jana kabla sijafanya operation deletes kuna ujumbe fulani wa kimiujiza sijui hata ulitumwa na mjinga gani kuja kwangu, hatimaye ujumbe huo ulifanikiwa kunishawishi niiangalie
the tale of nokdu drama japo kwa njia ya uvivu kama samaki pono.
bingo, nilijikuta naiangalia hiyo drama kuanzia saa 12 jioni mpaka saa 8 usiku na nilipoamka kabla sijaosha uso wangu nikamaliza kiporo changu.
nimempenda bidada kim so hyun halafu ni mdogo wangu tuliozaliwa matumbo tofauti.
nimempenda jang dong yoon halafu naye ni kaka yangu tuliozaliwa matumbo tofauti.
kwa nini huyu mfalme gwanghae uhusika wake anapenda kutengenezwa kama ni mwanadamu aliyejawa na hofu inayoambatana na msongo wa mawazo?
mfano mwengine angalia
the crowned clown drama and movies
kwa mujibu wa maandiko ya kihistoria kabla ya kufa kwa mfalme seonjo alifanikiwa kuandaa document yenye kumtaja mrithi wake wa madaraka na kupitia document hiyo alimtaja gwanghae kama ndiye mrithi wake japokuwa hapakuwepo mahusiano mazuri kati ya baba na mwana, document hiyo baadae ilifchwa na wanasiasa ambao hawakuvutiwa na gwanghae, wanamrengo hao (magharibi) pia ndio waliongoza kampeni ya kumuondoa madarakani mfalme gwanghae.
ukisikia ubunifu na ufundi wa kutengeneza hadithi ndio huu:
ukiangalia hii drama hadithi yake imegeuzwa kidogo sana na historia kwa lengo la kumfurahisha mtazamaji na muda huo huo kumuelimisha kwa njia ya kioo kwa asilimia fulani bila ya kusahau kumshajihisha aitafute historia ya ukweli.
kwa mujibu wa historia kama nilivyogusia hapo juu mfalme seonjo kabla ya kufa kwake aliandaa document na kumkabidhi mtu wake wa karibu, document hiyo inamtaja gwanghae kama ni mrithi wake wa madaraka.
kwenye hii drama mfalme seonjo alikuwa na mtoto mwengine ambaye ni Grand Prince Yeongchang, kabla ya kufa seonjo aliandaa document na kumkabidhi mzee wake Dong-Ju (kim so hyun), kupitia document hiyo anamtaja prince yeongchang kama ndiye mrithi wake wa madaraka pindi atakapokuwa mkubwa na si gwanghae.
jambo hilo likapelekea watu wake wa karibu crown prince gwanghae waisake hiyo document popote ilipo na aliyepewa kazi hiyo ni vice chancellor yun, hatimaye yoon akafanikiwa kuipata document hiyo kwa mzee wake Dong joo.
ndio maana dong joo amekuwa na chuki dhidi ya mfalme na muda mwingi hutamani kumuua mfalme gwanghae kwa sababu miaka ya nyuma familia yake ilihukumiwa kwa uhaini kwa kosa hilo la kuificha document ya seonjo, sijui episode ya 12 itakuaje kwa sababu inaonekana mfalme ameshamfahamu dong joo na historia yake.
pia miaka 20 iliopita kuna mganga fulani alimwambia gwanghae ya kwamba mtoto wako aliyezaliwa mwezi november atakuja kubeba ufalme wako, kitachopelekea mtoto wake abebe ufalme huo ni ile nguvu inayotoka kwa mama yake na si baba yake, gwanghae kihistoria mama yake alikuwa ni concubine ndio maana hakuwa na nguvu kubwa sana mbele ya wanasiasa na mirengo yao. Kwa kuwa mke wake gwanghae anatokea kwenye koo zenye nguvu jambo hilo litapekea mtoto wake awe mfalme kuliko baba mtu ndio maana gwanghae akaona solution ni kumtelekeza mtoto wake ambaye ni nokdu. Malikia ameshapewa taarifa ya kwamba mtoto wake yupo hai na yumo ndani ya palace na wakati huo huo gwanghae na yeye ameshapewa taarifa ya kwamba mtoto wake yupo hai.
Je kipi kitatokezea hapo mbeleni, malikia atakubali tena kumpoteza mtoto wake kwa mara ya pili?
gwanghae atachukuwa hatua gani dhidi ya binti anayeitwa dong joo ambaye wazazi wake ndio waliokabidhiwa document yenye kumtaja mrithi wa mfalme seonjo miaka mingi iliopita?
kwa mujibu wa historia baadae anatawala mfalme INJO, na humu ndani huyu grand prince ndiye anatekeleza mipango ya kumpindua gwanghae, sielewi hii hadithi itakuwa na mrengo gani (either gwanghae ataondolewa madarakani kama ilivyo historia au gwanghae kwa msaada wa mwanawe nokdu atafanikiwa kuzima jaribio la kupinduliwa)
mwenzangu na mimi ichukue historia ya shujaa yeyote nchini kwetu halafu itengenezee hadithi yenye historia iliopinda ndani yake, huenda ukapingwa na muhimili mzito uliojaa roho mbaya mpaka ukatamani scripts ulizoandaa uzichome moto.
nataka nijaribu kuiangalia
EXTRAORDINARY YOU kabla shetani hajanishawishi niifute.
KBS 'The Tale of Nokdu' and MBC 'Extraordinary You', two currently on-going dramas that have captured the heart of the young generation in South Korea. Although their ratings may not be that high, but the response online tells otherwise
View attachment 1256547