Gyeoul
JF-Expert Member
- Jan 28, 2015
- 3,758
- 5,365
Bogoshipseyo Sana Sana!WAIKIKI SEASON 2Kwa wale wapenzi wa comedy season 2 ya waikiki imeanza rasmi siku ya jana, haijalishi hukubahatika kuangalia season 1 hii inakuhusu kuifuatilia.
unapaswa mbavu zako uzipeleke kwanza kwa fundi seremala apate kuziweka sawa zisije zikavunjika (ni amri na si ombi) kabla hujaingia kwenye ulimwengu wa waikiki.
aminas japokuwa bado unaendelea kusherehekea ushindi wa simba, na Taifa stars pindi utakapomaliza kugonga chupa zako za soju ya makonda naomba urudi kijiweni kwetu kabla sijachukia tafadhali.
Lee Yi Kyung a.k.a mzee wa gwenchanah gwenchanah ndiye muigizaji pekee aliyeshiriki season 1 na 2.
namnukuu director Lee Chang Min:
lee yi kyung amekuwa akija mara kwa mara ofisini kwangu, sikufikiria mara mbili kufanya maamuzi ya kumchagua tena kushiriki season 2. Kuhusu kuwachagua waigizaji wengine aliendelea kusema takribani waigizaji wote wana viwango vikubwa, nilitaka kuonyesha upande mwengine wa vipaji vyao vya uigizaji (comedy) na kiukweli nilikuwa nikiwagombeza mara kwa mara pindi wanapofanya makosa
View attachment 1054148
View attachment 1054149
lets go (가자 = gaja)
nimemkumbuka my beautiful chewbacca na style yake ya muharmusi fashion style
View attachment 1054150
hii taarifa nimeiona wakati ambao bando langu limebakia mb 350, pumbavu nitaitafuta magharibi ya leo inshaallah ep 1 pamoja na 2 kama itakuwa imeshawekwa subtitle na viki.
update:
episode 1 ya season 1 iliangaliwa kwa asilimia 1.7.
episode 1 ya season 2 imeangaliwa kwa asilimia 2.118.
tusisahau JTBC ni cable tv hivyo basi ni tofauti na mashirika ya umma kama vile MBC, KBS, SBS kwa kufuatiliwa, unaweza kukuta hata huko korea kuna watu ni mwendo wa TBC mchana kutwa.
Kutoingia Kwako Umu Sana Kumenifanya Nami Nikufate!...
Natumai Umzima!!