Kwa Wanayanga: Nini Kifanyike ili Yanga icheze Fainali ya CAF Champions League msimu ujao

Kwa Wanayanga: Nini Kifanyike ili Yanga icheze Fainali ya CAF Champions League msimu ujao

Hii ni kwa sababu watu wengi hawajui.

Angalia sasa hivi wanavyocheza akina Mamelodi..wanajua kila kitu..wana bajeti kubwa na pia wana mipango mingi.

Ukicheza nao hata kama utawazidi kila kitu wanajua unachowazidi ni nini na wanatakiwa wafanyaje ili wakuepuke.

Hivi ndio sisi wa afrika mashariki hatuvijui.

Tunapaswa kuwashukuru sana Simba kutufungulia mwanya huu wa kujifunza zaidi kwenye mpira..na kujaribu mbinu mpya rahisi na ngumu.

Timu za kaskazini wakishajua unajua zaidi yao..wanaogopa..wanaanza kucheza vituko..fitna na kadhalika..na inasaidia kwa sababu mru mweusi anawahi kupanick na kutoka mchezoni.

Niliona mamelodi walivyocheza na wale wydad sijui..

Mechi ya kwanza wamechezewa figisu flani za kijinga..wakala nyekundu mbili..ingawa hawakufungana..alafu mechi ya pili wakalazimishwa sare ya magoli ambayo imewaumiza na kutolewa.

Na hapo kumbuka kua mamelodi anajua sana zaidi ya aliyecheza naye...

Sent from my SM-A310F using JamiiForums mobile app
hata wachezaji wa kaskazini(waarabu)wanajua kumzonga refa.refa anajikuta anaweka tuta au faulo au kubadili maamuzi kwasababu ya kuzongwa zongwa tu wachezaji.
 
Tusajili wachezaji warefu hasa back Ili kuwin aerial balls, baadhi ya magori tunafungwa kwasababu wachezaji Wana vimo vya wastani
 
Waboreshe maslahi kwa wachezaji+ benchi la ufundi na waepuke uswahili ili hiki kikosi kiendelee kuwepo na zaidi wakiboreshe zaidi.

Wanamhitaji mtu mjanjamjanja aina ya Tumisang Orebonye hapo mbele ni walewale akina Khama Billiat.(forward nyoronyoro)

Ukimgusa tu akiwa na mpira kwenye eneo la hatari tayari yupo chini,hawa huamua sana matokeo mechi zenye presha kubwa.
 
Wings zipatikane mpya, wenye uwezo sio wa kupiga chenga tu hata kupiga nje ya Box, tuna tatizo la upigaji wa mashuti nje ya box, na game nyingi za hatua za Mtoano unahitaji magoli mengi ya aina hiyo.

Beki ya kushoto ya uhakika zaidi, sio tu awe na ball control kubwa ila pia awe na nguvu ya kubattle.

Tunahitaji Modern no. 8, na 6 mpira wa sasa unahitaji zaidi maamuzi ya Haraka.

Mwisho kabisa tupate Straika au Namba 10 wa kariba ya Ngonga wa TP Mazembe.
 
Kwangu Mimi. Usajili wa Kwanza ni kubakiza Nabi na timu hii. Cha pili, wanahitaji wachezaji wanne wazuri wa Kigeni kwa nafasi za yule Kipa Johora, BM33, Beki Mmali na Tuisila. Wasajili Winga Mzuri napendekeza yule Kinzumbi wa TP Mazembe. Wasajili yule Kijana wa Kibrazili wa Singida Big Stars(Acheze 8 au 10) na striker mmoja atakaye compete na Mayele(Malepo wa Alh Hilal kwani wanapogana vita) pia waongeze kiungo mwingine.
 
"Yanga hawajafa KIUME wala hawajafa KISHUJAA.

Vita inapofika MWISHO wanajeshi wote—walioshinda na walioshindwa—hurudi nyumbani wakiwa HAI. Waliokufa ni wale ambao hawakufika mwisho wa mpambano.

Yanga HAWAJAFA kabisa. Wamefika mwisho wa mpambano na sasa wanarudi nyumbani wakiwa HAI." Maundu Mwingizi


Kwanza niipongeze timu ya Yanga Kwa kufika Fainali ya Kombe la shirikisho barani Afrika, hii ni mara ya Kwanza Kwa timu ya Tanzania kufika hiyo hatua kubwa kabisa. Tumekua tukishuhudia timu za kaskazini na walau Kwa ukanda huu wa kusini mwa jangwa la Sahara ni timu za Congo na Afrika kusini pekee ndo hua zinafika hiyo hatua.

Hii sasa italeta hamasa kuelekea msimu ujao. Kikubwa tujipange kuboresha kikosi. Viongozi wafanye usajili kulingana na matakwa ya mwalimu Kwa kuzingatia nafasi zinazopwaya....

Hakika tulikua na msimu Bora Sana, na tumepata mafanikio makubwa Sana lakini tunatakiwa kufanya makubwa zaidi.

Karibu mwananchi mwenzangu tujadili maboresho na mapendekezo ambayo tunapaswa kufanya ili msimu ujao tufike Fainali ya CAF Champions League...
View attachment 2645534View attachment 2645536
Wampe Nabi mahitaji anayo yataka,wamwachie yy apendekeze wachezaji wa kiwasajili na mwisho viongozi waache ubahili, hela ambayo Yanga kaingiza kwenye michuano hii ina karibia dola 3m,inatosha kufanya usajili wa wachezaji hawa 3-5 wakubwa na nyingine tufanyie mambo mwengine.

Tukifanikiwa kumbakisha Nabi,Mayele na Diara ,tutakuwa hatari sana.
 
mm ushaur wangu kwa yanga ni wachezaj waongezewe mazoez ya kubeba tofar za inchi sita zinasaidia sana
 
Back
Top Bottom