Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Haha sasa hapo tusijeanza kuchukiana mtu na dada yake watu wote mle hujawaona ila shemeji yako? Mimi nilipenda kwa kweli labda kwa kuwa sikuwa nimewahi kumuona Hye Kyo before kwa hiyo akanivutia kweli.
Sasa hivi sina kitendea kazi siku nitakayopata nitakujia unigawie lol naomba unipokee tu
 
Naisubili Hii.

Now Nimeianza My Mister Baada Ya My Prince Kuisha.
daebak kwangu mimi ukiondoa MR SUNSHINE drama kwa mwaka huu drama yangu ya pili kwa ubora ni MY MISTER (my ahjussi).
ila sijui kama na mimi nitakuja kuwa na moyo wa kusamehe kama alivyofanya ahjussi wetu mule ndani baada ya kugundua mke wake anatembea na bosi wake ambaye pia ni rafiki wa karibu.
ni maamuzi ya kishujaa aliyoyachukua ahjussi park dong
unamuonaje mwanadada IU?
 
hivi huko kwenu fairy wanapatikana?
kama wapo namuhitaji lakini awe mrembo kama Moon Chae Won
kwa hali hii ninayokwenda nayo sijui kama nitaweza kuachana na huu ulimwengu wa korean drama.
takribani wiki mbili zilizopita nilitest mitambo ya kuacha kuangalia korean drama lakini cha ajabu mitambo ilikuwa ya kichina.
kwa wale wapenzi wa going on drama ingizo jipya la wiki hii.
Mama Fairy and the Woodcutter at Dramanice

 

Attachments

  • 1541688090011.png
    247 KB · Views: 44
I see TvN hawajawahi niangusha
 
Gu Am Heo Joon drama
laiti kama wanadamu tungelikuwa na utamaduni wa kupenda kusaidiana tungelikuwa tunaishi kwenye ulimwengu wenye furaha na amani kwa kila mwananchi.
nimebaki najiuliza kwenye huu uliwengu tunaoishi wanafika angalau madaktari 10000 wenye tabia kama alizokuwa nazo dokta heo jun?
naamini jamaa aliletwa duniani kwa ajili ya kuwasaidia wale wenzangu na mimi tusiojiweza kwenye huduma za afya.
  • ni daktari ambaye aliwachukulia wagonjwa wote kama familia yake
  • ni daktaria ambaye hakuthubutu kuangalia heshima ya mgonjwa kwenye jamii, awe tajiri, masikini au fukara kwake yeye wote walikuwa ni sawa.
aigooo hii drama imevunja rekodi ya kunitoa machozi ovyo, naamini kama ningelikaa na ndoo ya maji basi ningeliijaza machozi yangu.
kilichoniumiza zaidi ni kwamba hii ni mara ya pili ukiachana na god of war drama umeigiza unafariki.
kwa nini ahjussi ulikuwa unajitabiria kifo bila ya kujijua?
hatimae umeondoka kweli kwenye ulimwengu huu bila ya kumuaga hata mchumba wako ambaye ulikuwa tayari una mipango naye ya kufunga ndoa.

Profile
  • Name: Kim Ju-Hyeok
  • Hangul: 김주혁
  • Birthdate: October 3, 1972
  • Date of Death: October 30, 2017
endelea kupumzika kwa amani huko uliko gu tae hyungnim
 
I see TvN hawajawahi niangusha
public broadcasting kama KBS, SBS na MBC wanapata tabu sana miaka hii.
mwaka huu nusu na robo ya waigizaji maarufu wamefanya kazi na kituo cha TvN au Jtbc.
cable tv zimejipanga sana.
 
aminas muda wa kuanza kufanya maandalizi ya kuweka mbavu na kinywa sawa kwa ajili ya kucheka umewadia.

Kim Seon Ho In Talks To Play Leading Role In 2nd Season Of “Waikiki”
 
bogoshipda
unapoiponda descendent of the sun ni sawa sawa na kumponda huyu mama kim eun sook.
kiupande wangu nilimpenda zaidi song hye kyo kuliko song joong ki.

  • mr sunshine
  • goblin
  • descendent of the sun
  • secret garden
  • the heirs
  • gentleman dignity
zote hizi ameandika yeye
 
public broadcasting kama KBS, SBS na MBC wanapata tabu sana miaka hii.
mwaka huu nusu na robo ya waigizaji maarufu wamefanya kazi na kituo cha TvN au Jtbc.
cable tv zimejipanga sana.
Ila KBS walisumbua hadi 2015 hv
MBC nao hadi sasa wanajitahidi
Ila SBS sasa hivi sijabahatika kupata hata ongoing yake
 
Ilikuwa ajali?,duu mi mpaka Leo ndio series ambayo nmeshindwa kiofuta kwenye storage Yangu,mingu pumzishe
 
AUDIO | Nash MC Ft. Grace Matata - SAUTI | Download Mp3
 
Nimeimaliza Jana Hii Drama Yaani!!

Nilitaka Nije Andika Malalamiko Umu Kwa Kuchelewa Kunipa Hii Almasi, Ila Nikasema Ngoja Niimalize Hili Nikamlaumu Vizuri.

