Kwa wapenda safari na kutalii vya ndanii

Kwa wapenda safari na kutalii vya ndanii

Kijana Jr

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2016
Posts
564
Reaction score
889
Habari wanaJamiiForums, tunaopenda kusafiri iwe nje au ndani ya mipaka ya tanzania.

Kusafiri ni raha sanaa kunaufanya ubongo upate maarifa mapya, mtu anajifunza mengi sana kuanzia kubadirisha mtazamo wa mtu na kujifunza mambo mbali mbali ya ulimwengu.

Je ushawahi safiri ndani ya nchi kutoka wilaya moja kwenda wilaya nyengine ndani ya mkoa mmoja?

Kuna kitu gani huwezi kusahau?
Na nini ulijifunza katika safari yako?

Binafs safari yangu ya kuvutia zaidi ni kutoka wilaya ya ulanga mkoa morogoro kwenda wilaya ya mvomero Morogoro yani ndani ya mkoa wa Morogoro mkoa mmoja tu huo huo ni safari ndefu zaidi ya masaa 10 kwa gari yani umbali kama wote vile! Sawa na kutoka arusha kwenda Dar es salaam Unakaa kwenye gari mpk unajisahau,

sanje water fail,udzungwa mountains,great ruaha river ,mikumi national park

Visit morogoro
 
Kutoka Iringa kwenda Dodoma pale katikati kuna njia inaitwa mlima nyoka (sijui nimepatia)

Daah pale siwezi kupasahau maana abiria wenzangu walikuwa wanapiga kelele na story zao uchwara ila walipofika pale walikaa kimya ghafla kwa jinsi zile Kona za mlimani zinavyotisha
 
Wazungu ndo hua tunawachaji ivo wala sio uonevu mna ukienda kwao izo bei zao heheeeee ni pasua kichwa kwaio tunafanya Tit for tat is a fair game
Ngoja niscreenshot hii mkuu. Tukijipanga tutakucheki utupe ABC.
 
Majukumu yanatufanya tusisafiri safiri, ukigeuka huku ada, ukigeuka kule kodi, ukigeuka kule tena mafuta kupanda bei, ukienda kule sadaka ya kujimaliza; kwa mazingira hayo, utapata furaha ya wapi ya kusafiri safiri?​
 
Back
Top Bottom