D A E M U S H I N
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 22,665
- 121,102
Mwezangu Hmmm!! Mahaba Yanatuzidi Na Iyo Poster Ni Wakati Hiyo Drama Inaonyeshwa Japan Nahisi.dah mzuka wako wa simba day umekufanya utuwekee poster lenye maandishi ya kijapani.
au ndio team madeepa?
mungu azidi kumponyesha ugonjwa wa nasopharyngeal cancer na pia awape afya wagonjwa wote wanaohangaika kurudisha afya zao.
Nguvu Ya BinAdamu Wa Jinsia Ya Kike, Hiyo Ndo Nguvu Yao Kwenu Hata Uweje Ukifika Kwa Mtoto Wakike Unakuwa Kama Mkate Tuuh.hahahahahaaaaa uyo bwege madeepa ( madeera) vurugu lake lote akifika kwa beautiful lady Ae shin anatulia kama bata anapoongozana na mama yake..
ananikumbusha yeom jang kwenye emperor of the sea dhidi ya mwanadada jung hwa.
mhhhhhhhh mapenzi ni zaidi ya ugonjwa wa cancer ndio maana naogopa kuyakaribia.
fighting my brother ambaye hatuna uhusiano wowote mr yoo yeon seok
ilikuwa ni 17/10./2017.ndipo uliniomba nikuweke link ya historical movie inayoitwa the fortress.
bahati nzuri leo nimetembelea tovuti ya dramanice ndio nimeona wameshaiweka subtitle ya kiingereza.
kwa ufupi
mnamo mwaka 1636, Qing dynasty ambayo ndio china ya kipindi hiki kama sijakosea waliivamia nchi ya joseon ambayo kwa sasa ni korea japokuwa imegawanyika nchi mbili. mfalme Injo na watumishi wake waliikimbia ikulu na kwenda kujificha kwenye ngome iliopatikana maeneo ya milimani inayoitwa Namhansanseong.
mtumishi mmoja aliyekuwa anaitwa Choi Myung-Kil aliamini njia pekee ya kurudisha hali kama ilivyokuwa mwanzoni ni kuingia makubaliano na QING, kwa tafsiri ya haraka haraka ni kwamba joseon pia wakubali matakwa ya utawala wa Qing.
Pia kulikuwa na mtumishi mwengine aliyeitwa Kim Sang-Hun ambaye aliamini njia pekee ya kurudisha heshima ya serikali ya joseon ni kuendelea kupambana hadi mwisho wa nguvu zao.
je mfalme atachukua maamuzi ya nani?
starringAwards
lee byung hun = choi myung kil
kim yun seok = kim sang hun
park hae il = mfalme Injo
nakuomba radhi kutoka ndani ya kiwililiwili changu kilicho hai muda huu, hivyo basi usije ukadhani nilikupotezea kwa kipindi cha miezi 10.
- 2018 (54th) BaekSang Arts Awards - May 3, 2018 ,"Best Film"
- 2017 (38th) Blue Dragon Film Awards - November 25, 2017 ,"Best Screenplay" (Hwang Dong-Hyuk)
aigoooo lakini mimi sijaiangalia mpaka muda huu.
upande mmoja wa sarafu unaweza kumchukulia Dong mae kama ni mwanadamu asiye na chembe ya huruma anapokuwa kwenye mawindo yake ila mwisho wa siku utagundua ya kwamba kumbe hata yeye ameumbwa na hisia tofauti na robot Namshin na ndio maana anapokutana na mwanadamu anayemfanya hisia zake za kikatili zitulie anakuwa mnyonge sana.Nguvu Ya BinAdamu Wa Jinsia Ya Kike, Hiyo Ndo Nguvu Yao Kwenu Hata Uweje Ukifika Kwa Mtoto Wakike Unakuwa Kama Mkate Tuuh.
Mi Alinikera Pale Alipomvuta Yule Binti Mdogo, Then Akakubari Kupigwa Kibao Na Binti Mkubwa. Huyu Jina La Bwee Linamfaa
Hahahahah Pole.upande mmoja wa sarafu unaweza kumchukulia Dong mae kama ni mwanadamu asiye na chembe ya huruma anapokuwa kwenye mawindo yake ila mwisho wa siku utagundua ya kwamba kumbe hata yeye ameumbwa na hisia tofauti na robot Namshin na ndio maana anapokutana na mwanadamu anayemfanya hisia zake za kikatili zitulie anakuwa mnyonge sana.
mfano wa pili muangalie anapokutana na manadada Hina ambaye ni mmiliki wa hotel anakuwa mkimya sana, hii inaonyesha kwa kiasi kikubwa sana ameathirika na maisha aliyoyapitia udogoni kwake.
dongmae hakuzaliwa kuwa shetani ila maisha mabovu aliyoyapitia pamoja na wazazi wake yamemfanya ajione kuwa ni shetani aliyetakasika ambaye ana uhuru wa kutoa adhabu yoyote na kwa mtu yoyote na kwa muda wowote.
aigooooo maandishi ulioanza nayo sijayapatia majibu.
anakusalimia jang hyuk sunbaenimATa mi nampenda,sijui kwa nn li bang ji wasifu wake humu sijaupenda
Sorry mkuu wewe ni mkorea?nami niwatakie kheri ya kutimiza miaka 5 kwenye ndoa yao
lee byung hun na lee min jung
Kufatilia ongoing mateso sana. Halafu sijui kwann sijaipenda hii movie kama nilivyozipenda wok of love na whats wrong with secretary kim
Sorry mkuu wewe ni mkorea?
Hiyo series ni hatari niliangalia Iljimae na return of Iljimae yaani huwezi kuchoka kuziangaliaIljimae
Hi series ni nzuri kwangu. Huwa si ichoki kuingalia.
Yanajitosheleza ila naona unafahamu mengi kuhusu Korea. Labda uongezee tena nyama kidogo...
- hapana nimezaliwa Tanzania.
- wazazi wangu wote ni watanzania kutoka Zanzibar japokuwa kihistoria wametokea sehemu tofauti za East African
- sijawahi kufika nchini korea na pia sijui kuzungumza lugha ya korea.
- wala sijawahi kulala nikaota nimepanda mnara wa Namsan Tower.
- pia sijawahi kulala nikaota ninakula jjajangmyeon na chupa ya soju.
- uhuru wa kufanya ninachokitaka nikiwa Tanzania pasina kuvunja sheria ndiko kulikonipelekea kuwa ni mfuatiliaji wa korean entertainment.(korean hallyu). wale watu weupe wanaita demokrasia.
- je majibu yangu yangu yamejitosheleza?
Na Dong Mae Akamjibu kuwa, Uo Ukubwa Wa Iyo Ardhi Ndipo Atakapoenda Kumzika Sababu Hatapata Shida ya Kutafuta Pakuzikia.amemwambia dongmae unashangaa mimi kulipia tiketi zote za treni?
- dah! nimeshangaa sana kuona kumbe mfalme ndiye kiongozi mkuu wa kikundi cha righteous army.
- naona kim hee sung naye ameshaanza kunasa kwenye sumaku ya mwanadada go aesin, hapo anamwambia kama umeamua maisha yako kuwa mpigania haki wa joseon basi nipo tayari kuwa kivuli chako.
- kuna nukuu moja ameizungumza kim hee sung imenichekesha sana kwenye icho kipande hahahahahahahaaaaa
inawezekana mfalme wa joseon ndiye mmiliki wa milima na wanachi wote lakini familia yangu ndiyo wamiliki wakuu wa ardhi ya joseon