noona sbs drama awards nao wana category nyingi sana na halafu mwaka huu wana drama nyingi sana zilizofanya vizuri, sijaangalia suspicious partner ila nitakuwa wa mwisho kuamini ya kwamba ji chang wook atashinda grand prize (daesang awards), labda category nyenginezo atashinda. waigizaji 16 wanawania tunzo ya daesang awards kupitia sbs drama awards
- ji sung na uhm ki joon : kupitia defendant drama, sijaiangalia ila huenda ikashinda tunzo kwa sababu ilikuwa na rate kubwa sana.
- lee bo young na lee sang yoon : so cute, lee bo young ni mke halali wa ji sung naye pia anawania tunzo ya daesang kupitia drama ya whisper. hii pia sijaiangalia.
- nam goong min na yoon joon sang : kupitia drama ya distorted. hii pia siajiangalia, ila nam goong min sijui atahudhuria sherehe ipi kwa sababu kbs drama awards pia anawania kipengele cha grand prize kupitia drama ya chief kim. sijaiangalia ila ilikuwa na rate kubwa sana na huenda akashinda daesang kupitia drama hii.
- lee young ae : kupitia drama ya saimdang lights diary,ila sijui kwanini mtu wake mjr95 hagombanii tunzo hii wakati alikuwa ni muigizaji mkuu wa kiume, namzungumzia song seung hun (black). pia drama hii sijaiangalia.
- joo won na oh yeon soo : kupitia drama ya my sassy girl, niliishia episode ya 3
- lee jong suk na bae suzy : kupitia drama ya while you were sleeping.
- seo hyun jin: mmoja kati ya wanadada niliochelewa kuwafahamu katika ulimwengu wa korea drama, drama ya temperature of love ndio inayomfanya agombanie tunzo ya daesang, japokuwa sijaimaliza ila nadhani kwa waigizaji wa kike wengi huyu dada hawamuwezi labda kwa kuwa si idols ndio maana alikuwa hapewi heshima kubwa sana mwanzoni ila kwa sasa offer zinamfuata mwenyewe, bado naiangalia romantic doctor teacher kim kwa ajili yake.