Kwa Wanayanga: Nini Kifanyike ili Yanga icheze Fainali ya CAF Champions League msimu ujao

Kwa Wanayanga: Nini Kifanyike ili Yanga icheze Fainali ya CAF Champions League msimu ujao

Nitajie bara ambalo timu zote huchukua kombe
Kama unajua hivyo hoja Yko inakosa mashiko moja kwa moja . Timu ulizozitaja haziwezi kuwa kipimo cha timu na mashindano yote Na ushindi siyo kombe tu. Miaka yte simb walishiriki si walipata pesa na nchi kuongeza nafasi? Hayo siyo mafanikio???
 
"Yanga hawajafa KIUME wala hawajafa KISHUJAA.

Vita inapofika MWISHO wanajeshi wote—walioshinda na walioshindwa—hurudi nyumbani wakiwa HAI. Waliokufa ni wale ambao hawakufika mwisho wa mpambano.

Yanga HAWAJAFA kabisa. Wamefika mwisho wa mpambano na sasa wanarudi nyumbani wakiwa HAI." Maundu Mwingizi


Kwanza niipongeze timu ya Yanga Kwa kufika Fainali ya Kombe la shirikisho barani Afrika, hii ni mara ya Kwanza Kwa timu ya Tanzania kufika hiyo hatua kubwa kabisa. Tumekua tukishuhudia timu za kaskazini na walau Kwa ukanda huu wa kusini mwa jangwa la Sahara ni timu za Congo na Afrika kusini pekee ndo hua zinafika hiyo hatua.

Hii sasa italeta hamasa kuelekea msimu ujao. Kikubwa tujipange kuboresha kikosi. Viongozi wafanye usajili kulingana na matakwa ya mwalimu Kwa kuzingatia nafasi zinazopwaya....

Hakika tulikua na msimu Bora Sana, na tumepata mafanikio makubwa Sana lakini tunatakiwa kufanya makubwa zaidi.

Karibu mwananchi mwenzangu tujadili maboresho na mapendekezo ambayo tunapaswa kufanya ili msimu ujao tufike Fainali ya CAF Champions League...
View attachment 2645534View attachment 2645536
Huko Hakuna rivers, bamako. Huko Kuna raja, widadi, Esperance nk

Mkumbuke Hilo.
 
Hao wachezaji wapo ila bei yake sasa...ndio kizingimkuti.

Klabu yako bado haina hela..tuongee ukweli..tusiwe wanafki..

Sent from my SM-A310F using JamiiForums mobile app
Wapo wengi tu mfano namba 8 hata ile team ya mali kuna namba 8 mzuri sana pale anamiliki mpira na anapiga pasi kiusahih na first touch yake ni fire
 
Back
Top Bottom