Nilikuwa Nalia Pamoja Na IU Nilikuwa Nalia Pamoja Na Doong Hoon! Kila Scene Ambayo IU Alikuwa Analia Nami Nimelia Kila Scene Doong Hoon Alotoa Chozi Nami Nimetoa Chozi (Huu Ni Uchizi Najua, Ila Kama Uelewi Hisia Za Mtu Hata Kimaigizo Bado Ujapitia Hayo Maisha Ukaelewa Mtu Anamaanisha Nini Kwenye Hayo Maigizo)

Kuna Watu Wanapitia Haya Yaloigizwa Umu Ndani Kuna Watu Wanaishi Hivyi Ndani Ya Nyumba Zao, Kuna Wanaume Kama Dong Hoon Ndani Ya Nyumba Zetuu! Wanalia Ndani, Bila Kuyatoa Machozi Nje....Na Hawana Wakuwaambia Sababu Ni Aibu! Aibu Ilo Na Maumivu Makali Sana Daah!!

Malezi Alopitia IU Kuna Watu Sasa Ivi Wanapitia Malezi Haya, Kujutia Kuwa Duniani Kuomba Kuondoka Duniani Haraka Hili Kosa Kubwa Ulilowahi Lifanya Lisijulikane na Watu Wengi Zadi,Kuona Ulimwengu na Watu Wake Kama Wamekutenga Auko Kama Wao! Haya Maisha Yanaumiza Sana Sana..

Hii Drama Imenigusa,Imenigusaa!

Kudo Kwa IU Umu Ndani Kakua Sana, Kudo Kwa Doong Hoon Ahjussi Nilotamani Damushin Awe Hivi Na Subira Ile InshaAllah Mola Ataizidisha.

Lawama Zako Zinakuja.
 
aminas muda wa kuanza kufanya maandalizi ya kuweka mbavu na kinywa sawa kwa ajili ya kucheka umewadia.

Kim Seon Ho In Talks To Play Leading Role In 2nd Season Of “Waikiki”
View attachment 926643
Sasa Huyu Si ndo Nitkuwa Hospital Kila Nikiangalia Maana Mbavu Zitabidi Zirudishwe Kila Episode Moja Ikiisha..

Wameamua Kutoongezea Chizi Mwengine Dooh! Apa Nijiandae Hasa.
 
Daebak daebak kalamu yangu imeishiwa wino na fedha ya kununulia mpya imekuwa ni ngumu kuipata kama maisha ya IU hivyo basi sina cha kuongeza.
Lakini na wewe baadhi ya nyakati unakuwa mbishi kama mkuu wa mkoa wa konki konki konki.
unaikumbuka because this is my first life drama ilivyokuwa tunaisifia pamoja na EMPTY dongsaeng cha ajabu mwenzetu ukatia pamba masikioni na kuamua kuipotezea.
siku uliamua kuotafuta kwa jinsi ilivyokuwa nzuri ukaiangalia kwa siku mbili.
kwi kwi kwi kwi.

 
Sasa Huyu Si ndo Nitkuwa Hospital Kila Nikiangalia Maana Mbavu Zitabidi Zirudishwe Kila Episode Moja Ikiisha..

Wameamua Kutoongezea Chizi Mwengine Dooh! Apa Nijiandae Hasa.
ndio nishaanza mazoezi ya kuweka mbavu zangu sawa naona mwaka mpya utaanza tena na balaa.
ningependa chawbacca arudishwe tena kwenye season 2 ili akutane na jamaa yake wa kwenye strongest deliveryman.
muharmusi style
lets gooooooo
 
Aigoooo Ubishi Nao Uko kwa Damuu.! Ila Hii Ukuniambia Chinguya Kweli Tena...

Hii Ilikuwa Siku Mbili,My Ahjussi Nimeangalia Siku Nne Imeeisha..Omo Omo Omo Umenikumbusha Mbali Sana Hii Drama
 
Huyu Atakuepo Tuu! Ndomna Wanamueka Chizi Yule,Mi Napenda Sauti Yake, (100 Days My Prince)
 
Aigoooo Ubishi Nao Uko kwa Damuu.! Ila Hii Ukuniambia Chinguya Kweli Tena...

Hii Ilikuwa Siku Mbili,My Ahjussi Nimeangalia Siku Nne Imeeisha..Omo Omo Omo Umenikumbusha Mbali Sana Hii Drama

kwa hizi going on drama unaangalia zipi?
usiniambie the beauty inside drama huaingalii nitachukia sana kwa sababu naogopa utakuja kunitupia mzigo wa lawama.
hao waigizaji wenu uchwara wakiume wanaotamba kwenye rom comedy drama waambiane wajiandae kisaikolojia kumpa heshima huyu brother wangu lee min ki, hizi project zake mbili amezitendea haki sana na inaonekana jamaa ana bahati ya kuchagua project nzuri kama lee jong suk.
na bila ya kusahau waigizaji wenu wa kike wanaopewa promo sana na media watapata tabu sana kwa huyu bidada Seo Hyun Jin a.k.a mke wangu wa ndotoni.
halafu humu ndani yumo lee da hee ni mrembo na fashion zake ndio shidaaa, nitachukia sana kama lee da hee na Ryu Eun-Ho uhusiano wao ukashindwa kunawiri.

hadithi ya hii drama ni kwamba Han Se-Gye ana tatizo la kubadilika maumbile yake kila inapofika mwisho wa mwezi na seo do jae ana tatizo la kutokutambua sura.
nathubutu kusema hii ndio best romantic comedy kwa kipindi hiki.
NB:
kwa wadau wa korean drama tusije tukachanganya madawa kama movies za bwana yule na mjomba wake.
kuna lee da hee na lee da hae

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…