Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Nashukuru mkuu kuna baadhi nimeziona kama Quuen Seondeok, Emperor of the sea, Kingdom of the wind ndio land òf the wind ya Yiri mtoto wa Jumong?
 
Shukrani sana mkuu
 
Naomba link ya dramacool Og mkuu niendeleze Dae Jo Young maana niliclear history nikapoteza sasa nikigugo zinakuja dramacool fake link ya mwanzo nikipata humu kuwa mdau alituma.

Nimezoea dramacool kimoi nimeingia sasa adds kibao mpaka nimeshindwa kupakua muvi.
 
Dramacool Og ipo ila ukigugo unakuta pacha wake kila kitu Sawa ila ukija kuidownload mizinguo wankupeleka mdundo.com unapotea ,mimi niliingia kwa msaada wa link humu bahati mbaya nimesahau hiyo page niichukue .
 
The Secret Romantic Guesthouse (2023) Korean Drama | Dramacool

Link ya dramacool hio
Dramacool Og ipo ila ukigugo unakuta pacha wake kila kitu Sawa ila ukija kuidownload mizinguo wankupeleka mdundo.com unapotea ,mimi niliingia kwa msaada wa link humu bahati mbaya nimesahau hiyo page niichukue .
 
Chief kim ni mwehu,
Chief ni mjinga,
Chief kim ni madenge mwenye elimu,
Chief kim ni chepe mwenye elimu,
Chief kim ni mwanadamu mwenye maudhi,
Chief ni kibilisi makero,
Chief ana roho nzuri,
Chief na ulipaji kisasi usio umiza.

Hii drama nakumbuka mwaka jana nilishusha episode zote 20, nikaingalia kwa dakika 20 then ni mwendo wa delete.

Nimepatwa na arosto ya kumuangaliaa namgoong min.

Nimeishusha tena, najishangaa hii drama nakwenda nayo kwa speed ya kinzhal missile.


Hakuna drama mbaya duniani,
Ishu ni timing na mudi yako mwenyewe.
 
Kama unahisi taste zetu zinafanana, itafute Jealousy Incarnate/ Don't dare to dream...Mimi binafsi nimeipenda sana japo episode za mwanzo inaboa kidogo
View attachment 2645714
Nilibahatika kuiangalia kwa episode 8, episodes zake hazikushiba sana ikanibidi niiweke pending.

Love triangle ilikuwa inakwenda vyema,
Nilipenda upinzani wa jadi waliokuwa nao wale anchors wawili ma ahjumma.

Wote walikuwa wanagombea ulezi wa binti oohhh nimeshamsahau jina lake mpaka niende google (moon ga young)

Ikitokezea siku wamevaa sare basi ofisini inakuwa ni vita,

Walivyokuwa wanajibebisha kwa bwana mpishi wa mgahawani
Waooooww!!!
Walikuwa ni vichaa


Yule mwehu na binti siku waliokutana wodini, aigooo
Mvulana yule alipokwenda kutibiwa kensa ya titi ilikuwa kitahanani wodini na ofisini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…