Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Hongera sana Damushin kwa kutimiza miaka mitatu ndani ya hii miaka wengi tumenufaika na uwepo wako na tunatarijia kunufaika zaidi Mungu jalia. Noona anasema asante sana kwa sifa kem kem ulizommwagia, nimefurahi kumuona huyo dogo hapo nilimpenda sana kwenye Dr stranger.
  1. hahahahaaa sijakusifia ila nimekupa ukweli noona, laiti kama ingelikuwa kinyume chake basi ningelikuwa nimekuchamba kwa maneno ya wanawake wa mjini.
  2. hahahaaaaa kama JF ingelikuwa ni chuo kikuu basi noona unapaswa uwe na elimu ya master mimi niwe na diploma yenye supplementary 3 kwa kila semester.
  3. kiukweli inafika wakati baadhi ya thread nikizitembelea huwa najiuliza inawezekanaje kuna watu wanaweza kujenga hoja kama hivi na mbona mimi nashindwa, kiukweli JF ni hazina kubwa sana na popote alipo aliekuja na wazo la kuanzisha mtandao huu mungu amzidishie baraka na furaha na sisi sote atujaaalie maisha yenye furaha, amani, atuzidishie hekima na atupunguzie wivu (lakini si wa kupenda) na atuondolee chuki binafsi kwenye nafsi zetu.
 
hahahaaaaaa kuna waigizaji wa kiume hata kama binti ni kilaza basi atang'arishwa akitaka asitake,hivyo hivyo kwa muigizaji kilaza wa kiume akikutana na muigizaji hodari wa kike naye atang'arishwa akipenda asipende.
Akipenda mungu wiki hii nitaitafuta doctors ili nimuangalie yeye tu na si park shin hye japo kuwa si mpenzi mkubwa sana wa medical drama.
https://ondramanice.io/drama/doctors-detail
basi siku moja nilitembelea forum soompi special thread ya kingdom of the wind ili nijifunze masuala mbali mbali kuhusiana na production ya drama ile, asilimia kubwa ya mashabiki walikuwa wanamponda sana mwanadada choi jung won, wengi wao walikuwa wanamuona uwezo wake ni mdogo kusimama pamoja na king of historical drama( song il kook/guk). mwisho wa siku kwenye KBS drama awards za mwaka 2008 alipata tunzo tatu ikiwemo ya best actress. mashabiki wengi hawakufurahishwa kwani wengi waliamini sung yuri aliyeigiza hong gil dong ndiye anastahili tunzo ya best actress.
lakini nilipenda style yake ya kuvaa magauni mawili kwa usiku mmoja,hahahahaaaaahaaaaaaa alikuwa anaingia na kutoka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kama waimbaji wanapofanya matamsha.
kbsaward_song_choi2.jpg

kbsaward_choijungwon3.jpg

mimi naamini song joong ki amen'garishwa na song hye kyo kwenye descendent of the sun drama.nitaendelea kuamini hata kama stering angelikuwa kim woo bin basi mwanadada song hye kyo angelimfanya aonekane ni bora.
song.jpg
Kweli Kabisaaa,Apo Kwenye DOTS ni Hye kyo ndo Alomng'arisha uyo Hubby Wake...
 
Hahahahhahah!!! Utamaduni Siyo..

