Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Nimepata kuitazama What Happens to My Family? Kwa upande wangu nimeipenda.

Huyo mzee anaonekana ni mtu mstaarabu na mpole hususani katika malezi kwa watoto wake (katika drama lakini).

Ila upole nao una mipaka yake maana inafikia hatua ambapo watoto wako mwenyewe wanakuvuruga kiasi kwamba unaanza kujiuliza "hizi tabia za hawa watoto mbona hazifanani kabisa na zangu?" "Wamerithi kwa nani hizi tabia?"

Kesi zisizoisha na ugomvi kila leo.

Ni 'vurugu mechi' mtindo mmoja katika familia ya huyo mzee. Vituko vya hapa na pale bila kusahau umbea, kuna watu humo ndani siku kwao haipiti vyema bila ya umbea.

Ni drama nzuri yenye visa vya kufurahisha na pia kuhuzunisha.

Nakutakia utazamaji mwema kabisa wa hiyo project!
 
Nimeangalia muda huu imekua hivyo tutapata tabu sana mwaka huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…