Kwa wanaume. Hakikisha hukosi hivi nyumbani kwako

Mr DIY

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2016
Posts
1,188
Reaction score
2,553
Kwa wanaume wenzangu habari za muda huu, naomba niende moja kwa moja kwenye mada husika kama nilivyoitambulisha hapo juu. Ikiwa una familia au unaishi bachelor tafadhali zingatia hili linakihusu.

Nyumbani kwako hakikisha mwanaume hukosi essential tools kadhaa kwa ajili ya kupunguza changamoto ndogo ndogo ukizingatiwa wewe ni mwanaume, familia nzima itakutegemea wewe. Vifaa muhimu kabisa hutakiwi kukosa kwako ni kama ifuatavyo:

1. Tester ya umeme. Hakikisha hiki kifaa hukosi kwako, kitakupunguzia ajali kwako za umeme kwa kutambua wapi kuna leakage ya umeme pia itakusaidia ku repair issue ndogo ndogo zinazohusiana umeme kwako, imagine hata kubadilisha holder ya balbu ya taa chumbani kwako uende kumwita fundi aingie chumbani kwako na mkeo.

2. Nyundo ndogo. Vifaa vingi ndani ya nyumba vimeundwa kwa misumali, sasa hata kugongea msumali ulio loose ushindwe?

3. Screw driver. Wengine wanaiita "bisibisi" siku hizi kuna set hata machinga wanaziuza itakusaidia hata kukaza nati ya kitasa chako cha chumbani

4. Panga. Licha ya kazi nyingine ni silaha pia.

5. Jembe. Kila mtu anajua kazi yake

6. Shoka, sururu, kwanja hii inategemea na mazingira yako

7. Tool box, sio lazima liwe special weza tengeneza la mbao au chuma, hifadhi powertools zako.

8. Drills, siku hizi kuna simple drills zinauzwa madukani tena za kuchaji ambayo una regurate speed unaweza tumia kama drill au hata kama screw driver, bei yake inategemea ila ni tool muhimu sana, imagine chumban kwako sasa hivi ukitaka tundika tv ukutani unafanyaje? Utamwita fundi chumban kwako? Kuitumia ni rahisi sana tena YOUTUBE WANAFUNDISHA.

9. Spana. Hapa si lazima uwe na set nzima angalau hata ile adjustable ambayo inaweza fanya kazi kwenye nati tofauti tofauti.

10. Koleo (pliers) siku hizi zipo zenye kazi hadi 4 ndani ya moja

11. Chepe. Hata kuzoa taka ndani ya nyumba uweze, usishindwe hata chimba shimo la taka

12. Reki. Usiwe kila siku wa kuazima reki ya sh 5000

13. Baiskeli. Hii kwa mazoezi, kama nafasi yako ni ndogo siku hizi zipo unazoweza kuzikunja na kuhifadhi sehemu ndogo.

14. Misumari, akiba ya misumali saizi tofauti tofauti itakusaidia repairs zisizotarajiwa

15. Air pump yoyote hata ya mkono. Kama unamiliki chombo chochote cha usafir kilicho na tire ya kujaza upepo usikose hii kitu, imagine umeamka pikipiki au gar imepungua sana upepo utafanyaje? Ndio wamwita fundi? Jaza upepo ukusogeze kwenye tire services

16. Torch. Kazi ya tochi inajulikana kuna wenzetu hata tochi ya battery hana, dharula haina hodi

17. Mashine ya kunyolea (homecut). Kama una watoto hakikisha una mashine yako, weekend watoto unawanyoa mwenyewe, hii inaongeza mapenz ya baba na watoto.

18. Msumeno, yes kwenye toolbox yako uwe na msumeno mdogo hata ule wa 5000 utakusaidia siku moja

19. Mzani, hata ule simple wa spring unaoishia kilo 5 wa bei ndogo sana, kuna siku utakupunguzia kazi hapo kwako.

20. Toroli, kama unaishi nje ya mji toroli muhimu sana kwa shughuli ndogo ndogo nyumbani, usipende kila kitu kubeba utapata madhara ya mgongo.

21. Extension ya umeme, yes kaa na extension ya ziada ya umeme, kuna siku utahitaji kuliko kwenye wagongea majiran upate fedheha.

Kwa mwingine anaeweza endeleza list, share nasi
 
Wee bado mtoto sana kimaisha, Condoms ziko wapi? Hujui mwanaume ukifa sbb hutumii condoms familia na wategemezi wote wataumia sana..

Condoms ingekuwa ya kwanza katika hiyo list, alafu acha ujinga plz, zana zingine ndio zifuate.
 
Wee bado mtoto sana kimaisha, Condoms ziko wapi? Hujui mwanaume ukifa sbb hutumii condoms familia na wategemezi wote wataumia sana..

Condoms ingekuwa ya kwanza katika hiyo list, alafu acha ujinga plz, zana zingine ndio zifuate.
Condom sio powertools mzee, hiyo ni sehemu ya medical supplies ndio maana sjaongelea hata Paracetamol, cotton wool au iodine tincture ambavyo pia ni muhimu kuwa navyo nyumbani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…