Ad hominem logical fallacy.
Hii hua inatokea pale mtu anaposhindwa kuhimili mjadala kisha anaamua kuku-attack personally.
Usirudie hilo kosa, unapunguza credit, usiruhusu jazba kwenye mijadala.
Kama wewe unauwezo wa kufikiri katika uhalisia, Thibitisha kwa kutumia uhalisia kama Mungu yupo.
Angalizo kidogo unapotumia misingi ya logic kama msegemeo yako katika mjadala huu ni udhaifu pia, kadhia ya Ad hominem logical fallacy inaingia humo. Hapo hujashambuliwa bali umeambiwa ukweli na kuonyeshwa udhaifu wako, kwenu nyinyi logical kama fani huwa haiwapeleki katika ukweli au kuujua ukweli. Hili kosa usilirudie wewe tena,jikite katika kuutafuta ukweli na uangalie nini kimeandikwa.
Ithibati zangu zote nilizo zitoa ni uhalisia, labda kama hujui uhalisia ni nini ? Unaweza kuonyesha wapi sijatumia uhalisia ?
Mkuu nimesoma hapo, Huyo Mungu asijitetee "excusses" lazima apingwe, atapingwa na ataendelea kupingwa sababu hawezi kujithibitisha kama yupo.
Kwanza hata wewe huna hoja ya kumthibitisha kama yupo.
Nafurahi kwanza kwa wewe kusoma kilicho andikwa. Kingine ambacho huwa mnatupa kazi tunapojadiliana na nyinyi ni kutokujua kwenu maana za maneno. Hakuna sehemu ambayo Allah anajitetea hapo, kasome tena maana ya kujitetea.
Hapo anawazindua watu na kuonyesha sababu miongoni mwa sababu ambazo zinawafanya watu wapinge mambo, miongoni mwa sababu ni ujeuri tu muda ambao wahusika hawana hoja, katika sababu nyingine zinazo fanya watu wapinge ni ujinga yaani kutokujua kama mnavyo fanya nyinyi.
Ili niwe sina hoja ni wewe sasa kukosoa hiki ninacho kiandika na utuandike kilicho sahihi.
Sijaona alipojielezea kwamba yeye ametoka wapi?
Kama ye mwenyewe hawezi kujithibitisha, wewe utawezaje kumthibitisha?
Kama huwezi kumthibitisha kama yupo then hizo ni hadithi za "Alfu lela ulela" .
Kama hizo sio hadithi za kale, Thibitisha yupo, na yuko wapi na alitokea wapi?
@Kisai
Anajieleza vipi ametoka wapi wakati yupo na haja tanguliwa na kutokuwepo yaani wakati. Kusema wapi alipotoka ni udhaifu na kuonyesha yeye si mkamilifu wakati amepwekeka na hiyo sifa.
Yeye amejithibitisha tayari katika kila kitu, hapa ndipo pale tunaangalia sababu zenu za nyinyi kumpinga na tuna washangaa. inakuwaje kwa uwazi ambao Mola ameuweka juu ya uwepo wake nyinyi namuuoni, hapa ndipo pale tunakuja kuhitimisha ya kuwa ni ugonjwa wa akili, ujinga, ulimbukeni, utoto na kutokufikiria mambo katika uhalisia wake.
Kwanza sijashindwa kumthibitisha na hili ni jambo dogo sana, bali tumemthibitisha kila tunapoingia katika hii mijadala.
Kulinganisha ya ufunuo na hadithi za kale huu ni utoto mwingine sababu hivi havifanani kuanzia machimbuko yake na uhalisia. Huku sasa ni kukosa hoja na hili sharti dhaifu sana.
Mola wetu alishatueleza ya kuwa yeye yuko wapi, Allah yuko juu ya Arshi yake amestawi na Arshi ni katika kiumbe kikubwa cha Allah ambacho amekiumba kuzidi viumbe vyote, Arshi iko juu ya mbingu ya saba. Ama ametoka wapi hili swali la uongo sababu haliingii kwake hilo.