Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!


Naanza Kuangalia Hii Drama, Japo Nimekuwa Na Tabia Yakutozimalizia Medical Drama Mpka Mwisho Nilofanikiwaga Kuimaliza ni Doctors Ya Kim Rae Won na Park Shin Hye. Natamni Na Hii Nifike Nayo Mbali kama Siyo Mwisho
doctor stranger ndiyo drama pekee yenye maudhui ya medical ndio niliimaliza episode zote.
unajua ni kwa sababu gani?
kang sora
 

Wamecheza Kiserious Sana Umu Ndani Jamni Uwaoni Kucheka Cheka.

Kuna Sehemu Kuna Mtu Alicomment kuwa Yeyote Aliejitolea Kusub Hii Drama Ashapoteza Uhai Maana Si Ugumu Wake.

Yaani Ata Kauli ama Maneno Yanyotumika Umu Ndani Ni Magumu Gumu Na Ukweli Kuwa Ni Tofauti na Drma Nyingi za Medical!
 
hahahahahaaaaaaaa umenifanya nicheke kama jinga jinga
baadhi ya wakati nalazimika kunotes terminologies ndipo nikamuulize MR google maana yake.
subtitle yake nayo kama hujapita shule zetu za speaks english please utapata tabu sana na unaweza kuichukia hii drama. inanilazimu baadhi ya wakati nami nisome comment za wachangiaji ndipo niiifahamu zaidi stori yake.
nahisi anayetafsiri hii drama ni mwanasheria.
 

Ila Nimependa Uhusika Wa Huyu BinAdamu Ananifanya Hata Nisimchukie Yaani! Uhusika Kauvaa Hasa.
 
Hapana Siijuhi Sababu Nidokezee.
jawabu nimeliweka hapo juu.
kuna project moja nilikuwa naiangalia inaitwa MISAENG (incomplete life) ni nzuri sana sana ila nimeiacha kwa muda vyuma vimeanza kukaza.
humu ndani yumo im siwan, kang sora, kang ha neul, byun yo han n.k
ndio best drama kwa mwaka 2014.
some time inafika wakati najiuliza maswali mbona hii drama kama iannihusu na mimi na wengineo niliyoyapitia na ninayoyapitia kwenye maisha yangu ya kila siku.
ndio nikaikumbuka hii nukuu
maisha yote njia hufunguka pale ambapo utakapoamua kutembea, njia isiyofunguka haiwezi kuwa ni njia.
njia inaweza kuvunguka kwa mtu yeyote yule lakini si kila mtu anaweza kuwa na njia.


hii mitandao wanatufanya sisi watumiaji kama ni matajiri sana wanaamua bila ya sababu kupunguza bundle lakini thamani haishuki.
nimeshazoea free internet kupitia wireless basi kipindi hiki nasumbuka mnoooo.
na kwa hali niliyofikia siwezi tena kuangalia drama zilizotafsiriwa kwa kiswahili.
kwa hali ilivyo acha niendelee kuifuatilia MR SUNSHINE kila week end na hizi nyengine nazihifadhi kwenye mtungi.
 
Dah!
 
Your Honor
hii nayo pia nilikuwa naifuatilia kila wiki lakini itanisamehe kwa muda mchache sana mpaka nitakaporudi katika hali ya kawaida.
nimefika episode 4 kwa 8
achana na drama zifuatazo ambazo zimeeleza uhusika wa watu wawili wanaofanana
im not a robot
are you human too

humu ndani muna ndugu wawili wenye mfumo tofauti wa maisha wanayoishi kila siku.
mmoja ni jaji ambaye ni han soo ho na mmoja ni mkorofi sana kwenye maisha yake na hakupenda kusoma na jina lake ni han kang ho.
balaa kuna siku huyu hakimu alitoa maamuzi ambayo familia moja hawakufurahishwa nayo sasa wakaamua kumteka na siku hiyo hiyo mdogo wake naye akafanya tukio la kihalifu.
daebak

kang ho akaona njia pekee ya kujinasua ni kukimbilia kwa kaka yake ambaye ni jaji ili amsaidie sasa kufika ndani kaka yake hayupo.
mhhhhh akaona ngoja nijifanye mimi ndio jaji japokuwa sina sheria hata moja ninayoijua.
unadhani kaka yake atarudishaje nafasi yake ya ujaji pale mahakamani na wakati jamaa ameshaanza kupendwa na wanachi kwa sababu hukumu anazotoa haangalii heshima ya mtu kwenye jamii?

