Kwa wanaoamini hakuna Mungu, njooni hapa

Kwa wanaoamini hakuna Mungu, njooni hapa

na ha
watakupasua kichwa watu waongo na wanafiki kama hao, wamejizatiti katika engo iyo iyo eti wao awa amini kwamba hata tukiacha habari za mungu watakwambia wao hawana kitu kina itwa imani imagine huu si upuuzi wa wasiwasi juu ya watu hawa
na hawa wanataka kuthibitisha kitu kwa kuona ndo wanasema kinastahili kuwa chakweli sasa unaanza kuwaza kwamba kila kinachoonekana kwa macho ndiyo tuthibitishe cha kweli?
 
Ufunuo unatuambia ya kuwa Ulimwengu umeumbwa na yeye, yaani muumbaji anatuhabarisha sisi ya kuwa yeye ndio ameumba viumbe.
Kama huo ufunuo umekwambia kuwa ulimwengu umeumbwa na yeye na umekubali.

Kumbe hata mimi Ibn Unuq nikiandika kitabu nikasema mimi ndiye Muumba utakubali.

Kama utakataa, Basi tumia huo ufunuo kuthibitisha kwamba yupo.
 
watakupasua kichwa watu waongo na wanafiki kama hao, wamejizatiti katika engo iyo iyo eti wao awa amini kwamba hata tukiacha habari za mungu watakwambia wao hawana kitu kina itwa imani imagine huu si upuuzi wa waziwazi juu ya watu hawa
Wewe na hiyo imani yako wote hata msaidiane hamuwezi kuthibitisha.

Kama mnaweza thibitisheni.
 
Wapi nimeshindwa kuthibitisha ?

Ufunuo ni Taurati, Zaburi, Injili na Qur'an.

Ufunuo umetoka kwake, unatupa majibu ya pale ambapo akili imekomea.

Ufunuo unatuambia ya kuwa Ulimwengu umeumbwa na yeye, yaani muumbaji anatuhabarisha sisi ya kuwa yeye ndio ameumba viumbe.
Mkuu unathibitishaje kwamba huo UFUNUO umetoka kwa muumbaji?
 
Kama huo ufunuo umekwambia kuwa ulimwengu umeumbwa na yeye na umekubali.

Kumbe hata mimi Ibn Unuq nikiandika kitabu nikasema mimi ndiye Muumba utakubali.

Kama utakataa, Basi tumia huo ufunuo kuthibitisha kwamba yupo.

Kwanza kitendo Cha wewe kuandika ya kwamba uandike kitabu kisha useme wewe ndio umeumba, inaonyesha una akili ndogo na hufikirii vitu katika uhalisia au hujui nini unachokiaegemea.

Nukta yako au sharti lako au hitimisho lako halihusiani kabisa na kuwepo kwa Mola.

Ufunuo kwanza unasema hivi :


35. Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji?

36. Au wao wameziumba mbingu na ardhi? Bali hawana na yakini.

37. Au wanazo khazina za Mola wako Mlezi au wao ndio wenye madaraka?

38. Au wanazo ngazi za kusikilizia? Basi huyo msikilizaji wao na alete hoja ilio wazi! [at-Tur : 35 - 38]

Hapa ufunuo ulikuwa unawajibu wale ambao walikuwa wanaukana na kukana juu ya uwepo wake. Kwanza kabisa unatakiwa ujue ya kuwa nyinyi sio wa kwanza katika kumkana Mungu na Wala hamtokuja kuwa walau na hoja za kuonyesha kutokuwepo kwake. Sababu Kuna ishara nyingi kuanzia kwenye miwili wako, mazingira na viumbe vingine juu ya uwepo wake.

Tafakari kwanza juu ya ufunuo huo na kile kilichoandikwa humo, kisha uje uoanushe na uonyeshe kinyume chake.
 
Mkuu unathibitishaje kwamba huo UFUNUO umetoka kwa muumbaji?

Swali zuri sababu ufunuo wenyewe ulitoa Challange kwa wale ambao waliukana na kudai ni tungo basi walete walau mfano aya moja tu kama wao wanasema kweli. Mnatakiwa mjue ya kuwa hizi tuhuma zenu hazijaanza leo lala jana bali ni tangu na tangu na tofauti yenu na wale wa kale, wa kale walikuwa wajuzi zaidi katika lugha na kujenga hoja.

Ufunuo unasema hivi, kuwajibu wale ambao walikuwa wanadai ni utungo tu wa mwanadamu na hautoki kwa Mola wetu muumba.


