Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Hivi kuna mtu alishawahi kufikiria hii. Laiti Kama CCCM ingekuwa na Fitina na Figisu Kama za wakorea ingekuwaje Tanzania hii. Maana washikaji kukupa kesi ya treason tena ushahidi wa kutosha Ni rahisi sana yaani.
 
Mbona hata Tanganyika figisu zinafanyika/zimefanyika sana mkongwe..!
 
Hizi zote itabidi nizitengee muda,,,,,asante kwa kunipa mwanga.
 
😂😂 Usije ukawa kama Lee bangwon abaye aliachia madaraka wakati jeshi bado analiongoza.
 
Hii drama inautofauti wowote ule na ile ya Dae Jo Young??? Ama tofauti ni majina tu?
 
Jodong Jeong( Sambong) nipo ep 10, even SIX FLYING DRAGON haiufikii huo moto wa Sambong hata kwa chembe, kifupi hawa jamaa walimaliza kila kitu hivyo sidhani kama Great Seer inaufikia.
Nimefanikiwa kuangalia zote Six Flying Dragon na Jeong Do Jeon naweza sema Sambong wa kwenye Six Flying amefanya Vizuri zaidi kuliko wa Jeong Do Jeon. Sambong kwenye Jeong hakuwa na ushawishi mkubwa au strategist Kama Sambong kwenye six flying.
 
Hapana mzee Sambong wa Jeong do jeon ni great thinker, pia amechorwa katika uhalisia na changamoto alizokutana nazo katika harakati zake za kuanzisha Taifa jipya. Kule kwenye Six Flying Dragon Harakati zake hazikuwa na milima mikubwa.
 
Upi moto wa kuotea mbali kati ya hizo mbili? Mi nimetizama King Gwangaetto pekee nataka kushuka na Dae Jo Yeong baada ya kuisaka kwa mda mrefu sana bila mafanikio.
Ila Dae Jo young ndio ya kwanza kutoka 2006-2007, Gwanggaetto imetoka 2011-2012.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…