Kuzaa Mapema Damushin kuna Umuhimu Wake Basi Tuuh Tunaenda tofauti Sababu Ya Aya Maendeleo ya Tecnologia..
Duuh 37 Bado Ajaoa Lol!!!!
  1. ni kweli kuna raha yake kuzaa mapema lakini wengi wao ukiwauliza kwa nini unazaa mapema majibu yao nataka nipumzike mapema kuzaa ili huko mbele watoto wanisaidie kimaisha.hapa mtaani kwetu nina rafiki yangu amefunga ndoa mwaka uliopita na amebahatika kupata mtoto na kiumri amenipita kwa mwaka mmoja,inamaana akiingia kwenye umri wa utu uzima atakuwa na mtoto ambaye ameshakuwa kijana, inapendeza sana.
  2. lakini wengi wetu maisha ya ndoa tunayoishi ni mabovu sana na yana sikitisha na si sababu ni umasikini, utakuta mwanamme anamuachia mwanamke tu jukumu la kulea watoto, kazi kubwa anayoifanya mwanamme ni kuleta chakula na huduma nyengine za kifamilia tu.
  3. na ukimkuta mwanamke hajielewi ndio mtihani unaanzia hapo, huku zanzibar wasichana wengi wanaolewa wakiwa na miaka 18 -22, wakati huu ni umri ambao alistahili ajishughulishe kwa kujifunza japo fani ya ushonaji wa nguo ili huko mbeleni apate japo kujishughulisha na kuacha utegemezi kwa mwanamme.
  4. na wanaume wenyewe ndio sisi kina Damushin, tukitoka kwenye shughuli zetu za kutafuta riziki hatuna habari ya kuuliza hata watoto wameshindaje,hata mabuku ya skuli hatuyaangalii, tunakaa vibarazani na kupiga stori za CUF na CCM.
  5. Matokeo yake ndani ya miaka 10 ya ndoa muna watoto 5 lakini hana hata cherehani ndani ya kuwashonea nguo watoto hamuna .tafsiri yake ni kwamba miaka 10 ya ndoa ilikuwa ni ya kuzaa tu, lakini maendeleo sifuri kwa sababu kula, kuvaa hata kabla ya kuolewa au kuoa ulikuwa huduma hizi unazipata kwa mzee wako.
  6. huwa namwambia mama yangu ya kwamba siku nitakayo jaaliwa kuowa basi mungu anijaalie kwanza nipate mke mwenye kujielewa kimaarifa na ambaye atanivumilia kwa hali nitakayokuwa nayo, hata kama niwe masikini kama maisha yetu tunayoishi basi nitajitahidi nimpunguzie mzigo wa kulea familia.katu sitataka kuishi maisha kama wanayoishi jamii kubwa ya watanzania ya kumfanya mwanamke kuwa ndio kama mtumwa wa ndani ya nyumba.
 
Aigooooo,Damushin Natamani Kujua Age Yako Japo Aihusiani...Ila Natamni

Maisha ya Sasa yapo tofauti Sana Na Walokulia Wazazi wetu Na Ata wao wakijaribu kutulea Vile Walivyolelewa Bila Kuhisi Maisha ya Sasa Yamebadirika Sana ukilinganisha na Yao...

Ila point yangu IPO pale kuwa kuna Umuhimu Sana Kuzaaa Mpema..

Nataka niandike mengi ila nashindwa Coz Natumia Simu,Nikishika Mpakato Nitaandika InshaAllah Nayotaka Kuyasema Kuhusu Hili.
 
nikimnukuu dk shika itapendeza zaidi kama ungelitaja drama zote ulizoziangalia zenye maudhui ya action ili iwe rahisi kuzitafuta na nyengine.
  1. https://ondramanice.io/drama/healer-detail
  2. https://ondramanice.io/drama/iris-detail
  3. https://ondramanice.io/drama/iris-2-detail
  4. https://ondramanice.io/drama/athena-goddess-of-war-detail
  5. https://ondramanice.io/drama/two-cops-detail : hii inaendelea
  6. https://ondramanice.io/drama/heartless-city-detail
  7. https://ondramanice.io/drama/bad-guys-detail : anza na hii kupitia (OCN)
  8. https://ondramanice.io/drama/bad-guys-age-of-evil-detail: season 2 imeanza jana kupitia (OCN). nimeangalia comment za mashabiki wanasema ni mwendo wa mapigano mpaka wakati wa ibada.
  9. https://ondramanice.io/drama/the-k2-detail
  10. https://ondramanice.io/drama/tunnel-korean-drama-detail (OCN)
  11. https://ondramanice.io/drama/signal-korean-drama--detail (OCN)
  12. https://ondramanice.io/drama/voice-korean-drama-detail (OCN)
  13. https://ondramanice.io/drama/secret-forest-detail :seoul best drama 2017. aigooooooo naomba uniagizie Bibimbap (Mixed Rice) na kinywaji cha Bokbunja ju ili nikumalizie
    EP_06_Bibimbap_-_Mixed_Rice_with_Beef___Vegetables_5.4_-_Logo-700x404.jpg
    bokbunja+ju.jpg
Shukrani kwa ku reply ila ambazo tayari nimeziona ni hizi

