"Yanga hawajafa KIUME wala hawajafa KISHUJAA.
Vita inapofika MWISHO wanajeshi wote—walioshinda na walioshindwa—hurudi nyumbani wakiwa HAI. Waliokufa ni wale ambao hawakufika mwisho wa mpambano.
Yanga HAWAJAFA kabisa. Wamefika mwisho wa mpambano na sasa wanarudi nyumbani wakiwa HAI." Maundu Mwingizi
Kwanza niipongeze timu ya Yanga Kwa kufika Fainali ya Kombe la shirikisho barani Afrika, hii ni mara ya Kwanza Kwa timu ya Tanzania kufika hiyo hatua kubwa kabisa. Tumekua tukishuhudia timu za kaskazini na walau Kwa ukanda huu wa kusini mwa jangwa la Sahara ni timu za Congo na Afrika kusini pekee ndo hua zinafika hiyo hatua.
Hii sasa italeta hamasa kuelekea msimu ujao. Kikubwa tujipange kuboresha kikosi. Viongozi wafanye usajili kulingana na matakwa ya mwalimu Kwa kuzingatia nafasi zinazopwaya....
Hakika tulikua na msimu Bora Sana, na tumepata mafanikio makubwa Sana lakini tunatakiwa kufanya makubwa zaidi.
Karibu mwananchi mwenzangu tujadili maboresho na mapendekezo ambayo tunapaswa kufanya ili msimu ujao tufike Fainali ya CAF Champions League...
View attachment 2645534View attachment 2645536