Kwa muongo mmoja uliopita umuhimu wa elimu ulikuwa na thamani sana kwa vijana maana thamani yake iliendana na mazingira yaliyokuepo na watu wengi walitamani kupata elimu ili waweze kujikomboa kiuchumi
Baadaya ya muongo mmoja kupitia, hali iliyopo sasa KWA TANZANIA SIO DUNIANI KOTE elimu sio kitu kinachoweza kumkomboa mtu kiuchumi au kumfanya aweze kuishi maisha nzuri, kwa wengi hii ni baada ya waziri husika Ndalichako na mfumo wake kutokuendana na teknolojia
Yaani namanisha kwamba mfumo wa elimu upo nyuma sana na teknolojia ya dunia inavyotaka ndio maana kuna wasomi wengi sana mtaani na hawana pa kwenda. Hali iliyopo sasa MTU MWENYE DEGREE ANAWEZA KUWA MUUZA MAHINDI YA KUCHOMA BARABARANI AU anauza nyanya tu
Sasa unajiuliza Huyu mtu kapoteza miaka zaidi ya 16 kusotea kuuza nyanya ni UPUUZI WA Hali ya juu, wakati huo kuna mtu kaishia darasa la saba (kama yupo smart) kwa miaka hiyo kumi na sita ambayo mtu anatafuta degree utakuta maisha yake amejipanga na tayari ameshakuwa na vitu muhimu kulingana na mahitaji ya binadamu.
Hapo ndipo utakaposhangaa msomi kasota miaka yote hiyo na mtaani akirudi anaonekana hana maaana na hata akitaka baadhi ya kazi alizosomea miaka yote hiyo atahitajika awe na uzoefu wa miaka kadhaa ni upuuzi mkubwa sana na bado msomi huyu akichelewa kupata ajira na kwa bahati nzuri akafanikiwa baada ya miaka kadhaa kuipata hiyo ajira utakuta anaishi na MADENI maisha yake yote ya utumishi.
Ili kuboresha mfumo wa elimu nchini Tanzania ipo haja ya Huyu Waziri Ndalichako na kundi lake kuondolewa katika sekta hii maana ni kama hawajieliwi kwa sababu wao wanaamini katika mfumo wa kutupa wasomi mtaani na bila kujua kile walichowaandalia kina manufaa gani mtaani na kufanya thamani ya elimu kushuka kwa speed kubwa sana.
Anatakiwa kiongozi katika sekta hii awe na uthubutu wa kuvunja baadhi ya mitaala isiyokuwa na TIJA na awe na uwezo wa kutatua changamoto ya thamani ya elimu na mazingira ya kiuchumi kwa msomi atakaye kuwa yupo mtaani Kwan kwa hali iliyopo sasa ni mbaya sana.
Profesa huyu ana amini katika makaratasi yasio endana na uhalisia inasikitisha sana na kutia aibu sana ELIMU YA TANZANIA NI TAKATAKA na Ndalichako hatoshi kwenye mfumo, ukweli huu lazima usemwe ili tujenge mfumo mpya kwa vizazi vijavyo.
Kuna kitu kinaitwa system thinking.
Toka dunia imeanz licha ya technolojia kubwa umaskin, maradhi na vita havijawahi kukoma ni matatizo constant.
Tatizo la elimu linaenda mbali zaidi ya wizara ya elimu inayaoongozwa na Ndalichako,
Ukifuatiliwa kwa makini hata huko amerika na ulaya mifumo yao inakosolewa sana
na wazawa sababu kubwa ya elimu kutokidhi viwango vinavyotakiwa ni pamoja
na kuamin kuwa huyu mwanadam akipatiwa elimu realy atakuwa hatabiriki kama kesho
ataamka na ajenda gani na itakuwa na madhara gani kwa watawal.
Machiavele alipo ulizwa kipi bora kiongozi aogopwe au apendwe alijibu ni bora kiongozwi aogopwe.
Imagine unakuwa mtu ambaye huna cha kuogopa(huna cha kupoteza) unakuwa hautabiriki tena
na unaweza kumchallenge mtu yeyote i.e kama watu wachache tu wakii-challenge selikari wanaandamwa vile kama polepole au gwajboy au lissu vip uwe na taifa la watu mil20 tu wa vile?
Ndio maana elimu ika shift kutoka kuwa critical and creative thinking kwenda kuwa elimu ya kutoa ujuzi(skills) tu.
NB: ikumbukwe elimu ni silaha ya kupambana na ujinga na ukiushinda ujinga umeishinda hofu kwa sababu hofu
ni matokeo ya ujinga.