Kwa wanaoamini hakuna Mungu, njooni hapa

Safi kabisa, unaposema kwamba mahubiri unamaanisha ni kitu kisicho kuwa na maana au ni vipi ?

Sababu hata hayo mahubiri ni fact na uhalisia, Sasa unatakiwa upinge kile ninachokiandika na kuonyesha udhaifu wake, na usikimbie hoja.

Mfano, ni huu nakuuliza swali la msingi, je huu Ulimwengu umetokea pasi na chochote au umejiumba ? Bali au ni nyinyi ndio mmeumba mbingu na ardhi ? Karibuni kunakishi hoja na msikimbie hoja, ili muonekane walau mna akili. Kinyume chake mnaendeleza na kuweka sifa zenu wazi za udhaifu wa kujenga hoja, kukosoa hoja na kukimbia maswali.
Kwa nini unahisi ulimwengu lazima utokee au uumbwe?
 
Sio nahisi, yaani nina uhakika huo na ushahidi upo.

Nitakuuliza swali, kwa akili yako huu Ulimwengu umetokea tu pasi na chochote au umejiumba wenyewe ? Hili linawezekana vipi ? Tumia akili yako kisha weka hoja tujadili.
 
Kwa nini unahisi vitu ili viwepo vinahitaji alie viweka awepo? Halafu unakataa Uwepo wa Mungu haujawekwa na mtu mwingine tena na huyo mwingine na mwingine to infinity 🤔🤔
 
Sababu uhalisia unalazimisha viwepo na aliye fanya vikawepo. Unaweza kutuambia imekuwaje vitu vikawepo pasi na chochote ?

Twende taratibu na tufate adabu na nidhamu za mjadala, ulianza kuuliza swali nikakujibu, na Mimi nikakuuliza swali. Utaratibu unakutaka wewe ujibu kwanza kisha uulize swali. Hivi ndio mjadala utaleta maana na huenda tukapeana faida.
 
Hapana, hapa umelazimisha.

Mtu kuwa hai kunathibitisha vipi Mungu yupo?

Logical nonnsequitur fallacy.
Imani ikithibitika haita itwa imani tena siku hiyo hiyo itabadilishwa jina na kuitwa maarifa na ukweli 🤔🤔🤔
 
Sababu uhalisia unalazimisha viwepo na aliye fanya vikawepo. Unaweza kutuambia imekuwaje vitu vikawepo pasi na chochote ?

Twende taratibu na tufate adabu na nidhamu za mjadala, ulianza kuuliza swali nikakujibu, na Mimi nikakuuliza swali. Utaratibu unakutaka wewe ujibu kwanza kisha uulize swali. Hivi ndio mjadala utaleta maana na huenda tukapeana faida.
Sijui inakuje vitu kuwepo pasipo chochote.

Je inakuaje Mungu awepo pasipo chochote? Na hicho chochote pasipo chochote to infinity ------
 
Na kwa nini tushupalie imani ikiwa imani inaweza juwa hata ya uongo na tunaweza kuhakiki mambo tukaondoka kwenye imani na kujikita kwenye ukweli na maarifa?
Mkuu ukwel utafanya watu wakose tumaini , ebu fikiria tu mtu toka mchanga anaambiwa akifa ataenda mbinguni halafu leo ajue ukwel 🤔🤔

Watu wanakubishia sio kwamba wanajua Mungu yupo ila wanabisha kushindana na zile ahadi na matumaini hewa 🤔
 
Sijui inakuje vitu kuwepo pasipo chochote.

Je inakuaje Mungu awepo pasipo chochote? Na hicho chochote pasipo chochote to infinity ------

Safi kabisa, sababu hujui basi leo ujue ya kuwa hakuna kitu kinachokuwepo pasi na chochote isipokuwa MOLA muumba.

Swali zuri, sababu yeye ni chanzo cha kila kitu ambacho hakihitaji chochote ili liwepo.

Infinity hai exist kijana, yaani haipo na hizi ni fikra finyu ambazo zinaenda kinyume na uhalisia. Huwa napenda kuwapo mfano mwepesi wa Entropy kama wewe ni mfatiliaji wa mambo ya Sayansi ? Au second law of Thermodynamics ? Ukivisoma hivi navyo vinaonyesha ya kuwa uwepo wa lazima wa kitu kimoja pekee ambacho hakihitaji chanzo Wala chochote ili kuwepo kwakez sababu chenyewe ni kamilifu.
 
Aya ya kwanza tu imethibitisha ulicho kisema ni maneno ya kiimani tu ambayo hauwezi kuyathibitisha ili yatoke kwenye imani yawe ukwel na hakika.
 
Mkuu ukwel utafanya watu wakose tumaini , ebu fikiria tu mtu toka mchanga anaambiwa akifa ataenda mbinguni halafu leo ajue ukwel 🤔🤔

Watu wanakubishia sio kwamba wanajua Mungu yupo ila wanabisha kushindana na zile ahadi na matumaini hewa 🤔
Kati ya matumaini ya uongo na ukweli usio na matumaini, nachagua ukweli usio na matumaini.
 
Mkuu ukwel utafanya watu wakose tumaini , ebu fikiria tu mtu toka mchanga anaambiwa akifa ataenda mbinguni halafu leo ajue ukwel 🤔🤔

Watu wanakubishia sio kwamba wanajua Mungu yupo ila wanabisha kushindana na zile ahadi na matumaini hewa 🤔

Kwanini unaandika uongo wa wazi ambao unaonyesha wazi kabisa hujafikiria hiki unachokiandika.

Kwetu sisi Waislamu aya nyingi sana zinatuhimiza juu ya kufikiria na kutumia akili ? Dini hasa Uislamu kwa maana ya vitabu vile vinne yaani Taurati, Zaburi, Injili na Qur'an vimekuja kumpa majibu mwanadamu ambayo akili haiwezi kuyajibu.

Swali la kwanza ambalo unatakiwa uniulize na mwenye akili timamu lazima ajiulize tu, kwanini tunaishi ? Je tunaishi ili tukue tuazliane kisha tufe halafu iwe basi ? AKILI iliyo salama inakataa hili. Ikiwa hivi basi itakuwa hakuna maana ya maisha bali kupoteza muda tu.

Lakini, vipi wale watu waovu na wanao wadhulumu watu ? Je itakuwa hivyo tu halafu basi ? Aisee dini inawataka watu wenye akili.
 
Aya ya kwanza tu imethibitisha ulicho kisema ni maneno ya kiimani tu ambayo hauwezi kuyathibitisha ili yatoke kwenye imani yawe ukwel na hakika.

Swali, ni ya uongo au ya kweli ? Maana hapa tunatafuta ukweli. Kama ni uongo niambie uongo uko wapi na ukweli ni upi ?
 
Back
Top Bottom