The next is me sidhani kama huu mwezi utaisha,kwaherini wana jf
Acha ujinga.. Unadhani kujimaliza ndio tatizo, fikiria matatizo yako ukijiua uzito kiasi gani unaenda kwa wale wanaokutegemea, kiasi gani unawaacha na majonzi..
Mtume s.a.w anasema, usijilinganishe na wajuu yako, jilinganishe na wachini yako... Utaona neema za mola kwako..
Kama ni maradhi kuna watu wana maradhi ya hatari huko mahospitalini, kama ni dhiki, kuna watu wan dhiki za kila rangi we mpaka simu ya kuchat jf unayo
Kama ni stress za mapenzi, umechukuliwa demu/mke ndio we ukijiua na kikojoleo chake unaondoka nacho!!? [emoji848], we unakufa huku duniani watu wanaendelea kuruka nae vizuri tu
Pambana maadui zako siki wakuheshimu
Kama ni kufirisika, kuna watu wamefirisika si mchezo..
Kwangu kujiua ni wazo la kifala zaidi kuliko mawazo yoote, labda mtu aliyerogwa..
Mfikirie mzazi wako yupo, fikiria wanao kama wapo n.k
Shida tumeumbiwa sisi, hiyo ni mitihani tu na lazima tuishinde.
Achana kabisa na huo ufala kaka.
Jama jama jama, mie najitolea kwa yeyote yule mwenye fikra za kujiua, kumsaidia kadri niwezavyo... Uwe na ndugu jamaa au rafiki usisite kunicheki