, anajitutumua kujibu kwa kariri zake shallow tu.

Unaona kabisa huyu hajaweza kulijibu swali, kwa sababu kwanza hata hajaelewa swali ni nini.
Mm sitetei dini alaf hujui mm ni nani so you can't judge me and compare to pope Francis. I'm not a religious person , alaf najib bila kutumia lugha ya kufedhehesha mtu Wala kutkana , mambo ya kushindwa hoja nakuanza kutumia lugha na maneno yasiofaa hiyo mijadala mm siwez kuwepo
 
Kwa mantiki hiyo Kweli unae hoja

Mungu ndio mwanzo

Yaani kuna Nguvu iliyo juu ya nguvu zote.. hata babu zetu walikuwa na namna yao ya kuwasiliana na Muumba wao. Na hawakufundishwa na mtu yeyote ( kutoka kwa mzungu au mwarabu) etc

Wachina wanasema pia kuwa hakuna Mungu ila kuna practice wanazozifanya au wanazoziamini ukiziangalia zinarudi mule mule kwenye a super natural power fulani
Kwa msingi wa hoja yako umeweka ulazima wa kila kitu kuwa na muumba hata akiwemo huyo mungu mwenyewe
 
You don't understand what I mean by perfection, I'll use a simple analogy. Nyumba yako Ina paa, Kuta, umepigà rangi, mabati mazur, ceiling ulioyoitengeza na mvuto , milango na madirisha pamoja na ventilators , that's perfection , kwasabb we ni designer umefkria kabla hujajenga au umeona wengne waliovojenga. Hivyo ndivyo kwa " Muumba" yaani God ( designer) . Ukienda kwenye mapango hayana sakafu au tiles kama nyumba yako kwasabb "nature" ndio imeyatengeneza in it's chaotic ways
Nyumba yako si perfection.

Itahitaji maintenance, votu vitaharibika itabidi ubadilishe.

Ikipigwa tetemeko kubwa itaanguka.

Mpaka hapo ushakosea kusema nyumba yako ni perfection.
 
Ukishaanza habari za "haiwezekani..." chochote kinawezekana, hivyo habari hizo hazitusaidii. Hazitusogezi upande wowote mahsusi. Zinatupeleka all over the place.

In fact ukifuatilia "the many worlds interpretation" ya quantum physics, kila kitu unachoweza kukifikiria kinawezekana. Including ulimwengu ambao Mungu yupo na ulimwengu ambao Mungu hayupo na ulimwengu ambao Mungu yupo na hayupo katika wakati mmoja huohuo.

Ndiyo maana ni muhimu kufanya kazi kwa ushahidi, utafiti, uthibitisho.

Mpaka sasa, hakuna ushahidi, hakuna uthibitisho kwamba Mungu yupo.

Wanaosema Mungu yupo, wathibitishe yupo.
Sasa mkuu kama chochote kinawezekana basi inawezekana Ulimwengu ni eternal au sio eternal, AU Mungu ambaye ni eternal pia yupo au hayupo.
Kwa nini usifungie breki na kusimamia hapo badala ya kesema una uhakika hayupo huyo mungu??
 
Mm sitetei dini alaf hujui mm ni nani so you can't judge me and compare to pope Francis. I'm not a religious person , alaf najib bila kutumia lugha ya kufedhehesha mtu Wala kutkana , mambo ya kushindwa hoja nakuanza kutumia lugha na maneno yasiofaa hiyo mijadala mm siwez kuwepo
Maneno mengi lakini hujathibitisha Mungu yupo.
 
Back
Top Bottom