dear brother,
sifahamu mfumo wako wa kimaisha ukoje ila unaonekana ni mwanadamu ambaye either uko bize sana jambo linalokupelekea ukose muda wa kufungua hata link moja, pengine una tatizo la kusahau au vile vile pengine ni mwingi wa dharau (sifa hizi mbili za mwisho Mungu akuepushe nazo).
umeomba nikutajie drama alizoigiza
ha ji won ila kwa wema wangu nimekuwekea link iliokusanya taarifa zake zote, cha ajabu unaniomba tena nikupe taarifa ya drama mpya aliyoshiriki au atakayoshiriki.
maana yake ni kwamba umenidharau na hiyo link niliokuwekea hujaifungua.
gwenchanah gwenchanah.
drama yake mpya inaitwa
chocolate na inatarajia kuanza kuonyeshwa mwishoni mwa mwezi November.
View attachment 1256713
musiendelee kuugeuza wema wangu kuwa ni utumwa, kuna siku
nitachoka, nitachukia na
baadae nitakimbia humu ndani tofauti na watumwa wale weusi walioendelea kuvumilia mateso yalioongozwa na mafedhuli baada ya kufungwa kwao minyororo jambo lililopelekea washindwe kukimbia.
bado sijachukia ila siku naona kama zinazidi kukaribia.