Bridal Mask,
City Hunter,
A Man Called God,
Iris 1,
Iris 2,
Three Days,
Criminal Mind,
Innocend Defendant,
Good Thief Bad Thief,
Faith Doctor,
Remembe The War Of Son,
Glass Mask,
Man to man.
 
inaonekana ni mpenzi mkubwa sana wa crime drama,unapaswa uache kuangalia TBC na uanze kuangalia OCN naamini hutajutia.
 
TBC umeniacha mkuu haha ni hii channel au neno la maana nyingine ?! Na OCN pia?
Pia kuhusu drama napenda za aina hiyo huwa ambazo wanachallenge na akili sana,mahakamani,watu wakicheza na system ya nchi,computer na maisha ya story za mapenzi yasitawale maana sichelewagi lala nikiwa na drama ya aina hiyo.
 
Aigooooo,Damushin Natamani Kujua Age Yako Japo Aihusiani...Ila Natamni

Maisha ya Sasa yapo tofauti Sana Na Walokulia Wazazi wetu Na Ata wao wakijaribu kutulea Vile Walivyolelewa Bila Kuhisi Maisha ya Sasa Yamebadirika Sana ukilinganisha na Yao...

Ila point yangu IPO pale kuwa kuna Umuhimu Sana Kuzaaa Mpema..

Nataka niandike mengi ila nashindwa Coz Natumia Simu,Nikishika Mpakato Nitaandika InshaAllah Nayotaka Kuyasema Kuhusu Hili.
  • umri wangu nakaribia robo karne
  • nakubaliana na msimamo wako wa umuhimu wa kuzaa mapema lakini utakapoamua kupumzika ni bora ujishughulishe na usisubiri tu watoto waje wahitimu chuo kikuu au wapate kazi nzuri ndipo waje wakufungulie duka la kuuza nguo kutoka dubai na thailand.
  • mimi nina baba yangu mdogo ameoa akiwa na miaka 42 wakati ni umri ambao unapendeza zaidi kama una mtoto mwenye umri wa miaka 17,kama maisha ni mazuri na una vitega uchumi kwangu mimi sioni tatizo kuchelewa kupata mtoto kwa sababu hata kama utakuwa umezeeka na ukafariki watoto wako hawatakuwa kwenye hali ngumu sana.labda tuchukulie mfano wa celebrity ambaye ni role model wangu kama baba bora song il kook ambaye ana miaka 46 lakini watoto wake wana miaka 6, ina maana wakifikisha miaka 20 song il kook atakuwa na miaka 60, ni umri ambao alipaswa awe na wajukuu lakini kiupande wake watoto wake watakuwa ndio wanaingia kwenye ulimwengu wa kujitegemea. ingelikuwa ni masikini basi watoto wake watakuwa kwenye mtihani kwa sababu nguvu za kutafuta maisha ukiwa na miaka 60 ni tofauti na za mika 40.
 