32. Au hizo akili zao ndio zinawaamrisha haya, au wao basi ni watu majeuri tu?

33. Au ndio wanasema: Ameitunga hii! Bali basi tu hawaamini!

34. Basi nawalete masimulizi kama haya ikiwa wao wanasema kweli. (at-Tur : 32 - 35)

Watu wa zamani walimtuhumu ya kuwa Mtume Muhammad aliitunga Qur'an, Allah aliye tukuka akamwambia Mtume awaambie hivyo wale walio mtuhumu kwa utunzi.

Mwenye akili timamu lazima atafakari kwanza, wapo watu humu wanadai Qur'an ni kama Hadithi tu, yaani imetungwa wanatakiwa wajue ya kuwa wao sio wa kwanza katika hilo, ili wawe wa kweli walete huo mfano wa Qur'an au wathibitishe utunzi wake kama wao wanasema ukweli.
 
Mwe! Mwe! yani unathubutu kusema kwamba mungu hayupo, kwahiyo wewe ulijiumba

senga-pic.jpg
 
Uongo wake uko wapi ?

Nani alikwambia masuala ya kiimani sio kweli ?

Unajua ya kuwa katika elimu kubwa na bora kushinda zote ni elimu ya kumjua Muumba ?

Naomba ujibu maswali kwa usahihi, unaposema ni masuala ya kiimani unaonyesha huijui Imani ni nini ?
Imani inakuaje ukweli au uhakika?
 
Hapa naona bado unakimbia hoja, unatakiwa ukosoe ninachokiandika na uonyeshe ya kuwa si sawa, sasa unaposema ni imani tu pasi na kuonyesha dosari ni uchachefu wa maarifa.

Imani ina jengwa na vitu viwili au zaidi, kwanza kusadiki, kusadiki hutanguliwa na elimu yaani kujua, asikudanganye mtu imani inatbitishika na ina uhakika kabisa sababu inatanguliwa na elimu yaani kujua kisha unasadikisha kile ulicho kijua.

Ambao mnasema ni imani tu bila kuichambua hiyo imani mnaonekana mnaleta utoto na hii si adabu katika mambo ya kielimu. Ndio maana kila siku mnakimbia hoja kwa kisingizio cha imani, na huku ukiambiwa uielezee imani ni nini pia hamuwezi.

Kwahiyo wito wangu kwenu ni nyinyi mlete yale ya kweli na mkosoe haya tunayo yaandika hapa.
Mkuu thibitisha Mungu yupo ukiona sijibu jua hakuna cha kujibu.
 
Wapi nimeshindwa kuthibitisha ?

Ufunuo ni Taurati, Zaburi, Injili na Qur'an.

Ufunuo umetoka kwake, unatupa majibu ya pale ambapo akili imekomea.

Ufunuo unatuambia ya kuwa Ulimwengu umeumbwa na yeye, yaani muumbaji anatuhabarisha sisi ya kuwa yeye ndio ameumba viumbe.
Mwamposa anapouza mafuta na maji kuponya watu nao ni Ufunuo.
 
Kwa wanaoamini hakuna mungu, ukiwachunguza kwa makini hawa watu ndiyo ujifanya wao ni majiniazi, kumbe ni wapumbavu wa mwisho katika hii dunia, na hoja yao kubwa ni kwamba kila kitu ni nature hoja hii haina mashiko hata kidogo na ni hoja ya kipuuzi ambayo utolewa na watu ambao kwa kawaida wameshindwa kuamini katika imani zao kwa uthabiti maybe wamechunguza kuwa katika imani zao ambazo wamekuwa na kulelewa umo aziko sawa sawa na azijawapa majibu yakutosha kiasi cha wao kuamini

Kuna wengine majeuri tu na kwakweli katika hii dunia watu hao awawezi kukosekana wanajua na kuona lakini nyoyo zao zimekufa na wauwaji ni wenyewe na matendo yao.

Na rudi katika hii hoja ya kusema kila kitu kipo sababu ni nature, huyu huyu anaesema hivi anaamini kwamba simu anatengeneza mzungu internet mzungu,

ila jinsi mungu alivyoumba kila kitu kwa ustadi wa hali ya juu wanasema ni nature, ushuuzi!
Dhana ya kuwa Mungu yupo ni wazi maana yupo aliyetuzidi maarifa akatuweka huku duniani Mungu huyo aligundulillka zamani sana kwa watu jamii ya wayahudi,nchini israel ziko shuhuda ukienda nchini humo zikiinyesha shuhuda kwamba yupo Mjanja kuliko sisi ambaye ndiye alituumba,isitoshe alishuka mwamba mmoja toka huko ikulu alipo akazaliwa na mwanamke bikira ,huyu mwamba alifanya meng ya kutisha na inaaminika alikufa akafufuka,haya mambo kama hujafika Israeli hutoamin
 
Back
Top Bottom