Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

basi amani ya bwana iwe juu yako usiku huu.
na mimi hii comment asifanikiwe kuiona aminas
jamani tupeane mikono ya amani kuanzia leo mpaka siku tutakayokwenda uarabuni kulima mitende.
 
Amen...uarabuni tena sio South Korea kula kimchi?

Sent using Jamii Forums mobile app
niliyemkusudia atakuja siku chache zijazo, anaonekana hana furaha kwa sasa kama yalivyo mahusiano ya park bo gum na song hye kyo.

south korea usiwe na wasiwasi naandaa mipango ya kuwa balozi wao wa sanaa nchini kwetu.
japokuwa nasikia nina wapinzani wengi sana wanaotamani nafasi ya ubalozi lakini kwa uwepo wa JF watapata tabu sana kama simba anapokutana na mwindaji anayecheza sebene.

simba mnyama ndie kusudio langu.
 
Naomba hii isiwe utani kama ulivyozoea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Damushin Noona anasema Heri ya mwaka mpya.
ahsante sana dada yangu kwa kunikumbuka, kesho ukienda sehemu ya ibada ukishaomba kwa ajili ya shida zako zinazokukabili baadae niombee na mimi.

shida yangu mimi ni moja tu nayo ni hitaji la kuwa na hekima zitakazokuzidi wewe utakayeniombea.

sihitaji uniombee nipate pesa japokuwa ndio tatizo jengine sugu kwa sababu pesa bila ya hekima ni sawa na mlevi bila ya uongo.

naogopa kuandika maneno mengi nikaishia kudanganya kama nipo kwenye foleni kumbe kuna mtu namla kimya kimya.

kwa sauti ya rais wa venezuela ya afrika
 
[emoji23][emoji23][emoji23] nimependa ya pili kutoka mwisho
Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23] nimependa ya pili kutoka mwisho

Sent using Jamii Forums mobile app
😛😛😛😛😛
mulizoweshwa maneno matamu na aliyekuwa mshika funguo wa gereza la Venezuela, sasa huyu mpya aliyechaguliwa miaka 3 iliopita maneno yake ni sumu tosha. Unaweza kutumia sumu ya panya ukafanikiwa kuwa hai kuliko maneno yanayotoka kwenye ulimi wake ambayo yana tafsiri zaidi ya 500.
ni rahisi kuyatafsiri maneno ya bible kuliko maneno ya mshika funguo za gereza kuu la venezuela.

umeshalima ekari ngapi tokea litolewe tangazo kuu na mshika funguo ya kwamba hatogawa chakula kwa mfungwa yoyote asiyelima wakati majira ya mvua yalikuwepo.
 
talnam castle, popote ulipo nunua unachohitaji halafu woo joo atakuja kulipa, watapata tabu sana wapinzani wetu (makjang drama) na kipigo chao ni kizito muda huu kuliko cha mwizi aliyeiba soko la butcher.
wakorea siku ya jana wamejua kunifurahisha yaani nilikuwa naombea rate iongezeke kwa 0.7% lakini cha ajabu imezidi zaidi ya hapo.
siku yangu ya kwanza kuiangalia hii drama kama kawaida yangu nilikuja kuisifia humu ndani lakini watu kimyaaa wanahangaika na makjang plot, PD nim pleaaaaseeeee ongeza episode zifikie angalau 50 ili watu wahame mtaa wakajifiche kwenye ngome zetu.

“SKY Castle” Overtakes “Goblin” To Set Highest Viewership Ratings In Cable Network History

kwa mujibu wa taasisi ya Nielsen Korea episode ya 18 ya drama hiyo imeangaliwa nchi nzima kwa 22.3 %, ikiwa ni ongezeko la 2.4% ukilinganisha na episode ya 17. Goblin ndio drama iliyokuwa ikishikilia rekodi ya kuangaliwa zaidi nchini korea kupitia cable network.
zikiwa zimebakia episode mbili wadau mbali mbali nchini korea wamebaki na swali moja kubwa sana kwenye bongo zao
Je ni rekodi ipi itakayowekwa tena na sky castle?
je itavuka 25%?
  1. sky castle = 22.3%
  2. goblin = 20.5%
  3. Reply 1988 = 18.8%
yule mwanadamu aliyesema dawa ya moto ni moto kama bado yupo naombe nikutanishwe naye kwa ajili ya mazungumzo machache.

