kujiua ni mwendelezo wa ubinafsi alionao binaadam.kuna kipindi binti niliyempenda na kuwa naye ktk uhusiano,aliniandikia tu sms"sikupendi fulani nina boyfriend nampenda tayari"hii sms ilikubali kuingia kichwa baada ya mwezi,baada ya kupiga simu,sms hazijibiwi.nikaanza kukosa nuru rohoni na kukonda kwa kasi sana,hamu ya msosi ikakata,kila nikimuona facebook anampost na mpenziwe natamani nawaza mambo mengi sana,labda kazi niliyo nayo!!!au sikuwa nampa hela sana!!labda sijui kuvaa kama jamaa yake!!,lakini baadae sana nikashtuka kwamba haya ni mawazo tu nawaza mimi kama hajanambia yeye sababu na hataki kupokea hata simi zangu basi,landa ni kweli hanipendi wacha nimwache kwa amani.baadae nikaja gundua kumbe najiendekeza,mademu ni wengi sana na maisha lazima yandelee.
binafsi kwa sasa nina watoto wawili+mke,ndugu zangu 4 wa tumbo moja,baba na mama yangu,wote hawa wataumia zaidi ya ninavyoumia mimi wakati maumivu hayo yananipeleka huko yakifanikiwa.
njia bora ya kupanchi haya majanga ni kushirikisha watu wako wa karibu,hao nilio wataja kwa upande wako,marafiki wa karibu jamaa na wasela wako mnaojuana japo kwa uchache,utajua ni kiasi gani kujiua ni uamuzi wa hovyo.
1.unajiua kwa kuachwa na mpenzi,kuna wenzako walimfuma ndani na maisha yaliendelea.
2.unajiua kwa kukosa kazi,kuna mtu hana hela hata ya kununja chakula,na bado ana tumaini na kesho.
3.unajiua kwa kuwa kilema ama muonekano mbaya,nguruwe anachukiwa na dini nzima na ndio kwanza ananenepa,jifunze kujipenda kwanza.
4unajiua kwa kukataliwa na ndugu,kuna watu wanaenda nchi za watu huko hawana hata mtu wanayemjua,wanaota na vitambi,bro unafeli.
5.unajiua kwa majibu mabaya ya vipimo vya hospital,kuna watu wamepewa majibu wamebakiza masaa kadhaa wafariki,na bado wana tumaini.
ni uamuzi wa hovyo sana kuwaza kujiua.