하하하하 하하하하
ahsante sana brother kwa heshima ulionipa inanipasa nizipokee kwa moyo mkunjufu pasina kinyongo..
unajua binadamu hawezi kuwa mkalifu kwa kila jambo ndio maana pakawepo na chain kwa dhumuni kuu la kusaidiana ili kuyakabili maisha kwa urahisi zaidi.
msingi mkuu wa kuyafurahia maisha ni kupenda kila ambacho kinaleta mwangaza kwenye nafsi yako na kwangu mimi kwa miaka hii 5 ukiachana na football kitu pekee kinachonivutia ni kufuatilia korean wave entertainment.
na sababu kubwa hii ndio starehe pekee isiyoniletea athari kwenye kiwiliwili changu.
nitakapovutiwa na kitu chengine cha kuondoa stress zaidi ya korean drama basi nitaachana na series za Asia.
upande wa pili hata wewe upo vizuri baadhi ya maeneo ambayo mimi sina uelewa nayo mkubwa na inafika wakati najiuliza maswali kama wewe
je ninaweza kuwa mfuatiliaji mzuri wa masuala ya dunia, imani, historia kama Da'Vinci ?
unaweza ukawa na dhana ya kwamba nakudharau au kukukejeli lakini ndio ukweli, ninayoyaeleza yana ukweli kutoka ndani ya kiwiliwili changu kilichohai muda huu na kimaarifa.
japokuwa inavyoonekana tuna tofautiana kiimani lakini hainizuiii mimi kusoma maandiko yako yenye maudhui ya dini unayoiamini unayoyaweka kwenye jukwaa la intelijensia na kiukweli nimekuwa nikijifunza mambo mengi sana kupitia kwako.
pia kupitia andiko lako linalomuhusu leonardo davinchi nimejifunza mambo mengi sana yanayomuhusu genius wa kitaliano aliyeishi karne nyingi zilizopita lakini uwezo wake wa kufukiri ulikuwa ni kama mwanadamu wa karne hii ya ARTIFICIAL INTELLIGENCE
maisha yote anayechagua sehemu ya kujifunza hawezi kuwa msomi mahiri katika ulimwenguu huu wa sasa.
nami pia nikushukuru hyung nim /dong saeng / ahjussi / harabuji kwa uwepo wako hapa JF.