kuna nukuu yake moja ameizungumza nimeipenda sana

sheria ndio kipimo pekee kinachoweza kuigawanya dunia kimatabaka, kama utakuwa unaiogopa sheria basi maisha yako yote utakuwa chini ya sheria ila kama utaichukulia sheria ni kama utani basi utakuwa juu ya sheria
 
Familiar Wife
ni moja kati ya drama ambayo unapoiangalia hupaswi kuongozwa na hisia za kijinsia, ni vigumu sana lakini unapaswa hisia zako uzizuie japo kwa saa moja utakalolitumia ukiwa kwenye TV yako.
Nimebahatika kuziangalia episode mbili za mwanzo hivyo basi huko mbele sijui kimetokezea kitu gani.
pia ni mwendo wa time travel baadhi ya wakati humu ndani usije ukabaki njia panda.
  1. kwa sababu kama ni mwanamme basi utamchukia mwanamke wa humu ndani na kumdharau pamoja na wanawake wengine.
  2. kama ni mwanamke pia vile vile utamtetea mwanamke mwenzako na utawaona wanaume wote wanatabia zinazofanana kama anazozionyesha ji sung kwenye hii drama.
  3. nilichojifunza ni kwamba changamoto kuu za wanandoa zinaanza pale wanapobarikiwa kupata mtoto mmoja au zaidi.
  4. na pia furaha kuu ya wanandoa huzidi zaidi pale wanandoa wanapofanikiwa kupata mtoto mmoja au zaidi.
  5. kazi kwenu wanandoa na wale wanaojiandaa kuingia kwenye pambano la ndoa.Nitakapofika miaka 80 ya kuzaliwa ndio nitaanza kufikiria kuingia kwenye ndoa.
 
Mkuu nashukuru sana kwa kusoma mabandiko yangu,Nadhani umenipita kila kitu.
Mimi ni orabanyi (?)mkuu..
Nimependa tone ya uandishi wako
 
Mkuu nashukuru sana kwa kusoma mabandiko yangu,Nadhani umenipita kila kitu.
Mimi ni orabanyi (?)mkuu..
Nimependa tone ya uandishi wako
hahahahahaaaaaa naomba comment yako uifanyie mabadiliko haraka kabla wenye jinsia yao hawajaamka.
orabeoni wanatumia wanawake to indicate brother.
wanaume wanatumia hyungnim to indicate brother.

umenikumbusha episode moja ya return of superman ambapo ilitokezea song il kook alimuuliza mtoto wake wa mwisho kati ya wale mapacha watatu umri wake wa kuzaliwa.
jina lake anaitwa song manse na alipoulizwa akajibu umri wake ni manse
manse = hurray, long live, idumu miaka 10000.
song il kook alicheka kama mwehu
lakini ndio kujifunza kama nilivyokwambia binadamu tunategemeana.
 
Hahaaaaaaaaaaaaaaà umeniingiza mtego bro Mimi ni Hyungnim Lee Kang to ndio alivyokua anamwita kaka yake (blidal mask)
 
Happy National Liberation Day of Korea
kila inapofika tarehe 15 August nchini korea wanasherehekea siku yao ya kupata uhuru kutoka kwa wakoloni wa kijapani.
hii ni sherehe ambayo husherehekewa na wakorea wote pasina kuangalia itikadi zao na sera zao za kiutawala( south na north korea)

  1. korea kusini sherehe hizi wamezipa jina la Gwangbokjeol wakimaanisha siku ambayo muangaza wenye nuru umerudi kwa wakorea.
  2. korea kaskazini sherehe hizi wamezipa jina la Chogukhaebangŭi nal wakimaanisha siku ambayo uhuru umerudi kwenye ardhi ya mababa zetu.
ilikuwa ni 15/08/1945 ndipo bendera ya japan iliondolewa nchini korea na kupandishwa bendera ya korea kwa msaada mkubwa wa Marekani na Urusi.
kosa kubwa walilolifanya wakorea ni kuwa walishindwa kuchagua sera halisi za kuongoza taifa lao hivyo basi kila upande uliamua kufuata itikadi wanazoziamini.
unadhani nini kinatokezea kama upande mmoja unafuata sera za kijamaa kutoka kwa urusi na upande mmoja wa wapigania uhuru wanafuata sera za kibepari kutoka kwa marekani.?
ndipo mwaka 1948 pande hizi mbili zikaamua kugawana madaraka.
  1. pro U-S dictator syngman rhee akachaguliwa kuwa rais wa korea kusini.
  2. pro soviet dictator kim IL sung akachaguliwa kuwa rais wa korea kaskazini.
wote nimewaita madikteta kwa sababu pande zao walishindwa kuziunganisha na kuzifanya nchi moja na hatimaye kusababisha vita iliopoteza zaidi ya watu millioni 5. miaka miwili baadae.
  1. mwanadada kim so hyun ameandika maneno yafuatayo kwenye account ya instagram : sitoisahau siku hii.
  2. mwanadada chae soo bin ameandika maneno yafuatayo: leo tunasherehekea miaka 73 ya uhuru lakini sitosahau sadaka zilizotolewa na watu wenye tabia za kishetani.
  3. song il kook naye ameandika maneno yafuatayo : nipo mbele ya ukuta wa berlin muda huu, nimekutana na marafiki ambao wamenipa zawadi, nasisi leo tunasherehekea uhuru na natumai siku moja tutakuwa nchi moja.
Jamhuri ya watu wa korea iendelee kudumu kwa amani na mshikamano.
 
