Drishyaam ya ajay devgan ni muvi kali kinyama.ngoja niwape trela yake.
Ajay aliacha shule hajafika hata form4 ikabidi ajiajiri akafungua tv cable katika huo mji wao na kuendesha maisha yake na familia yake ya mke na watoto wawili wa kike mmoja akisoma chuo mwingine elementary.
Ajay ni mtu anapenda kutazama muvi hiyo inamfanya hadi wakati mwingine kuchelewa nyumbani au kurudi asubuhi kabisa.
Kuna kijana wa kiume mtoto wa IGP wa polisi alikuwa akisoma na mtoto wa ajay.kuna siku mtoto wa ajay aliingia bafuni kumbe yule dogo katega kamera ili aitumie hiyo video kwa kumtisha mtoto wa ajay afanye nae mapenzi!
Kiburi cha mtoto wa IGP kikampeleka hadi kwa ajay ndani na kutaka kumbaka yule mtoto kilichotokea ni bahati mbaya yule mtoto akapigwa kichwani akafa!
Usiku sana ajay anarudi na kukuta huo mkasa wa kuuliwa mtoto wa igp na kuzikwa uwani kwake.
Hapo ndipo anaposolve hiyo crime kwa kutumia mifano ya muvi alizokuwa akiangalia na kufanikiwa ingawa wote yeye na watoto wake na mke walikula kichapo cha haja