Kheri ya mwezi mpya wa
December chingus, Mungu atujaalie uwe ni mwezi uliojaa baraka na neema zinazozidi uzito wa vijisenti trillioni 1.5 kwa kila mdau humu ndani.
kwa nini December kiupande wangu?
- ndio mwezi wa mwisho wa mwaka huu 2018.
- waumini wa imani ya ukristo duniani husherehekea kuzaliwa kwa mtakatifu wao aliyetakasika kuliko kiumbe yeyote aliyezaliwa na mwanamke.
- huyu lofa aliyeandika ujumbe huu atatimiza mwaka wa 3 tokea awe mwanachama wa JF ifikapo 15/12/2018 endapo atakuwa na uhai.
- na kama mambo yataendelea kuwa mazuri basi inshaalllah kama ilivyokuwa mwaka jana tutapeana updates za tunzo zitakazo fanyika mwishoni mwa mwezi huu kupitia mashirika ya KBS, SBS na MBC drama awards .Hili litawezekana kama mtandao wa soompi watakuwa live.
natumai bado tunakumbuka kilichotokezea mwaka 2017.
- SBS drama awards: muigizaji bora wa mwaka alikuwa ni JI SUNG kupitia drama ya INNOCENT DEFENDENT.
- MBC drama awards: muigizaji bora alikuwa ni mzee Kim Sang Joong kupitia drama ya the rebel thief who stole the people.
- KBS drama awards:washindi walikuwa ni mzee cheon ho jin kupitia family drama inayoitwa my golden life na mzee kim young chul kupitia family drama inayoitwa father is strange.
nimalizie kwa kumtakia kheri ya kuzaliwa
Khantwe, nilitaka niwe mtu wa mwisho kumtumia ujumbe utakaomjaza furaha lakini cha ajabu kila ninapotembelea jukwaa la chit chat nakuta bado watu wanaendelea kumtumia jumbe za pongezi huyu ahjumma mtarajiwa.
nimebaki najiuliza maswali yasio na majibu kama uchumi wa Afrika.
hivi huyu mwanamke ni mtakatifu sana anayemkaribia bikira maria aliyemzaa yesu kristo?
hivi huyu mwanamke utakatifu wake anamkaribia khadija yule mke wa mtume wa waislamu?
sidhani kama anawafikia hao japo kwa 40% bali silaha yake kubwa ni kuishi na watu wote humu ndani kwa upendo na hekima zinazoendana na lugha inayopendeza kutumika kwa rika lolote lile.
kumbe mwanzoni nilikuwa nafanya makosa nilipokuwa naogopa kunukuu hata comment yake pindi alipokuwa anatoa mchango wake humu ndani kwa kudhani ni goi goi.
naomba unisamehe noona kwa ujinga wangu.
naamini kupitia thread hii nitatimiza ndoto yangu ya kuwa wa mwisho kumtakia kheri ya kuzaliwa.
sitaki stori za wakorea siku ya leo kwa sababu bado nina hasira na jose mourinho na watoto wake wazembe.