TBC umeniacha mkuu haha ni hii channel au neno la maana nyingine ?! Na OCN pia?
Pia kuhusu drama napenda za aina hiyo huwa ambazo wanachallenge na akili sana,mahakamani,watu wakicheza na system ya nchi,computer na maisha ya story za mapenzi yasitawale maana sichelewagi lala nikiwa na drama ya aina hiyo.
OCN ni channel ya cable ya korea kusini na ndio wanaongoza kwa crime drama ndio maana hata hiyo list niliokuwekea baadhi ya drama zilizoooneshwa na OCN.
pia nimekusudia TBC hii ya kwetu tunayoangalia taarifa ya habari za kuvutia kama
  • Damushin atoa msaada wa magari 200 kwa hospitali ya chuo kikuu cha muhimbili
  • rais atoa msaada wa billion 1 kwa kila mlemavu wa ngozi
  • muigizaji mrembo wa kitanzania aminas ashinda tunzo ya best actress kwa kumshinda song hye kyo na waigizaji wengine kutoka marekani
  • EMPTY dongsaeng ashinda tunzo ya young best programmer baada ya kuwashinda washindani wengine kutoka vyuo vya marekani licha ya kuwa amesoma computer science kwenye chuo cha mwanahakogi university ambacho hata huduma ya computer laboratory hakina.
 
TBC nifate nini boss wangu dah hata kwa channel list natanigi niitoe kwakweli
Ila hii OCN ni mpaka kuwe na access ya kisimbusi au hata simu janja au mpakato unaweza kuwa na access nayo!
 
  • umri wangu nakaribia robo karne
  • nakubaliana na msimamo wako wa umuhimu wa kuzaa mapema lakini utakapoamua kupumzika ni bora ujishughulishe na usisubiri tu watoto waje wahitimu chuo kikuu au wapate kazi nzuri ndipo waje wakufungulie duka la kuuza nguo kutoka dubai na thailand.
  • mimi nina baba yangu mdogo ameoa akiwa na miaka 42 wakati ni umri ambao unapendeza zaidi kama una mtoto mwenye umri wa miaka 17,kama maisha ni mazuri na una vitega uchumi kwangu mimi sioni tatizo kuchelewa kupata mtoto kwa sababu hata kama utakuwa umezeeka na ukafariki watoto wako hawatakuwa kwenye hali ngumu sana.labda tuchukulie mfano wa celebrity ambaye ni role model wangu kama baba bora song il kook ambaye ana miaka 46 lakini watoto wake wana miaka 6, ina maana wakifikisha miaka 20 song il kook atakuwa na miaka 60, ni umri ambao alipaswa awe na wajukuu lakini kiupande wake watoto wake watakuwa ndio wanaingia kwenye ulimwengu wa kujitegemea. ingelikuwa ni masikini basi watoto wake watakuwa kwenye mtihani kwa sababu nguvu za kutafuta maisha ukiwa na miaka 60 ni tofauti na za mika 40.
Bado Bado Lakini Kwa Umri Uo Kwaiyo Ni Lazima Usifikiri kuwa na Mtoto kwa kipindi hiki.
Maisha ni uchaguzi lakini Kwaiyo Ayo ni Machaguo yako na Sina Budi kuyaheshimu.

Ila naomba usifikie Mpaka 40 Uko bila Ya Mtoto.
 
EMPTY dongsaeng ashinda tunzo ya young best programmer baada ya kuwashinda washindani wengine kutoka vyuo vya marekani licha ya kuwa amesoma computer science kwenye chuo cha mwanahakogi university ambacho hata huduma ya computer laboratory hakina.
Eti MwanaHakogi! Hahahahaa.
Hapo ilikuwa umuweke Sheikh Google.
 
aminas leo nimeanza kuangalia IM NOT A ROBOT mpaka episode ya tatu ,hahahahahaaaaa kama ningeliendeleza kuiangalia tena basi muda huu ningelikuwa hospitali ya wagonjwa wa akili.
nimecheka sanaaaaaaaa mpaka wanakijiji walitoka majumbani mwao na kuja kuniangalia kiukweli walidhani nimechanganyikiwa.
huwa nawashangaa sana wale wanaosema korean drama stori hazibadiliki nahisi wana chuki na wajoseon.
I%27m_Not_a_Robot-P1.jpg
 
Back
Top Bottom