Mkuu una kichwa cha kushika na kupenda historia?
Hahahahahahahaha.
Kwanza anza kwa kuingia google type the GoJoseon, anzia hapo utapata links nyingi sana.
Historia ya Korea imeanzia hapo haswa kuna mtu anaitwa DANGUN ndiye anayechukuliwa kama baba wa Korea. Ila inasemekana sio binadamu. Hizo sasa ndo myths na folklores zilizonifanya nikatafute ivyo vitabu vya SAMGUK SAGI SAMGUK YUSA na vinginevyo. Can you beleve according to the books JUMONG, KING GEUMWA, HAE MOSU, na maprince wengi wa GAYA confederacy pia PARK HYEOKGEOSE mwanzilishi wa Silla na KIM ALJI mwanzilishi wa ukoo maarufu wa KIM, hao wote wanasemekana kuzaliwa kwa kutotolewa toka kwenye mayai according to the books.
Then kila unapoangalia drama ya Kikorea jipe homework ya kuja kutafuta about events ama watu waliohusika humo.
Kwa mfano ukiangalia GENERAL GYE BAEK au Ukiangalia the GREAT KINGS DREAM ukimaliza nenda search kuhusu Gye Baek, Na Kim Yusin (greatest general in Korean History) pia search kuhusu the Battle at Hwangsanbeol ambapo ndio Baekje ilipoanguka baada ya Gye Baek Kupigwa na kuuwawa dhidi ya Kim Yushin.
To cut the long story short;
Gojoseon->Pre-three kingdoms era (Buyeo kwa kina Gimwa na Taeso/Daeso, Young Goguryeo, Okjeo, Samhan)->Three kingdoms Era (Baekje, Silla,Goguryeo, Gaya confederacy baadae ikawadiffused/submitted into Silla)->Unified Silla(pumbavu zao Silla waliungana na Wachina wa Tang wakaangusha Gogurye na Baekje) and Balhae->Later three kingdoms;Silla(iliyoanza kuanguka na kumeguka), Later Baekje (Hubaekje), Later Goguryeo (Hugoguryeo) NB; Hubaekje na Hugoguryeo zilijimega toka kwa Unified Silla->Goryeo/Koryo->Joseon->Korean Empire->Chini ya Japanese rule na Provisional government->Baada ya Japan na wenzao kina Germany na Italy kupigwa na kushindwa vita ya pili ya dunia ndipo marekani na Urusi wakagawana Urusi akakaa North na Marekani akakaa south(ilipotokea civil war ndo mgawanyiko ukawa rasmi mpaka sasa North na South Korea from 1948.
Kwaiyo Silla Kwa leo wangekuwa mostly South Korea kabla ya kuziangusha Baekje na Goguryeo ila baada ya kuziangusha angekuwa kote, Baekje wangekuwa kotekote,wakati Goguryeo angekuwa China, Korea Zote, Urusi hata Mongolia. Koryo na Joseon wao pia wangekuwa kote.
Mkuu Kazi kwako.
Call Me Kim Mo Jo San from Ansiseong fort under Yang Manchun.