Kwa wanaoona mbali, Waziri Ndalichako ni sumu kwenye mfumo wa elimu

Kwa wanaoona mbali, Waziri Ndalichako ni sumu kwenye mfumo wa elimu

scatter

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2013
Posts
1,667
Reaction score
926
Kwa muongo mmoja uliopita umuhimu wa elimu ulikuwa na thamani sana kwa vijana maana thamani yake iliendana na mazingira yaliyokuepo na watu wengi walitamani kupata elimu ili waweze kujikomboa kiuchumi

Baadaya ya muongo mmoja kupitia, hali iliyopo sasa KWA TANZANIA SIO DUNIANI KOTE elimu sio kitu kinachoweza kumkomboa mtu kiuchumi au kumfanya aweze kuishi maisha nzuri, kwa wengi hii ni baada ya waziri husika Ndalichako na mfumo wake kutokuendana na teknolojia

Yaani namanisha kwamba mfumo wa elimu upo nyuma sana na teknolojia ya dunia inavyotaka ndio maana kuna wasomi wengi sana mtaani na hawana pa kwenda. Hali iliyopo sasa MTU MWENYE DEGREE ANAWEZA KUWA MUUZA MAHINDI YA KUCHOMA BARABARANI AU anauza nyanya tu

Sasa unajiuliza Huyu mtu kapoteza miaka zaidi ya 16 kusotea kuuza nyanya ni UPUUZI WA Hali ya juu, wakati huo kuna mtu kaishia darasa la saba (kama yupo smart) kwa miaka hiyo kumi na sita ambayo mtu anatafuta degree utakuta maisha yake amejipanga na tayari ameshakuwa na vitu muhimu kulingana na mahitaji ya binadamu.

Hapo ndipo utakaposhangaa msomi kasota miaka yote hiyo na mtaani akirudi anaonekana hana maaana na hata akitaka baadhi ya kazi alizosomea miaka yote hiyo atahitajika awe na uzoefu wa miaka kadhaa ni upuuzi mkubwa sana na bado msomi huyu akichelewa kupata ajira na kwa bahati nzuri akafanikiwa baada ya miaka kadhaa kuipata hiyo ajira utakuta anaishi na MADENI maisha yake yote ya utumishi.

Ili kuboresha mfumo wa elimu nchini Tanzania ipo haja ya Huyu Waziri Ndalichako na kundi lake kuondolewa katika sekta hii maana ni kama hawajieliwi kwa sababu wao wanaamini katika mfumo wa kutupa wasomi mtaani na bila kujua kile walichowaandalia kina manufaa gani mtaani na kufanya thamani ya elimu kushuka kwa speed kubwa sana.

Anatakiwa kiongozi katika sekta hii awe na uthubutu wa kuvunja baadhi ya mitaala isiyokuwa na TIJA na awe na uwezo wa kutatua changamoto ya thamani ya elimu na mazingira ya kiuchumi kwa msomi atakaye kuwa yupo mtaani Kwan kwa hali iliyopo sasa ni mbaya sana.

Profesa huyu ana amini katika makaratasi yasio endana na uhalisia inasikitisha sana na kutia aibu sana ELIMU YA TANZANIA NI TAKATAKA na Ndalichako hatoshi kwenye mfumo, ukweli huu lazima usemwe ili tujenge mfumo mpya kwa vizazi vijavyo.
 
"Elimu ndo kitu Cha pekee kinacho weza kutumika kubadili dunia"Nelson Mandela
Sawa kwa tanzania kupoje?

Mtu ana degree anauza mtumba barabarani na anamkopa ana daiwa

Mtu asiye elimu naye anauza mitumba barabarani

Maana ya thamani hapo imekaaje?
 
Sawa kwa tanzania kupoje?

Mtu ana degree anauza mtumba barabarani na anamkopa ana daiwa

Mtu asiye elimu naye anauza mitumba barabarani

Maana ya thamani hapo imekaaje?
Kitu gani mkuu unatumia kama kipimo sahihi cha kupima uthamani wa elimu?

Ajira hakuna mtu kamaliza degree anaona asikae bure bora ajishughulishe na biashara ndogo ndogo napo mnawananga akika vijiweni napo mtawananga sasa unataka wafanya nini?
 
Kiufupi serikai nzima kwenye suala la elimu imefeli.

Hizi pesa wanazochezea kujenga madarasa nchi nzima.

Ni bora wangewekeza kujenga vyuo vya kati na VETA nchi nzima tupate kutengeneza ajira za vijana wetu.
 
