Kwa Wanayanga: Nini Kifanyike ili Yanga icheze Fainali ya CAF Champions League msimu ujao

hata wachezaji wa kaskazini(waarabu)wanajua kumzonga refa.refa anajikuta anaweka tuta au faulo au kubadili maamuzi kwasababu ya kuzongwa zongwa tu wachezaji.
 
Tusajili wachezaji warefu hasa back Ili kuwin aerial balls, baadhi ya magori tunafungwa kwasababu wachezaji Wana vimo vya wastani
 
Waboreshe maslahi kwa wachezaji+ benchi la ufundi na waepuke uswahili ili hiki kikosi kiendelee kuwepo na zaidi wakiboreshe zaidi.

Wanamhitaji mtu mjanjamjanja aina ya Tumisang Orebonye hapo mbele ni walewale akina Khama Billiat.(forward nyoronyoro)

Ukimgusa tu akiwa na mpira kwenye eneo la hatari tayari yupo chini,hawa huamua sana matokeo mechi zenye presha kubwa.
 
Wings zipatikane mpya, wenye uwezo sio wa kupiga chenga tu hata kupiga nje ya Box, tuna tatizo la upigaji wa mashuti nje ya box, na game nyingi za hatua za Mtoano unahitaji magoli mengi ya aina hiyo.

Beki ya kushoto ya uhakika zaidi, sio tu awe na ball control kubwa ila pia awe na nguvu ya kubattle.

Tunahitaji Modern no. 8, na 6 mpira wa sasa unahitaji zaidi maamuzi ya Haraka.

Mwisho kabisa tupate Straika au Namba 10 wa kariba ya Ngonga wa TP Mazembe.
 
Kwangu Mimi. Usajili wa Kwanza ni kubakiza Nabi na timu hii. Cha pili, wanahitaji wachezaji wanne wazuri wa Kigeni kwa nafasi za yule Kipa Johora, BM33, Beki Mmali na Tuisila. Wasajili Winga Mzuri napendekeza yule Kinzumbi wa TP Mazembe. Wasajili yule Kijana wa Kibrazili wa Singida Big Stars(Acheze 8 au 10) na striker mmoja atakaye compete na Mayele(Malepo wa Alh Hilal kwani wanapogana vita) pia waongeze kiungo mwingine.
 
Wampe Nabi mahitaji anayo yataka,wamwachie yy apendekeze wachezaji wa kiwasajili na mwisho viongozi waache ubahili, hela ambayo Yanga kaingiza kwenye michuano hii ina karibia dola 3m,inatosha kufanya usajili wa wachezaji hawa 3-5 wakubwa na nyingine tufanyie mambo mwengine.

Tukifanikiwa kumbakisha Nabi,Mayele na Diara ,tutakuwa hatari sana.
 
mm ushaur wangu kwa yanga ni wachezaj waongezewe mazoez ya kubeba tofar za inchi sita zinasaidia sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…