Inawezekana Mr. Sunshine Inaelezea Hii Ya Kutawaliwa Na Wajapan Kisha Urusi Na Marekani Wakaja Kuwakomboa, Maana Naona Ndo stori Inayozungumzia Sana Mule.
 


Kuna Vitu Vingi Sana Vinayoendelea Nyuma Ya Haya Majengo Marefu kwa Maana Ya Ghorofa au Hya Mafupi Kwa Maana Ya Majengo Ya kawaida Yaloandikwa Hospital.

Hii ni Biashara Kama Biashara Zengine Zianazotoa Huduma Kwa BinAdam, Tofauti Na Hii Ni Kuwa Inamuhudumia BinAdam Mwenye Maradhi, Kama Tunavyojua Maradhi Yaja Bila Hodi, Yanaweza Kukukuta Huna Hata Thumni Mfukoni Hasa Sie Wengi Wenye Hali za Kipato Cha Chini.

Hakuna Asiyehitaji Huduma Ya Haraka Na Bora Hasa Kwenye Ugonjwa, Wafanya Biashara Au Wamiliki Wa Hizi Hospital Walilijua Hili Ndomana Wakaamua Kuweka Izi Huduma Kwnye Majengo yao ya Hospital,Si kwa Bure Bali ni kwa Gharama kama Msemo Usemao ''UZURI NI GHARAMA'', Izi Huduma Zinaenda Kwa Pesa Lipa Upate! Hakuna Sina Au Nikope Kesho Mwisho wa Mwenz Ntakulipa Hili Mfanya Bishara/Mmiliki Wa Hospitalini Alijuhi Hili,Huduma Utaipata Baada Ya Kulipa Hata Uwe Maututi Unayetaka Kuikaribia Kuzimu Ahutapata Hiyo Huduma Unayostahiki Paka Ulipe, Hizo Ndo Hospital Zetu Ziwe Za Serikali Hata Za Binafsi Na Hii Tunaiona Kila Leo Tuwapo Mahosapitalini.

Hii Drama ''LIFE'' Inaelezea Tusoyajua Kwenye Uendeshaji Wa Izi Hospital Yanayoendelea nyuma Kati Ya Wamiliki na Madaktari/Nurse na Kati Ya Madaktari/Nurse na Wagonjwa, Sisi Wagonjwa Tunawaona Madaktari Hawataki kutupa Huduma Iliyo Nzuri,Ndugu wanawalalamikia Madaktari Kwa Makosa Wayatendao Mpaka Kusababisha Vifo Vya Ndugu Zao Bila Kujua Kiini Cha haya Yote, Kumbe Kuna Yale Yanayoendelea Baada ya Mmiliki Kmwambia Daktari Kuwa Unafanya Kazi Kwa Kuingiza Faida,Chochote Mtakachofanya Lazima Faida Muiingize, Na Hapa Si Wote Watakaoweza Kukidhi Gharama Za Hospitalini, Daktari Haruhusiwa Kukuhudumia Mpaka Ukidhi Izo Gharama Hiii Ni Amri Kutoka Kwa Mmiliki, We Mgonjwa Hutomjua Mmiliki Utamjua Daktari, na Usipotoa Hizo Pesa Mmiliki Hata Kujua Wewe Mgonjwa Atamjua Daktari Aloshindwa Kumfanyia Kazi Yake Vizuri, Na Daktari Hatokubali Aonekane Hafanyi Kazi Atarudi kwako Na Kukuambia Hupati Huduma Mpaka Ulete Pesa, Mimi Wewe Raia Wa Kawaida Ndo Tutakao Umia.na Tunaumia, Kwani Sasa Ghrama Za Hospital Ziko Juu Sana.

Hii Drama Inayafichua Hayo, Hii Drama Inayaelezea Hayo, BATTLE Kwenye Majengo Yalonamjina Ya HOSPITAL, uhalisia Wa Hii BIASHARA Ya ROHO Za BINADAM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…