Major Broadcasting Stations Making Changes After Popularity Of Cable Dramas
kama nawaona TBC za korea dawa zimeanza kuwaingia kwenye mishipa ya ufahamu, walibweteka sana na hatimaye wakawapa mwanya cable tv wawageuzie kibao cha ubora wa project.
kwa mujibu wa stori zilizotoka siku tatu zilizopita ni kwamba mashirika ya SBS na MBC wameamua kubadilisha mfumo wao wa uonyeshaji wa drama ili waweze kuendana na kasi ya cable tv drama..
SBS wameamua drama mpya inayoitwa
“The Fiery Priest" ratiba yake iwe ni siku ya ijumaa na jumamosi, hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa kituo cha SBS kuonyesha drama siku ya ijumaa ambapo kwa miaka 6 walikuwa wanaonyesha show
the law of jungle ambayo itahamishiwa siku ya jumapili.uongozi wa SBS unaamini ya kwamba kuonyesha drama siku ya ijumaa na jumamosii ni maamuzi bora kwa sababu project zote mbili zilizofanya vizuri kupitia cable tv zimeonyeshwa siku hiyo (goblin, sky castle).
MBC nao wameamua kurudisha tena ubora wao kwa kutafuta watu wenye vipaji, kwa kuthibitisha hilo wameamua kufanya kazi na director
Ahn Pan Suk ambaye project yake ya
some thing in the rain (pretty noona who buys me food) ilifanya vizuri sana kupitia JTBC mnamo mwaka 2018, MBC pia wameamua kuwapa offer waliokuwa waigizaji wakuu wa something in the rain ambao ni
jung hae in na
son ye jin kushiriki kwenye project mpya lakini bado hawajathibisha ushiriki wao.
pia MBC wameamua kuja na project yenye utofauti wa kimaudhui ya romantic comedy na kuamua kuja na project nyengine itakayowakutanisha waigizaji wazoefu kama chae sira, kim sang joong, yoo dong geun itakayoangazia matukio ya nyakati za ukoloni wa japani nchini korea.
Si hilo tu pia MBC wameamua kupunguza drama za mwisho wa wiki kwa dhumuni la kuhakikisha wanajiandaa vilivyo kupambana na cable drama.
hmmmmmmmm!!!!!!!!!!!!!
muhudumu niongezee chupa za soju na bakuli tano za kimchi, jajjangmyeon pamoja na ramen nipate kushuhudia huu mpambano kati ya televisheni za wananchi dhidi ya televisheni za sekta binafsi.
nimesikia stori eti tajiri huzidiwa na serikali kimkakati na utoaji wa huduma, ndio maana shule za serikali ni bora kuliko shule za sekta binafsi zilizokosa hata vikalio vya wanafunzi
huku kwetu tukiangalia drama hatukai na mabisi (pop corn)
hivi huku kwetu ukiiwekea ngumu TBC unakutana na suprise gani vileeeeeeeee..................................................;'[-;;';[p-[[';[[==''[]=--&^9*($#@