Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kuna ileeee nimeisahau ya wamarekani na wakorea(ambao walikua wananyanyaswa na wajapani) haikua na romance ni historical
 
Nianzie wapi?
Nimekuwa kimya sana kwa mambo yangu binafsi ila haikunizuia kuendelea na mambo yetu haya ya Wakorea.
Nimechangamka kiasi mwaka huu sitaki mchezo, lol

Crash landing on you (Sikulala siku 3 hadi nilipoimaliza)
Hii ni moja Kati ya drama zangu bora kabisa za mwaka huu.
Nina muda mrefu kidogo sijavutiwa na couple za kwenye drama kama hii.
Hyun Bin almanusra amtoe Oppa Bae Ill Gook Sung β€˜kitini’ lol...

Kingdom 1&2
Nikiri wazi kama sikuiangalia na rafiki yangu basi nisingeimaliza, ni kali ila ile midamu hapana. Nimefumba macho mara nyingi sanaaa

Kwa drama za mwaka huu naendelea na Itaewon Class (hii nimeipenda) pamoja na Romantic Doctor nipo Ep 2 lakini kama siielewi hiviiii
Tell me what you saw nimeachia Ep 1 nayo sikuielewa japo yupo Daegil...

Drama nyingine nimemaliza Yi San, nikacheki na Terms of Endearment yote nikaanza Jumong maana niliimiss sikuimaliza nimeiweka kiporo nikimaliza za mwaka huu niendelee.

Miss y’all


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Guy's hi?

Wadau naomba msaada kidogo kuhusu ku download Korean drama online Mfano kupitia kissasian,dramanice na hata dramacool,

Shida ni kuwa Mbona kila nikijitahidi kutafuta sehemu ya kudownload kwa mb chache bado zinaleta kwenye Kuanzia mb 230 hadi 500?
Hakuna source ya kudownload online drama kwa chini ya 100mb?

Maana kwa mb hizo 230 na kuendelea nadhan nakuwa sijaambulia kitu,na unakuta episode yenyewe ni ya dk 28.

Naomba mnisaidie nifanyeje?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna chini ya mb 200 au zinakuwepo chache sana. Wengi tunatumia night bundle kuvuta episode zote
South korea
Hivi hawa wote ni north au south Korea?!
 
Nimechoka ku-download series. Tafuta jina la series unayoitaka, naenda nunua. Huku niliko 2000 per season. Nacheck "Kingdom" ni kama copy ya walking dead, ingawa inautofauti mkubwa tu.
 
Historical Drama za kisasa ( zilizotoka karibuni).
 
17/04/ 2020
siku 15 zijazo;
the king eternal monarch
drama πŸ™lee min ho and kim go eun)
ila huyu jamaa hanivutiii na style yake ya uigizaji (namchukulia kama ni overrated actor), itakuwa yule binti aliyeniambia anavutiwa zaidi na lee min ho kuliko mimi ndiye sababu kuu......

aliniambia lee min ho ana miguu mizuri, sura nzuri, pua nzuri isiyogusa virus wa corona....... lakini mwenzangu na mimi umejaaliwa miguu mibaya iliopinda kama bunduki ya mrusi, pua ndefu kama kisheti cha msibani, mdomo umejaa porojo kama katuni ya rango.

ok, ok nitapata mwengine mwenye upendo wa dhati atakayeheshimu madhaifu yangu.

=================================
baada ya takribani miaka 7 kupita hatimaye mwanamama kim eun sook anarudi tena ndani ya SBS, kutoka the heirs drama hadi the king and eternal monarch drama.

hii itakuwa ni mara ya pili kwa lee min ho kufanya kazi na mwanamama kim eun sook (mmoja kati ya waandishi waliojijengea sifa kubwa sana kwa muongo mmoja)..... the heirs drama
pia hii itakuwa ni mara ya pili kwa kim go eun kufanya kazi na mwanamama kim eun sook........ goblin drama


  1. Mr sunshine
  2. descendent of the sun
  3. goblin
  4. the heirs
  5. secret garden
  6. gentleman dignity
  7. n.k
umeangalia ngapi kati ya hizo?

 
Kiukweli hata mm min ho hanivutii na uigizaji wake....


Hizo drama hapo ulizozitaja nimeangalia zoote
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nne tu hapa
Lakin kama Mr. Sunshine ni yeye basi nitaiangalia tenaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…