Mwandiko ni mzuri ila hoja hazimshawishi msomaji kukubali yaliyoandikwa. Binafsi naona hoja ya kukusokana ajira haiakisi mfumo mbovu wa elimu. Tufike mahala tukubali kwamba Watanzania tumelemazwa na ajira serikalini.

Tunapaswa kufikiria namna nyingine ya kujikimu kimaisha badala ya kutegemea ajira za Serikali kwa asilimia mia moja. Wakati ni huu hatujachelewa.
 
Kitu gani mkuu unatumia Kama kipimo sahihi Cha kupima uthamani wa elimu?

Ajira hakuna mtu kamaliza degree anaona asikae bure bora ajishughulishe na biashara ndogo ndogo napo mnawananga akika vijiweni napo mtawananga Sasa unataka wafanya Nini?
Kwanini usomee kitu kisicho na ajira.

Kama soko la ajira lipo sehemu fulani ni bora kusomea huko, yaana unapoteza miaka mingi kwa BAHATI NASIBU YA HAKUNA?
 
Kitu gani mkuu unatumia Kama kipimo sahihi Cha kupima uthamani wa elimu...
Lengo la elimu ni kutoa ufahamu uweze ku ya master mazingira Sasa bongo tunalaumiana bure ni vile ni magoigoi wa kutazama fursa ukichangia na ujamaa ulitulemaza Nigeria Kuna wasomi wengi kiasi PhD holder ni madereva na Ili kutatua changamoto ya ajira wameamua kusambaa duniani ku grad opportunities na hawachagui kazi.
 
Kitu gani mkuu unatumia Kama kipimo sahihi Cha kupima uthamani wa elimu?

Ajira hakuna mtu kamaliza degree anaona asikae bure bora ajishughulishe na biashara ndogo ndogo napo mnawananga akika vijiweni napo mtawananga Sasa unataka wafanya Nini?
Kipimo cha "thamani" ujuzi itumike kulingana na muda uliotumia.

Mfano unasoma miaka mingi kupata ujuzi basi utumie maisha yako katika ujuzi huo sio kutapatapa

Na hii sio kila mtu anaweza ndio maana inatakiwa kwenye mfumo wa elimu wakae watu smart na kwa kuanza tuna angalia aliyop juu amefanikiwa katika hili?
 
Ndalichako hana kosa lolote, ndalichako hatengenezi ajira...
Naungana na wewe ishu sio ajira serikalini focus yangu ni kumba mfumo mzima wa elimu haumpi mtu uhuru wa kutumia ujuzi wake kwa sababu ni "chakavu" na teknolojia iliyopo, namanisha kwamba DEGREE na UJUZI kwa tanzania ni mbingu na aridhi.

Mtu unaweza ukasoma na ukawa huna thaman hivyo jibu ni kwamba "MITAALA NI MIBOVU"

Wizara ya elimu inabidi ikune vichwa na kushirikiana na sekta zingine kubuni Mitaala yenye kuleta ujuzi kwa vijana asimame hata bila kua ajiriwa na aishi kulingan na muda aliopoteza kusaka ujuzi.
 
Pole sana kijana, naona kabisa jinsi unavyoona giza mbele yako.

Hili zigo unalomtwisha Ndalichako si zigo lake peke yake. Mfumo mzima wa serikali unawajibika katika hili.
 
Ajira hakuna badala yake unamlaumu Ndalichako kama waziri wa elimu badala ya kuilaumu serikali ya CCM iliyofeli kutusogeza mbele, kwa akili yako Ndalichako akiondolewa ndio ajira zitapatikana? zaidi utabadilisha mitaala na bado tatizo la ajira libaki pale pale.
 
Ajira hakuna badala yake unamlaumu Ndalichako kama waziri wa elimu badala ya kuilaumu serikali ya CCM iliyofeli kutusogeza mbele, kwa akili yako Ndalichako akiondolewa ndio ajira zitapatikana? zaidi utabadilisha mitaala na bado tatizo la ajira libaki pale pale.
Mkuu namlaumu kwa sababu amekaa pale zaidi ya miaka 20 isiyokua na faida kwa nchi.
 
Kwa kipindi cha miaka mitano, Ndalichako alihakikisha wanafunzi walio pata mimba hawarudi shuleni. Na kudiriki kusema wata wafundisha wengine tabia mbaya.

Leo yule yule profesa ana sema wataruhusiwa kurudi kwenye mfumo rasmi. Upuuzi mtupu.

Siasa ya Tanzania ni ya kujaza choo. Kwanini Mh. Rais hakumuondoa kwenye hiyo nafasi na hili tamko la kuwarudisha wanafunzi litamkwe na waziri mwingine?
 
Back
Top Bottom