Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

yoo dong geun
huyu mzee nimeangalia project zake zifuatazo
  1. jang do jeon
  2. gu family book
  3. the banker
  4. athena goddess of war
  5. the most beautiful good bye in the world
mwaka 2020 nimejiwekea lengo la kuangalia korean family drama japo chache na ni zoezi ambalo limekuwa likinishinda mara kwa mara.
mwaka 2019 nilijaribu kuiangalia my only one drama na father is strange drama ila bahati mbaya zote kwa pamoja sikufika hata episode no 5.

nimepata mbinu mpya ya kuweza kunishajihisha kuziangalia family drama ila sina uhakika kama itakata kiu yangu, mbinu yenyewe ni kuangalia project za waigizaji wenye mvuto kwenye nafsi yangu.

hivyo basi nimeanza na yoo dong geun ahjussi, nimetafuta project zake mbili zenye maudhui ya kifamilia (marry me now drama na what happens to my family drama) na kila mmoja nimezitafuta episode 5 za mwanzo.

kama wewe ni mpenzi wa family drama basi zitafute hizo project nilizozitaja hapo juu, fahamu project zote mbili kwa miaka tofauti zimempa tuzo ya daesang (muigizaji bora wa mwaka) bwana yoo dong geun kupitia KBS drama awards.

View attachment 1384515

nikipata muda nataka kuihifadhi My Kids Give Me a Headache drama

  1. Shall We Live Together at Dramanice
  2. What Happens to My Family at Dramanice
  3. Childless Comfort at Dramanice
TWENDE NA FAMILY DRAMA......
Nimepata kuitazama What Happens to My Family? Kwa upande wangu nimeipenda.

Huyo mzee anaonekana ni mtu mstaarabu na mpole hususani katika malezi kwa watoto wake (katika drama lakini).

Ila upole nao una mipaka yake maana inafikia hatua ambapo watoto wako mwenyewe wanakuvuruga kiasi kwamba unaanza kujiuliza "hizi tabia za hawa watoto mbona hazifanani kabisa na zangu?" "Wamerithi kwa nani hizi tabia?"

Kesi zisizoisha na ugomvi kila leo.

Ni 'vurugu mechi' mtindo mmoja katika familia ya huyo mzee. Vituko vya hapa na pale bila kusahau umbea, kuna watu humo ndani siku kwao haipiti vyema bila ya umbea.

Ni drama nzuri yenye visa vya kufurahisha na pia kuhuzunisha.

Nakutakia utazamaji mwema kabisa wa hiyo project!
 
Nimeangalia muda huu imekua hivyo tutapata tabu sana mwaka huu
tokea juzi nikitembelea kissasian sikutani tena na video quality 360, ni mwendo wa video quality 720 kupitia server ya kissasian beta.

nikitembelea server ya FE nakutana na video quality ya 480 na 720.......
episodes 1 unaweza kuikuta imebeba MB 300 - 370
sad, sad, sad........

kukesha usiku kama mlinzi wa ikulu hakukwepeki tena kama unahitaji mzigo wa kutosha wa kuweka hakiba (store) kwa ajili ya mapambano ya corona.
 
Back
Top Bottom