Kwa wanaume tu! Makosa haya 10 ya uvaaji yatakushushia "CV" yako, Yaepuke!

Kwa wanaume tu! Makosa haya 10 ya uvaaji yatakushushia "CV" yako, Yaepuke!

Joseverest

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2013
Posts
52,812
Reaction score
71,392
1.Kuvaa mkanda uliochakaa licha ya kuvaa viatu vizuri, suruali na shati la kisasa kabisa!

2.Kuruka Ruksi wakati wa kuvaa mkanda. Daima hakikisha mkanda wako umepita kwenye ruksi husika kabla hujatoka nyumbani

3.Kuvaa Soksi tofauti/zilizochakaa au kutovaa kabisa Licha ya kuonekana nadhifu kwa nje

4.Kutokubeba kitambaa matokeo yake unapiga chafya na kujifutia mikono, kisha kwenye nguo!

5.Kujaza vitu mifukoni matokeo yake mifuko inatuna

6.Kuruka vifungo vya shati

7.Kuvaa nguo bila ya kunyoosha

8. Shati Kubwa-Suruali ya kubana mpaka inaacha “mali” yako yote nje, au Shati la kubana-Suruali kubwa!

9. Rangi ya t-shirt ya ndani kuwa na rangi ya tofauti kabisa na shati ya nje! Mbaya zaidi t-shirt inang’aa na shati linaangaza

10.Kuchomekea kwenye nguo ya ndani ukidhani umechomekea kwenye suruali!
 
Bro kwa mtu anaye tafuta kazi au? Umesha ona Manji anavyo Vaa? MMBUNGE wa GEITA Anavyo vaa na bado CV zao zipo pale pale..ebu tupeane deal za kupata pesa nyingi apa tawn...ili tuandae kazi kwa watu wafanye siyo kutafuata kazi tufanye..i l mean watafuta kazi ndo ndo future Staff wetu....
 
Smartness pays
 
KWA kweli mimi huwa isvai nguo chafu lakini nimejikuta tu sina tabia ya kupangilia nguo....na ata nikienda kufanya manunuzi huwa sizingatii rangi wa uzuri wa nguo huwa nanunua tu kwa kuwa inanitosha...kuhusu hayo uliyo andika nashukuru umeniongezea kitu lakini sidhani kama yatanibadilisha.
 
Mabishoo bwana, wenzako tunahangaika kupangilia maisha wewe unang'ang'ana kupangilia nguo. Haya ndo mambo ya vijana wa Dar bwana.
 
Back
Top Bottom