Cha Min-Hyuk : munaionaje pyramid mpya niliowaletea, vipi ni nzuri? kuanzia sasa nataka muiangalie hii pyramid kileleni popote pale munapotembea.
nimefurahi sana mulipoivunja pyramid ndogo, nimedhibiti hasira zangu na nikaamua kuileta pyramid kubwa ambayo hamutathubutu kuivunja.
hahahahahahahahaaaaaaaaaaaaaa baba kama huyu dawa yake ni kumlaza nje kila siku.
 
“A Pledge To God” Continues To Achieve High Viewership Ratings
na hii pia naiangalia peke yangu humu ndani?
aigooooooooo
kwa mujibu wa Nielsen Korea episode ya 32 (= 16 episode) imeangaliwa na watu wanaofikia 15.4% wanaoishi nchini korea siku ya jana.

a pledge to god (a promise with god) ni family drama inayozungumzia maisha ya mwanadada Ji-Young ambaye ni mtangazaji wa televisheni na Jae-Wook ambaye anatokea chaebol family. Ji-Young alipokuwa ni mjamzito aligundua ya kwamba mume wake alichepuka na rafiki yake jambo ambalo lilipelekea mahusiano yao kuvunjika.

miaka 6 baada ya kuolewa na mume mwengine yule mtoto aliyezaliwa aligundulikana na tatizo la leukemia, cha kusikitisha zaidi bone marrow za kwake haziendani na za mtoto wake, akatafutwa baba mzazi lakini na yeye zikawa haziendani.
wataalamu wa afya wakashauri ya kwamba njia pekee ya kumuoakoa mtoto wao basi wazae mtoto mwengine kwa ajili ya bone-marrow transplant.
  • itokezee mke wa damushin amzalie tena mtoto aliyekuwa mume wake wa zamani
  • itokezee mume wa zamani wa mke wangu azae tena na mke wangu kwa dhumuni la kumuokoa mtoto wao.

sidhani kama kwenye dunia hii kuna mwanamme mwenye sifa za song min ho.
mke wangu azae tena na aliyekuwa mke wake kwa ajili ya mtoto ambaye si wa kwangu.
ebwana weee kwa wanaume sisi vichwa vibovu kauli yetu kubwa itakuwa
"acha mtoto wenu afe"
bora niishie hapo, hizi drama nyengine zimekaa kimtego mtego kuliko umbile la beyonce yule aliyekuwa na miaka 30.​
  1. https://kissasian.es/Drama/A-Promise-With-God/
  2. A Pledge to God – QuickDrama – Watch Full Episodes Free HD on QuickDrama
 
Park Shin Hye And Hyun Bin Share Thoughts As “Memories Of The Alhambra” Comes To A Close


Hyun Bin :
ambaye ameigiza uhusika wa CEO Yoo Jin Woo amewashukuru watazamaji wote wa project hii ambayo iliangazia zaidi magical game world kwa kuwa pamoja kwa takribani miezi miwili. Nimefanya project nyingi sana lakini hii ndio ilichukua muda mrefu zaidi kwa ajili ya filamu, ni matumaini yangu project hii itakuwa ni kumbukumbu kubwa zaidi kiupande wangu na crew nzima ya memories of alhambra ambao tulikuwa pamoja kwa takribani miezi 7, bado naikumbuka siku tuliokuwa tunaelekea mji wa granada uliopo Spain kwa ajili ya film location.

Park Shin Hye
ameigiza uhusika wa Jung Hee Joo pamoja na uhusika wa game characters anayeitwa Emma, " naye pia amewashukuru watazamaji wote waliokuwa wakiifuatilia drama hii kila ifikapo mwishoni mwa wiki kwa takribani miezi miwili. kiukweli kwa pamoja tumefanya kazi ngumu sana ambayo inakadiria kufikia tamati wiki hii, niwashukuru production staff kwa ushirikiano mkubwa waliotoa kwa kipindi chote cha kazi ", alimalizia kusema

episode ya 16 itaonyeshwa leo usiku ambayo itakuwa ya mwisho.


 
Hii ulinitamanisha sana mpaka nikavunja ka mwiko ka kutoangalia ongoing again,ila sasa dramania wamekata stimu wapo episode 15. Dramanice mizinguo tele. Hye Na daah naombea asiwe kafariki
 
Less than evil na ghost detective sio kitu kimoja kweli?
 
Wewe kama mie,City hunter ndio drama ya kwanza kabisa.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilopofikia nakosa hata maneno jamani, maana familia mchanganyiko Mambo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…